Thursday, August 7, 2014

BARAKA KUMI ZA KORESHI
PASTOR JOSEPHAT GWAJIMA
Pastor Josephat Gwajima

Isaya 45: Haya ndiyo Bwana amwambiayo Koreshi, masihi wake,ambaye nimemshika mkono wake wa kuume,ili kutiisha mataifa mbele yake,name nitalegeza viuno vya wafalme;ili kufungua milango mbele yake,hata malango hayatafungwa. 
nimeiumba. 

Koreshi ni nani?
Koreshi alikua ni mfalme ambae hakua myahudi na baada ya wayahudi kuwa wamekaa utumwani siku nyingi yeye aliona ni vema kuwarudisha nyumbani, baba yake  mfalme Nebukadneza aliwachukua utumwani lakini yeye aliona si vema waendelee kukaa utumwani, akawaruhusu waondoke. Si jambo la kawaida kuwaruhusu watumwa kwenda nyumbani na kuacha kukutumikia.

Kwahiyo pamoja na kuwa hakua myahudi wala hakua katika agano la wayahudi lakini Mungu aliamua kumuita Koreshi masihi wake.
Hapa tunaanza kujifunza kumbe yule mtu anayetumiwa na Mungu na kuwafanya watu kupokea kile walichopoteza , yawezekana walikua na afya lakini wakapoteza, utajiri, mali au masomo lakini wakavipoteza  mtu huyo anaye wasaidia watu wa Mungu kuvipata walivyopoteza unaweza ukamuita Koreshi na Mungu anamuita masihi wake na anamstahilisha.
Koreshi alikua ni mfalme wa kawaida na ikafika mahali moyo wake ukamsukuma awaachie wayahudi waende zao kutoka utumwani, ni kitu kigumu sana kama ulipigana ukaliteka taifa na kuwafanya watu wa taifa hilo kuwa watumwa wako. Ilikua ngumu kwa Farao na ni ngumu hata kwa falme nyingine za dunia yetu ya leo.
Baada ya kitendo hicho Mungu akamuita Koreshi masihi wake au mpakwa mafuta wake. Sasa mtu yeyote ambaye anafanya kazi kama ya Koreshi zipo baraka za Mungu zinaambatana na yeye na familia yake.
Zipo Baraka kwa mtu wa Mungu ambae amejitolea kuhakikisha anawaweka huru watu wa Mungu kutoka kwenye shida mbali mbali.
Wakati mwingine mtu anaweza kutafuta njia za kufanikiwa kwa kutumia nguvu nyingi, lakini mafanikio na Baraka za Mungu zinakuja pale unapoaamua kujitoa kusaidia wengine na kuwaweka huru.

Kama kuna kitu cha muhimu hapa duniani basi ni mwanadamu, na kila kitu unachokiona leo ni kwaajili ya mwanadamu, na kila kitu unachokiona pasipo mwanadamu hakina thamani. Watu wanakua madaktari kwaajili ya wanadamu, wanakua waandisi kwaajili wa wanadamu, magari, majumba hata spika hazina thamani bila uwepo wa binadamu.
Jaribu kuwaza leo duniani hakuna mtu spika ni ya nini?
Kwahiyo watu ni wathamani na ni vizuri kuuthamini utu wa mtu wakati angali bado anaishi, kwasababu hatuwezi kufanya chochote kwa mtu anapokufa na ndio sababu unaona mtu anapokufa watu wanatoa hotuba nzuri kwenye misiba, hotuba inayotolewa msibani hata kama ni nzuri kiasi gani inakua haina thamani kwa aliyekufa ni kwaajili ya wale waliohudhuria msiba, hii ndio sababu tunatakiwa kuuthamini utu wa watu wakati bado wako hai.


Jaribu kuwaza mtu alikua na matatizo na yuko nyumbani na alikua hajawahi kuwaza kwamba masaada wake anaweza kuupata kanisani, na wewe ulipomualika kuja kanisani mtu huyo anapokea muujiza wake, hakuna jamnbo ambalo mtu huyo anaweza kukulipa ndio sababu Mungu huwa anayo Baraka maalumu unapowasaidia wengine na kuwafungua wengine.

