Friday, August 8, 2014

NGUO ZA UCHAFU
na Pastor Josephat Gwajima


Zakaria 3:1

Yoshua alikua ni mtumishi wa Mungu na alisimama ili kuifanya kazi ya Mungu lakini shetani nae akasimama mkono wake wa kuume ili ashindane nae.
Kwanini shetani amesimama  mkono wa kuume na sio wa kushoto?
Mkono wa kuume maana yake ni mkono wenye nguvu, ndio maana tunasoma Yesu ameketi mkono wa kuume wa Mungu baba, kwa maneno mengine Yesu ndie ameshikilia nguvu za Mungu baba na kama unahitaji nguvu za Mungu baba unatakiwa kuwa kumpata Yesu.
Hapa tunaanza kuona shetani anashindana na mtu wa Mungu, na katika mashindano kuna kushinda au kushindwa kwasababu ni mashindano.
Ziko sababu kwanini shetani alipata  nafasi ya  kushindana na kuhani  wa Mungu Yoshua, shetani alipata nafasi kwasababu Yoshua alikua na nguo chafu.
Shetani huwa hawezi kuanza kumshambulia mtu bila kuwa na kitu kinachompa uhalali wa kushambulia, kwa Yoshua kuhani mkuu alipata nafasi kupitia maisha yake, maisha yake hayakua mazuri na ndio yanawakilishwa na nguo za uchafu. Hii ndio sababu maandiko yanasema wala msimpe ibilisi nafasi (waefeso 4:27)
Kumbe ibilisi huwa hatendi kazi mpaka apate nafasi, ukimnyima nafasi huwa anakosa nguvu kabisa. wakati shetani anataka kushindana na shetani alikuwako pia malaika wa Bwana mahali hapo.
shetani ni roho na kwakua ni roho huwezi kumgusa, kumuona, kumuhisi wala kumshika ila anachofanya anapotaka kutenda kazi anaingia ndani ya mtu na wewe unaweza ukaanza kumlaumu mtu kumbe ndani ya huyo mtu yuko shetani.
Hapa malaika wa Mungu alikua amesimama ili kumtegemeza Yoshua na shetani alisimama ili kushindana nae, hii inatuonyesha kumbe wako viumbe wa rohoni wanaosimama ili kututegemeza na wako wanaosimama ili kushindana nasi, hapo ulipo wapo wanaosimama ili kukusaidia usonge mbele na wako wanaokusaidia ili kurudi nyuma.
kwakua shetani ni roho anaweza akaingia ndani ya mtu aliye karibu yako ili kuleta uharibifu maishani mwako,anaweza akaingia ndani ya mume/mkeo, anaweza akaingia ndani ya rafiki (shetani akaingia ndani ya Yuda aitwaye Iskariote ili amsaliti Yesu)  na anaweza akaingia hata ndani ya mnyama( Yesu aliwaamuru mashetani wakaingia ndani ya nguruwe na nguruwe wakaangami abaharini)
Shetani aliingia ndani ya Yuda baada yakufungua mlango wa kutaka fedha katika maisha yake, kwa maana nyingine kwa namna ya rohoni sio yuda aliyemuangamiza Yesu bali ni shetani aliyekua ndani ya Yuda, