Sunday, August 31, 2014

JE WAJUA MWANADAMU ANAWEZA KUIBIWA NA MWILI WAKE KUENDELEA KUISHI?
JUMAPILI YA TAREHE 31/08/2014
SOMO: BIHASHARA YA ROHO NA MIILI YA WATU
MCHUNGAJI KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA
Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima akisoma Neno la Mungu.
UFUNUO18: 11 Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena;
12 bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari;
13 na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng'ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wanadamu.
Biblia imetupa ujumbe kwamba kuna wafanya bihashara wa nchi wanalia kwamba hakuna wanunuaji wa bidhaa zao kwamaana kuna miili na roho za binadamu hazinunuliwi. Duniani leo kuna kilio kwamba kuna wanadamu wanasafirishwa kwenda kuuzwa ni wengi wanatoka nyumbani kwao na wanakuwa wanapaspoti lakini hawajui wanakwenda wapi wanakuwa wanamkubwa wao ndiye anaye wapeleka . hapa kuna jambo limetendeka mpaka huyu anayenunua bidhaa anasema sitaki tena na Bibia inasema dunia na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana na shetani ni mwizi hana chakwake ni mtumiaji tu na mwaribifu.
Hapa unaanza kuelewa ile Isaya 42:22 ndio maana Yesu kwenye luka 4 huduma yake ya kwanza akasema Roho wa Bwana yu juu yanguu na alimaanisha nina kazi ya kutenda na Roho wa Mungu yu juu yangu na akasema kwa maana nimekuja kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao na huu ni ujumbe watu wengi hawaupendi kwamaana ni ujumbe wa aibu. Ndio maana Yesu anasema Roho wa Bwana yu juu yangu kwamaana ameenitia mafuta niwatangazie wafungwa kufunguliwa kwao. Kwahiyo Biblia inasema wafanya biashara wa roho na miili ya binadamu na watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa wamenasa katika mashimo, wamekuwa mawindo.

Mchungaji Josephat Gwajima akifundisha.
2wakorintho12: 1 Sina budi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia maono na mafunuo ya Bwana.
2 Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.
3 Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua);
Hapa inatupa picha kwamba mtu anaweza kuwa ndani ya mwili au nje ya mwili. Mtu ni Roho inayokaa ndani ya nyumba inayoitwa mwili. Na nyumba hiyo inaweza kuwa ni nyeupe au nyeusi na kifo ni bomoabomoa inayomwondoa mtu aondoke kwenda mahala pakee kama ameokoka anaenda rahani pake au kama hajaokoka anaenda kuzimu. Na mwanadamu akiwa nje ya mwili tunasema amekufa na akirudi ndani ya mwili  amefufuka. Paulo anasema anamjua mtu mmoja ambaye alitolewaa nje ya mwili na akapelekwa mpaka mbingu ya tatu akasikia maneno yasiyotamkika ambayo haijuzwi mwanadamu ayanene. Na anajisifu juu ya mtu huyo ambaye ni yeye.
Mchungaji Josephat Gwajima.
Ezekieli37:
Yaani akatolewa nje katika roho ya Bwana akawekwa katika bonde lililo jaa mifupa akaambiwa atabiri juu y mifupa ile. Alikuwaa ni nabii akapelekwa kwenye ulimwengu wa roho akaonyeshwa bonde lililojaa mifupa mikavu. Kutoka hapo tunajifunza kwamba mambo hayo  ambayo Ezekieli alionyeshwa ni taifa la Israeli kwamba watakuja kutawanyika na baadae kurudi tena na mana ya pili ni kanisa lililo kufa duniani halina nguvu tena halina uwezo tena limekuwa dini na litaanza kufufuka tena na Ezekieli akauambia upepo uje  ukawaingia watu wakaamka.

