google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

IBADA YA KUSIFU NA KUMSHUKURU MUNGU KWA MAMBO MAKUBWA ALIYOTUTENDEA.



IBADA YA KUSIFU NA KUMSHUKURU MUNGU.

03 - 08 – 2014











John Lisu
Ni ibada ya kusifu ambapo waimbaji mbali mbali wapo ndani ya bonde la kukata maneno Ibada imeanza na kundi la John Lisu wakituumbuza kwa nyimbo zao nzuri.









Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima:
 
Tunamshukuru Mungu Kwa  mambo matatu.
1.       Tunamshukuru Mungu kwa Helicopter ambayo imefika jana tarehe 2-8-14 lengo la kununua hericopiter hii ni kwa ajiri ya kuihubiri injiri katika mikoa yote kama tulivyoanza na Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, kilombero, na sasa tunaanza na Iringa, Njombe, Songea, Mbeya, Sumbawanga, Katavi, Kigoma, Kagera, Geita, Mara, Simiyu, Shinyanga, Kahama, Tabora, Singida, Dodoma hapo tutakuwa tumemaliza awamu (phase) ya kwanza. Awamu ya pili tutakwenda mikoa ya Lindi na Mtwara pamoja na Zanzibar. Baada ya hapo tutakwenda  wilaya zote, Tarafa zote, kata zote na vijiji vyote.
2.       Mbunge wetu wa kawe alituomba tusaidie shule za msingi kama kuwapatia madawati na umeme katika shule hizo.
3.       Ni mwaka wa tano tupo hapa kawe hivyo pia tunamshukuru Mungu kwa hilo.

Wageni wetu rafiki zetu tulionao leo ni hawa wafuatao:





Faustine Munishi na malebo, Rose Mhando, Tunajivunia vya kwetu  ni vizuri kuwatambua watu wangali wakiwa hai. Pia tuna John Lisu, Flora Mbasha, mwanapinduzi, chengula, mabisa ema jacksoni Benti, david Robart,
 
 upenndo nkone, Christina Shusho, Bon Mwaitege, watanzania tuna vitu vizuri tulivyopewa na Mungu, Mahanaimu Soundi hii ni bend mpya  (mwanzo 32:1-2)
1 Yakobo akashika njia yake na malaika wa Mungu wakakutana naye.
2 Naye Yakobo alipowaona, alisema, Hili ni jeshi la Mungu. Akapaita mahali pale, Mahanaimu.
Sisi ni watanzania hatuna chama sisi ni watanzania. Pia tuna Bend ya Jeshi la Magereza Tanzania
Serikali tatu ndo msimamo wetu Ufufuo na uzima maana tunaserikali tata kwa sasa maana sasa tuna serikali ya Zanzibar naya muungano na ya Tanganyika haipo Hivyo tunahitaji serikali ya Tanganyika nayo iwepo.
Kama kawaida yetu wimbo wa Tanzania unaimbwa na bendi yetu ya magereza.
Mahanaimu Sound na wimbo wao wa Utukufu kwa Bwana nao walikuwepo.
Baada ya hapo Mwenyekiti wa Mtaa wetu ndugu Hasani Ngonyani naye atusalimie Mheshimiwa mwenyekiti ametaja mwenyewe ipo siku ataokoka na anawaheshimu sana viongozi wa dini na hivi karibuni ataokoka na haya yawe kwake kwa jina la yesu.
 
Rose Mhando naye tunamkaribisha kwa nyimbo zake. Rose mhando anatoa somo na anasema kumiliki ni haki yetu hivyo tung’anga’anie kwa Mungu ili atubariki. Rose anasema kwake ni Unabii kwa maana anasema leo anazindua albamu yake ya kamata pindo la yesu akianzia ndani ya bonde la kukata maneno kawe kama alivyozindua nibebe miaka ile. Pia anamwambia mwenyekiti hasani kuwa hajakosea kusema kuwa ataokoka hivyo asiwe na wasiwasi maana amechagua fungu lililo jema kwani hata yeye alikuwa mwisilamu.
 