BARAKA ZA KORESHI
a)      Koreshi ameshikwa mkono wa kuume na Mungu. Isaya 45:1
Mmoja wa watu waliofunguliwa kutoka katika vifungo vya Ibirisi
Unaposema mtu ameshikwa mkono na Mungu inamaanisha huyo mtu hana Baraka zinazotokana nay eye bali zimetoka kwa Bwana. Kila anachofanya ni Mungu amefanya kila anachogusa ni Mungu amegusa, akikuonya ni Mungu amekuonya, nguvu za mtu huyo zinakua ni nguvu za Mungu.
Kwa kadiri mtu anavyojihusisha na kufungua watu ndivyo Mungu anavyojihusisha na kukubariki katika maeneo mabli mbali.
wakati mwingi inapofika wakati wa kuwasaidia watu mara nyingi watu wa Mungu wanakuwa wabaguzi, wanachagua wa kuwasaidia, lakini kama unataka Baraka za Mungu wafanye watu wote kuwa na thamani sawa, mwenye kazi sawa na asiye na kazi, meneja au asiye na kipato wafanye wote kuwa sawa, awe ni waziri, mbunge, au mtoto mdogo wote wahudumie sawa.
Na unapokutana na mtu msaidie kana kwamba utamuhitaji kesho, ongea nao kana kwamba kesho yako inawategemea hao na kwa kufanya hivyo Mungu anaachilia Baraka zake katika maisha yako.

“Ni maombi yangu Mungu akuishike kwa mkono wake wa kuume unapowaheshimu na kujihusisha na maisha ya watu wake kwa jina la Yesu”
b)      Ili kutiisha mataifa mbele yake. Isaya 45:1
Jambo hili kwa ulimwengu wetu si wazi sana, unawaza utayatiishaje mataifa.
Mwanzo 1:26..Akawaambia zaeni mkaongeke mkaijaze nchi nz kuitiisha.
Kutiisha maana yake kuwafanya wafuate unachosema, ni mamlaka ya kusema na kikafuata kile ulichokisema na kutii.
Unapojihusisha na kuwafangu awatu wa Mungu kuna wakati unapata usumbufu kutoka kwa hao watu kwasababu inahusisha maisha yao, lakini iko Baraka ya kutiisha mataifa inayotokana na kuwasaidia watu wa Mungu.
Mungu anakawaida ya kuwageuza watu wanaomtumikia kutoka kwenye yale maisha ya hali ya chini na ya dharau na kukugeuza kuwa kitu bora, ubora ule ambao ulikua umefunikwa kutokana na shida na misongo mbali mbali ya maisha.
Kile ambacho elimu haiwezi kutoa Mungu anaweza kutoa. Kuna watu ambao wanawaza kuwa hawawezi kufikia mafanikiofulani katika maisha kutokana na kiwango chao cha elimu walichonacho, lakini ni vizuri kugundua elimu ni jambo moja na mafanikio ni jambo linguine, yako maarifa ya kufanikiwa kutoka kwa Mungu, utajiri kutoka kwa Mungu na upenyo utokao kwa MUngu ndio sababu unaweza ukakuta profesa lakini hajafanikiwa katika maisha yake.
Ndio sababu ni vizuri kila mtu akaingia kwenye kazi ya kuwafungua watu wa Mungu, kufungua taifa, kufungua ndoa zilizofungwa ili Baraka za Koreshi ziambatane na maisha yako kwa Jina la Yesu.

Siku moja nilikua na mkutano karibu ulaya yote, nikafanikiwa kufika mpaka kisiwa cha PPatmo ndani kabisa. Nilipofika kule nikakuta watu wa aina yangu hawapo kabisa kule, watu wa kule wakaanza kushanga mbona hamna watu kama wewe huku, nikawaambia yuuko aliyenifikisha huku, nyie mmetumia njia zenu za kawaida na utaratibu wa kibinadamu kufika huku lakini mimi nimekuja kuweka mateka huru, nilijua kuna magereza ya kiroho, magereza ya magonjwa, magereza ya dhambi na shida na wanatakiwa kuwekwa huru kwa jina la Yesu.
Kipindi ambapo unaona maisha ni magumu na huoni pa kwenda fahamu jambo moja, uko ufunguo, neon la Mungu ndio ufunguo.
Mungu anaweza kuyafanya mambo yote yaliyoshinmdikana yakawa sawa, Mungu anaweza kuifanya huzuni yako kugeuka na kuwa furaha, Mungu anaweza kugeuza msiba wako na ukawa shangwe, Mungu anaweza kugeuza mauti yako na kuwa uzima. IKIWA MUNGU YUKO UPANDE WETU NI NANI ALIYE JUU YETU?
Iko mamlaka ya ya kawaida ya kibinadamu na iko mamlaka ya rohoni pia. Na mamlaka ya rohoni iko ya upande wa Mungu nay a upande wa shetani.
Ndio sababu wako viongozi ambao wanamtumikia shetani anawapa mamlaka ya kishetani na anaposema jambo kila mtu analitii hata kama ni jambo baya na anakua hana mtu anayeweza kumjibu.

