Sunday, August 17, 2014

MASHETANI WALIOVAA MIILI YA WANADAMU WAZIDI KUCHAKAZWA KATIKA BONDE LA KUKATA MANENO KAWE.IBADA YA TAREHE 17/08/2014
SOMO: SHETANI KATIKA UZAO WA WANADAMU
MCHUNGAJI KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima

Shetani ni roho lakini alishahama katika roho na yupo katikati ya wanadamu na unaweza kumkuta mtu anaonekana binadamu kumbe ana roho ya kishetani.  Mafarisayo walipomwendea Yesu katika Mathayo23:33 Yesu aliwaambia 33 Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?  pia katika kitabu cha Mathayo 12:34 34 Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake. 35 Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya.  pia kitabu cha Mwanzo 3:15 15 nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigin. Kwa ufupi kuna wanadamu kabisa tunaishi nao lakini si binadamu kama wanavyoonekana kwa jinsi ya mwili.
Mwanzo19:1-10 Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi. 2 Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani mwa mtumwa wenu, mkalale, mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na mapema mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha. 3 Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake. Akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala. 4 Hata kabla hawajalala, watu wa mji, wenyeji wa Sodoma, wakaizunguka nyumba, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka pande zote. 5 Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wa wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate kuwajua.
Lutu alikuwa anaongea na hawa malaika ili wale na wanawe miguu wakati ni malaika na hakujua kama ni malaika, lakini sio watu, malaika hawa Lutu amewaona kana kwamba ni binadamu na walikula chakula na hii inatufundisha kumbe sio kila anayekula umwite mtu lazima ujue kuna uzao usio wa kibinadamu unafanya kazi pamoja na wanadamu na kazi Yetu ni kuuondoa ule uzao  na kujenga Ufalme wa mwanakondoo. Hata wale wenyeji wa mji wa sodoma na gomora waliwadhania kuwa ni watu lakini walikuwa ni malaika.
Waebrania13:2 Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.
Hapa tunajifunza kuwa tunaweza kukutana na mtu njiani na kumfadhili kumbe ni malaika wa giza aliye vaa mwili na tunatakiwa tuangalie zaidi ya akili za kibinadamu ili kujua aliye mtu na asiye mtu, sio unakutana na mtu njiani anakuambia anakupenda hapohapo mnachukuana na kwenda nyumbani na baadae mnafunga ndoa na matatizo yanakujia tangu ulipoanza uhusiano na mtu huyo ama wa kibiashara au kimwili lakini kiuhalisia yule alikua ni uzao wa kishetani aliye kuja kwako na kukuletea matatizo.
Kuna binadamu lakini ni mashetani asilimia miamoja wamejichanganya katika uzao wa wanadamu na kufanya mambo ya ajabu lakini wanaonekana ni watu wa kawaida tu kumbe ni mashetani wametumwa toka kuzimu kuja duniani kuharibu mataifa na maisha ya watu. Majini,majoka,mizimu,miungu ya mashariki ya mbali, mapepo wanaitwa malaika wachafu(waovu) wote hao wanaweza kuvaa mwili na kuishi na binadamu makazi yao ni kuzimu ndio hao Biblia inawaongelea kwamba “ni rahisi  kueneza mambo machafu na wanahekima kwa mambo mabaya lakini ni wapuuzi kwa mambo yalio mema” na hao wataangamizwa kwa jina la Yesu. Na malaika wema ni malaika watakatifu wanakaa mbinguni. Malaika wote wanaweza kujigeuza kuwa kitu chochote.
Waebrania1: 7 Na kwa habari za malaika asema, Afanyaye malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa miali ya moto.
Malaika wetu wa mbinguni wanaweza kugeuka kuwa upepo
Yuda1: 6 Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
Hawa ni mashetani lakini ni malaika wagiza.
Ufunuo12: 7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
Uzao wa kishetani katikati ya wanadamu na nyakati hizi ni nyakati ambazo mpinga kristo anataka kuingia duniani na atakuwa na mama yake na Baba yake lakini watu hawajui hili kwakua wanajua kila aliye na mwili ni mwanadamu wa kawaida Mfano Yesu alikuwa anajulikana ni mwana wa Yusufu na Mariamu kumbe alikuwa katoka Mbinguni kwenye makao yake na ni mwana wa Mungu Baba wa mbinguni.