Sasa ni wakati wa kumsikiliza Mbunge wetu wa jimbo la kawe aseme machache mheshimiwa Halima Mdee mwanamke Jasiri Afrika kwa maana siku chache hivi karibuni amechaguliwa kuwa mwanamke jasiri kati ya kumi namoja waliokuwepo kwenye kinyang’anyiro hicho.
Mbunge anamshukuru mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima
Anasema hajazoea kusema neno kwenye madhabahu hivyo anatetemeka hivyo ananukuu kitabu cha isaya 43:18-19
18 Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani.
19 Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka. 
Anasema helicopter ni chombo cha gharama nafuu sana na kinawezesha watu wengi kulipata neno kwenye mikoa yote na vitongoji vyote. Pia anaghusia magazeti ya udaku  na anasema yataandika sana lakini nyinyi songeni mbele. Na anasema tutaweza kuongeza chombo kingine ili kazi ya Mungu iendelee mbele. Anasema asante kwa mwitikio wa kanisa la Ufufuo na uzima kwa kuwapatia madawati wanafunzi wa shule za msingi  kawe .
Hatimaye Halima achangia Milioni kumi kwa kazi ya Mungu katika kuwapatia shule za msingi madawati.  Kitu cha msingi kuliko vyote ni kusema nimepiga hatua. Anasema Mapato ya kinondoni kipindi kile ilikuwa bilioni 9 baada ya miaka 3 yameongezeka mpaka bilioni 40 na wanataka yafikie bilioni 100 ingawa safari ni ndefu lakini kwa uwezo wa Mungu tutashinda.
Kuhusu jimbo tumefanikiwa kupata miradi mbalimabali, tumejenga Barabara za rami na mambo mengine hata wao wanaamini neno. Na kwa neno tutafika.
Ameleta tena salaam za majadiliano ya kuhusu katiba mpya. Kwa mara kwanza ni katiba inayohusisha mawazo na maoni ya watanzania wote . salamu kutoka Ukawa wanawasalimia wamesema ipo  siku chembe chembe ya kuwa na katiba , yakutaka kuwa na taifa lenye neema, ya kutaka kuwa na viongozi wazalendo, yakutaka kuwa na Tanzania mpya itafika. Wao ukawa watarudi mbungeni kama maoni ya wananchi yataheshimiwa. Mwisho anawaasa watanzania wasiache mchakato uendeshwe na wanasiasa peke yao hivyo kila Mtanzania ashiliki ili kutoa mwelekeo wa taifa, wa rasilimali za taifa zigawanywe kwenye mgawanyo halali kwa wantanzania wote. Tukiwa na katiba bora inayotoa mwongozo bora kwa mgawanyo wa kweli na watanzania tujidhatiti ili kuokoa kizazi kijacho  Mungu awabariki sana! Hayo
Makofi kwa yesu.
 
Flora Mbasha na wimbo wake wa utukufu kwa yesu.









 
 Upendo Nkone na wimbo wake usifurahi Juu yangu ewe adui yangu.














 Chrisitina Shusho.


John Lisu apata gari Jipya
"John Lisu ni kama Don Moen wa Tanzania, na ni mtu anayeubariki sana moyo wangu, ni vizuri kujifunza kuwatendea mema watu wa Mungu ambao Mungu anawatumia kuyagusa maisha yetu, na kwasababu John Lisu amekua akitumiwa na Mungu kutugusa kwa namna ya ajabu tunamzawadia gari jipya siku ya leo" Dady Josepha Gwajima






.
 Bon mwaitege. Anashukuru sana kuwepo kwenye madhabahu hii.


Faustine Munishi anaelezea habari za malebo anaeleza kuwa ni rafiki yake wa tangia utotoni walisoma pamoja na walikuwa pamoja na sasa malebo naye ameokoka.






mwanamapinduzi.