Ufunuo1:9-9 Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu.
10 Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,
11 ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.
Yohana alikuwa katika Roho akatolewa nje ya mwili akamwona Yesu na kumbe kuna ulimwengu wa rohoni na ulimwengu wa mwilini, kuna maneno ya rohoni na maneno ya mwilini, ukishinda rohoni unashinda mwilini, na ukipigwa rohoni unapigwa mwilini. Biblia inaposema miili na roho za watu ni kwamba mtu unakuwa umelala na unaamshwa lakini hujui unauacha mwili wako wewe unakuwa unawafuata na mwili unauacha nyumbani na hapo unakuwa umeibiwa. Kwa kawaida roho inapo tolewa ndani ambayo ni wewe unatakiwa mwili ufe lakini wachawi wanapokuja kukuiba wanaacha roho ya mapepo au ya jini ili mwili usife na wewe unapelekwa kwenda kuuzwa kwenye bihashara za kichawi na kwanini wanakuchukua wewe uliye roho ni kwasababu wewe ndiye mwenye vipawa una ujuzi wote una kila kitu na wanaenda kukutumia. Ndio maana watu wanaporudishwa wanasema walikuwa kwenye mashimo au kwa baba mdogo au kwa bibi analima lakini ni mtu ni binadamu anakuwa ametolewa ndani ya mwili wake na mwili wake umeeachiwa joka au jini. Na mnakuwa mnashangaa mtu ameanza kufanya mambo ya ajau kumbe sio mtu. Sasa mwili wake unakuwa unatumika na roho yake inatumika unashangaa mtu anafanya kazi ya ajabu lakinni analipwa elfu ishirini na ukimwombea ataonekana ana mashetani yanasema naungua na hata Mungu hataki atoke maana akitoka huu mwili unakufa  sasa unatakiwa umrudishe aliyeibiwa alafu ndio umtoe joka aliyeingizwa ndani.
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima.
Unaposema shimo kuna mashimo ya mwilini na mashimo ya rohoni, kwa nini lusifer anawanunua hawa watu kwaajili ya kazi zake ni kwamba mashetani wote majini wote mapepo wote wameshalaaniwa kwa hiyo anawatumia hawa wanadamu kwasababu mwanadamu hajalaaniwa ndio maana watu ndio wanaojenga ufalme wa mashetani. Na unaweza kujiuliza kwanini hawa watu wanakuja kwenye mikutano ni kwasababu Mungu anataka roho za watu zirudi kweye miili yao na malaikaa wanawakusanya hao mashetani walio kwenye hiyo miili bila wao kujua na tukisema njooooooo watu wenye miili wanatoka kwenye mashimo yao na kurudi kwenye nyumba zao kwasababu hii ni saa ya mavuno.-
Kwa hiyo unakuta roho ya mtu haipo na hawa ukiwakuta wana magonjwa wana matatizo na unakuta kahaba anajiuza anatumika kuingizia watu hela kwa kuuza miili yao lakini wanakuwa sio wao wanaofanya hiyo kazi bali ni majoka, mashetani yalio ndani yao na roho zao zimeibiwa. Dakika hii kuna watu hawapo na shetani anaangalia kuna watu wanavipawa vizuri walivyo pewa na Mungu. Shetani anawaiba ili kuvitumia vipawa hivyo kwamaana kwa kawaida hawezi kutengeneza vipawa hivyo.

watu hawa walikuwa wameibiwa toka kwenye mili yao na kufichwa.


Inawezekanaa kuna mtu amekaa ana magonjwa ana matatizo kumbe tatizo lao ni hawapo wameibiwa. Yesu alipoeenda kumfufua lazaro alienda akasema lazaro njooooo na Biblia inasema lazaro aliyekufa siku nne akafufuka danieli nae alitupwa kwenye simba na mfalmle akahangaika usiku kucha na assubuhi  yake akaenda akamwita danieli ewe mtu wa Mungu na danieli akasema nipo. Na leo kipawa chako, kazi yako, elimu yako, biashara yako, imefichwa na kuna sauti ipo inaviita vilivyofichwa vitaitwa kwa jina la Yesu.
Biashara ya roho na miili ya watu kuna watu wengine wanachukuliwa kwa kufa lakini wanazika gogo, wengine wanachukuliwa mzima mzima anaeenda kulimishwa mashambani bila yeye kujijua, na wengine ndio hao wanaochomolewa kwenye miili yao. 
Binti akielezea jinsi alivyoisikia sauti ikimwita njoo kutoka baharini.