Yesu alikutana na mwanamke mmoja kisimani na Yesu alimuuliza kuwa unaye mume? Yule mama alimjibu hapana maana nilio nao ni watano na akajibu sina mume na Yesu akasema umesema vyema, maana yake alikuwa na wanaume ambao wanamharibia maisha yake.
Biblia inasema mpingeni shetani naye atawakimbia na hatutakiwi kuwakimbia watu hawa wenye miili ya kibinadamu waliotoka kuzimu bali tunawafuata huko huko walipo. Na huyu jini au joka anaweza kuwa Mchungaji, Mwanasiasa, Paroko, au mtu yeyote anaongea vizuri lakini sio mtu anamwili wa kibinadamu ndani anaroho ya kishetani.
Namna ambayo hawa mashetani watu wanaweza kumwangamiza mtu
1.       Kwa njia ya macho, mtu anaweza kukuangalia tu ukauua wiki mbili. Kwa kutumia macho yako anakurushia vitu na vinakupata.
2.       Kupitia mahusihano ya kimwili
“1Wakorintho6: 16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.” Biblia inasema mume na mke wanapooana wanakua na uhusihano na uhusihano unaewaleta pamoja na aliye umbwa na kahaba ni mwili mmoja . pia Yesu kristo na sisi kanisa tunauhusiano kupitia Roho mtakatifu. Shetani anapokuwa na uhusihanowa kimwili na mtu lengo lao ni kuwawekea watu matatizo unashangaa bihashara inaanza kuharibika au unashangaa unapatwa na mikosi kumbe ni unakua umejiungamanisha na shetani uliyefanya naye mahusihano. Pia kwenya ndoto unapoota unafanya mahusihano unakuwa unajiungamanisha na mashetani na hapo matatizo yanakua yanaanza na ukifuatilia maisha yako unaona matatizo yako yameanzia pale ulipokutana kimwili na mtu Fulani ambaye ndani yake anakusudi la kishetani.  Pia unapoona mtu anajiuza unadhani ni mtu kumbe ni shetani yupo mawindoni na anapokutana na mtu kimwili anamwachia ushetani ndani yake na mambo yake yanaanza kuharibika na anakua anamilikiwa na nguvu ya kishetani kwenye maisha yake ma mambo yanaanza kuharibika.
ZABURI 78:49 Akawapelekea ukali wa hasira yake, Ghadhabu, na uchungu, na taabu, Kundi la malaika waletao mabaya.
3.       Kupokea zawadi kutoka kwake. Nguvu inaweza kuwa ndani ya kitu ulichopewa na mtu
Matendo ya mitume19: 12 hata wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizotoka mwilini mwake, magonjwa yao yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka. Maana yake kile kinachotoka kwa mtumishi wa Bwana kinabeba uweza wa Bwana na kinaweza kutenda miujiza kwa wagonjwa. Sasa vilevile na mashetani wanaweza wakabeba uweza wa kishetani kwenye vitu na matatizo yakawapata watu mfano mikufu, saa, nguo viatu,gari, au kitu chochote kinakuwa kimebeba uweza wa kishetani  ndani yake kama magonjwa na matatozi mengine” kwa jina la yesu ninaangamiza chochote nilichopewa kama zawadi au nimenunua mimi mwenyewe, kwa jina la Yesu chochote kile kilichopandwa ili kuharibu familia au kazi yangu kama ni kitambaa nakuamuru uteketee, kama ni zawadi nakutetekeza kwa damu ya Mwana Kondoo  ushetani ulioletwa kwa njia ya macho au kwa njia ya zawadi ya aina yeyote naiteketeza kwa jina la Yesu, nateketeza kwa jina la Yesu(unapoomba hivi kwenye ulimwengu wa Roho vinateketea) kwa jina la Yesu naiteketeza kila zawadi niliyopewa na mtu yeyote asiye binadamu aliyekuja kwenye maisha yangu namteketeza kwa jina la Yesu, iwe ni zawadi iliyonuiziwa kifo, balaa, mikosi, naivunja kwa jina la Yesu, kitu chochote kilichonuiziwa manuizo ya kishetani  juu yangu au familia yangu nakiteketeza kwa damu ya mwana kondoo. Namshambulia binadamu yeyote aliyetumwa kuja kufanya mahusihano na mimi na kuniwekea manuizo ya kishetani namshaambulia kwa jina la Yesu, kwa damu ya mwanakondoo, aliyenitupia mishale kwa njia ya macho,  chakula,  maji  ninaiharibu kwa damu ya mwanakondoo, kwa jina la Yesu ushetani wowote uliotumwa ndani yangu naukataa kwa jina la Yesu.  Jini wa uchawi aliye tumwa kwangu kwa njia ya kishetani na balaa na mikosi iliyopangwa juu yangu naivunja kwa jina la Yessu na kifo kilichopangwa juu yangu nakifuta kwa damu ya mwanakondoo. Sitakufa kwa jina la Yesu, kifo chochote kilichopangwa juu yangu nakivunja kwa jina la yesu.  Navunja tamaduni zote za kishetani  kwa jina la Yesu.
 AMEN.


No comments:

Post a Comment