SOMO KWA UFUPI:
JINSI MTU ANAVYOWEZA KUIBA NYOTA.
NA MCHUNGAJI KIONGOZI.
MANENO YA MSINGI Mhubili 10:5-9, Ezekieli 13:19-21

Mhubili 10:5-9
5 Liko baa nililoliona chini ya jua, nalo ni kama kosa litokalo kwake yeye atawalaye;
6 ya kuwa upumbavu huwekwa mahali pa juu sana, nao wakwasi hukaa mahali pa chini.
7 Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa.
8 Mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake; Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.
9 Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo; Naye apasuaye miti huona hatari katika hiyo.

 Ezekieli 13:19-21
19 Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo.
20 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege.
21 Na leso zenu nazo nitazirarua, na kuwaokoa watu wangu katika mikono yenu, wala hawatakuwa katika mikono yenu tena kuwindwa; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.
Hapa anasema kuwa kuna watu ambao walitakiwa kufa lakini hawajafa na kuna watu waliokufa hawakutakiwa kufa.

Kuna kitu kinaitwa nyota ukisoma kitabu cha mathayo 1:1-2 kinaandika habali za nyota iliyoonekana mashariki.
1 Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,
2 Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.
 kwa habari ya nyota tunaweza kujifunza yafuatayo:
1.        Kila mtu ana nyota
2.        Numbe nyota inaweza kufuatwa
3.        Nyota ya mtu inaweza kuonekana.


NYOTA NI NINI?
Nyota ni ule uwezo au kipawa  cha mtu kutenda kazi na uwezo huo unaonekana kabla hata mtu hajazaliwa
Kuna wengine nyota yao imewekwa kwenye siasa wengine kwenye utawala na wengine kwenye biashara na kadhalika.
Kuna wengine nyota yao ipo kwenye  uso unaweza ukamwangalia tu unampenda au unataka kuongea nae, wengine darasani wengine biashara.
Shetani hakuumba chochote hivyo kwa kuwatumia wachawi na waganga kuchukua nyota za watu na kuwapa wengine wanaoshirikiana nao kwenye mambo ya kishirikina na mtu aliyechukuliwa nyota yake wanamwachia mapepo na kumwacha na taabu.

Angalizo kila mwanasiasa ambaye hana Mungu ana mganga wake wa kienyeji hakuna ambaye hayuko huku wala kule (neutral)  hivyo hao wanaoiba nyota lazima wapigwe kwa jina la Yesu. Sasa mamajusi wa mashariki Wakaiona nyota, lile neno mamajusi maana yake ni wataalamu wa anga (Astrologers or Magician) waliotoka mashariki ya mbali ambayo leo ni Uchina na Korea na sehemu za Japani wakaona nyota ya mfalme amezaliwa mashariki ya kati. Wakaja kutoa zawadi uvumba na manemane.

Maana yake nini sasa wale mama jusi wakasafiri mpaka Jerusalemu wakiifuata ile nyota
Ndiyo maana unaweza ukamuona mtu ni maarufu kumbe ni mtupu tu, ana nyota za watu
Hatuishi kwa majini wala mapepo hivyo mtu anayesema na kufundisha habari za nyota kwenye redio na television kama shehe Yahaya huyo mtu anafundisha uchawi hivyo hatufai mtu huyo.
Kwa dakika hizi chache nataka kuamuru nyota ya kila mtu irudishwe kwa jina la Yesu.
Wengine wana nyota za mvuto  wengine wana nyota za kupendwa .