Na pia kuna mamlaka ya roho upande wa Mungu ambayo mamlaka hiyo alipewa Adamu, Mungu alimwambia nimekupa mamlaka utawale vitu vyote, na shetani akaja akamnyang’anya mamlaka hiyo.
Kwakua Mungu anakua anaishi ndani yetu tunakua na sehemu ya uungu ndani yetu na ile mamlaka ya kutiisha na kutawala inakua ndani yetu.
mfano ukichukua jiwe ukalifunga ndani ya gazeti hakulifanyi lisiitwe jiwe au uweza wake wa kuumiza hautaweza kudhihihika kwasababu tu limefungwa ndani ya karatasi, hapana. ndivyo ilivyo kwetu Mungu yule aliyeumba mbingu na nchi na vyote anakaa ndani yetu na uweza wake ule ule uko ndani yetu bila kupungua kwa namna yoyote.
Adam baada ya kutenda dhambi ule uweza wake shetani akauchukua na kuanza kuutumia, ndio sababu Yesu alipokuja akamnyang'anya shetani ule uweza na kulikabidhi kanisa.
Lakini leo Yesu anashangaa ametupa nguvu lakini hatujui kama tunazo, ametupa nguvu lakini hatujui kama tunazo. ndio sababu wakati huu wa mwisho tutaenda kuona udhihirisho wa nguvu usiokua wa kawaida kwasababu kwanjia ya roho mtakatifu tataona udhihirisho wa nguvu hizi wa namna isiyokua ya kawaida.
Ndio sababu baadhi ya watu huwa wanauliza mbona nyie mnaongea kwa kujiamini? ni kwasababu ule uweza wa kutiisha uko ndani yetu na unatenda kazi kwa jina la Yesu.
wakati niko japani niliona maono ya ajabu wakati nimelala usiku.
nilikua nimelala usiku kitandani ghafla nikajiona nimefika kwenye kikao kimoja kimejaa wazee wa kijapani, lakini katika maono hayo nikajiona na mimi nimekaa hapo katika hicho kikao.
wakaaanza kujadili wakisemezana kuwa Budha ameanza kuishiwa nguvu, wazee wale wakatengeneza sanamu yenye mfano wa Tembo na wakaanza kuiongelesha kijapani wanaiambia ile sanamu amka Budha amka utiwe nguvu amka tunataka kushindwa, ghafla yule mnyama akaamka na akaanza kukimbia kwenye ule uwanja kwa maringo huku akiruka juu, wale wazee wajapani wakaanza kufurahi na kushangilia maana Budha ametiwa nguvu.
Gafla nikajiona nimetokea katika ule uwanja nikamuamuru yule mnyama huku nikisema kwa jina la Yesu. Yule mnayma aliponiona akaanz akunifuata sehemu nilipokua, wakati huo mimi nikiendelea kusema kwa jina la Yesu, huku akizidi kuja. Moyoni mwangu nikasikia sauti inaniambia huyo mnyama anaendelkea kuja kwasababu anajua akikaribia karibu na kabla kitu chochote hakijatokea wewe utakimbia. Akanikaribia kabisa nikamshika pembe na kumuamuru kwa jina la Yesu tii, baada ya kumuamuru atii akageuka n kuwa mwanaume wa kijapani akageuka na kuanza kukimbia, na mimi nikaanza kumkimbiza, na wale wazee wengine walipoona hivyo wakaanza kukimbia.

Ndipo Mungu akaanza kunifundisha kumbe kuna  mapepo ambayo yamepokea kafara na kufikia hatua ya kuwa kama miungu na kama binadamu, na hao wanatakiwa kutiishwa. na hii ndio baraka aliyopewa Koreshi ili kutiisha mataifa kwa jina la Yesu

Dada aliyekua hawezi kutembea kabla akifurahi baada ya uponyaji

ITAENDELEA 

2 comments:

  1. mungu yuko upande wako
    gwajima ulipo kuja tanga uli tuponya watu wa tanga

    ReplyDelete
  2. Inapendeza ninapoyaona mambo haya hakika Mungu wetu ni mkuu sana.Inabariki sana.

    ReplyDelete