Luka7: 21 Na saa ile ile aliwaponya wengi magonjwa yao, na misiba, na pepo wabaya; na vipofu wengi aliwakirimia kuona.
22 Ndipo alipojibu, akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana hayo mliyoyaona na kuyasikia; vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanahubiriwa habari njema.
23 Naye heri mtu ye yote asiyechukizwa nami.
 Luka8: 49 Alipokuwa akinena hayo, alikuja mtu kutoka nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi, akamwambia, Binti yako amekwisha kufa; usimsumbue mwalimu.
50 Lakini Yesu aliposikia hayo, alimjibu, Usiwe na hofu, amini tu, naye ataponywa.
51 Alipofika nyumbani hakuacha mtu kuingia pamoja naye ila Petro, na Yohana, na Yakobo, na babaye yule mtoto na mamaye.
52 Na watu wote walikuwa wakilia na kumwombolezea; akasema, Msilie, hakufa huyu, bali amelala usingizi tu.
53 Wakamcheka sana, maana walijua ya kuwa amekwisha kufa.
54 Akamshika mkono, akapaza sauti, akisema Kijana, inuka.
55 Roho yake ikamrejea, naye mara hiyo akasimama. Akaamuru apewe chakula.
56 Wazazi wake wakastaajabu sana, lakini akawakataza wasimwambie mtu lililotukia.
Binti akihojiwa na Mchungaji Josephat Gwajima  akielezea jinsi alivyoisikia sauti ikimwita njoo na alivyotoka kwenye kibuyu alimokuwamo.


Mathayo10: 8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.

Kijana huyu alikuwa  Bungeni.

Akihojiwa na Mchungaji Gwajima.
 Matendo ya mitume 10
Yohana11
Wanaochukua watu wanachukua kwasababu wanaona wewe ulizaliwa unakipawa cha kupendwa au una kipawa cha kuongea au cha biashara na waganga na wachawi wanaichukua na kwenda kukitumia na unakuta mtu anaombewa sana lakini hafanikiwi kumbe umechukuliwa. Kwa mtu kuna kiashiria cha yeye atakuwa ni nani baadaye na wanapokiona ndio wanakuja kukichukua ni kipawa kilichotoka mbinguni hata kabla haujaumbwa kinaitwa nyota na mwanasiasa au mfanya biashra anafanikiwa kuliko wenzake kumbe anachukua nyota za watu na kuzitumia. Na sio elimu yako ndiyo inayokuhakikishia mafanikio bali ni ile nyota yako au karama uliyo pewa na Mungu kutoka mbinguni ndiyo inayokupa mafanikio.
 
Mama huyu akielezea jinsi alivyoisikia sauti ikimwita njoo.
 “Kwa jina la Yesu ninaamuru tumbo la uzazi, moyo wangu, kinywa changu, akili yangu, kibali changu kinachotumiwa na mtu njoo kwa jina la Yesu”. Mungu ni Mungu wa kurudisha mfano taifa la Israeli lilikwenda misri miaka 430 lakini Mungu aliwarudisha, haitoshi pia taifa la Israeli lilikwenda  
Babeli miaka 70 lakini Mungu aliwarudisha, baadaye wakasambaa dunia nzima lakini Mungu akawarudisha ndio maana amesema nitakurudishia Afya yako nami nitakuponya magonjwa yako.
Imeandikwa Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale 
Mama huyu alikuwa Shambani.
waisikiao watakuwa hai. Ninaamuru wale waliochukuliwa na kufichwa mapangoni, mashimoni, wamekuwa mateka njoo kwa jina la Yesu, wafalme wa kishetani, wakuu wa kipepo achilia watu hao kwa jina la Yesu kristo mwana wa Mungu aliye hai, navunja nguvu zenu, nashambulia nguvu zenu, nateketeza majeshi yenu kwa damu ya Yesu, ninaamuru kwa mamlaka ya Jina la Yesu achilia mateka yenu kwa jina la Yesu, uliowachukulia nyota zao ulio wachukulia vipawa vyao ninaamuru achilia kwa jina la Yesu. wale watu waliofichwa njooo kwa jina la Yesu, visima vyenye maji yasio kauka, njia panda, mapori na mahala popote, walio mashimoni, walio mashambani, waliowekwaa ndani ya makabati ninaamuru njooooooooo kwa jina la Yesu.
Ameni.


maelfu ya watu walioudhuria ibada katika bonde la kukata maneno.


No comments:

Post a Comment