Neno la Mungu ni nyundo ivunjayo mawe vipande vipande.  Unakuta mtu anatumia nyota za watu anajichukulia umaarufu na kuonekana ana maana sana kwenye jamii.  kwa  yule ambaye nyota yake  imechukuliwa kama alikuwa anapendwa anaonekana hapendwi tena.
Kwa mfano Tanzania yenye Mlima Kilimanjaro ambao ni  mrefu kuliko milima yote Afrika, yenye ziwa kubwa kuliko maziwa yote ulimwenguni na ziwa lenye kina kirefu kuliko yote afrika na madini ya kila aina halafu leo shule zikose madawati na umeme kwa nini Tanzania nchi yenye Dhahabu. Hili ni tatizo la akili watu wanashindwa kutumia mali tulizonazo lakini jiulize Japani hawana chuma lakini ndiyo wanaongoza kuuza magari.
Tanzania mpya inakuja kwa jina la yesu.

Tanzania ni nchi ya watu wote na kiongozi asiyewasaidia watu hawa hafai kuwa kiongozi wetu nitaendelea kusema ‘’ Tanzania mpya inakuja’’
Unakuta mtu anahangaika kila siku kumbe wanaitumia nyota yake kwa kazi zao
Kuna aina nne za mashetani:
1.       Majoka - hawa ni wale malaika waliotupwa kutoka mbinguni pamoja na shetani
2.       Majini - ni mashetani wanaoendana na mila za kiarabu
 3.   Mizimu - ni mashetani yanayofuata familia ndio maana unakuta familia zina mambo
         Yanayofanana. 
                4.Miungu – Hawa wanatawala japani na nchi za mashariki ya mbali.
Ulimwengu wa Roho ni dhahili hivyo shetani anaweza kutumia wachawi na wanganga kufanya kazi yake ya kuuwa na kuharibu na kuchukua nyota za watu. Nyota ikichukuliwa maisha yako yanaanza kuharibika hapo, unaanza kitu unaacha wachawi wana uwezo wa kukufanya uache kazi, biashara familia mke au mme.
Unakuta mtu yule aliyekuwa kilaza darasani ndo anaamua hatima za watu.
matendo13:16
elimu ni taa ya kumulika mafanikio katika maisha kulingana na uwezo ambao Mungu amekupa hivyo ni uwezo wa kuendeleza kipawa chako ulichopewa na mungu maana kuna kitu ulichopewa. Hivyo kila mtu ana kitu chake ndani ambacho amepewa

UKIRI
‘’Sema nakataa, sema nakataa, sema nakataa sema tena nakataa’’ kwa nini tunasema nakataa kwa sababu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu hivyo kila tunachosema kinatokea hivyo kila jini kila mzimu unaoshikilia nyota za watu achia kwa jina la Yesu kila kiongozi wa kisiasa unayetumia nguvu za kichawi  na kung’oa kwa jina la yesu.
maelfu wakiponywa katika shida zao
Shika kichwa chako sema kwajina la yesu kuanzia leo aliyeiba nyota yangu nakuitumia awe kiongozi, awe shehe au imamu rudisha nyota yangu kwa jina la yesu.
Kwajina la yesu natumia uwezo wa jina la yesu kila mtu aliyeweka mkono wake kichwani na anasoma neno   hili naamuru katika jina yesu naamuru nyota yake irudi kwa jina la yesu.
Sema maneno haya ‘’Baba kwa jina la yesu naomba leo mahali nilipofungwa unifungue fungua maisha yangu leo’’
‘’Damu ya yesu inifungue sasa kwa jina la yesu’’.
Nakuamru ewe jini uliye ndani ya mtu huyu toka kwa jina la yesu.   
Yesu yu hai leo wewe jini unayemshikilia achia mwili wake  ewe jini uliyechukua nyota yake ya kazi, ya kupendwa, ya safari mwachie atembee kwenye Baraka zake katika jina la yesu  naagiza wewe usitembea tembea usiyesikia sikia usiyeona ona kwa jina la yesu.
Naomba ulinzi kwa watu hawa walionyosha mikono yao bwana yesu gusa mikono yao. Na kila aliyepanga kukuua afe yeye kwa jina la yesu naamulu uzima kwa jina la yesu.

               

Post a Comment

1 Comments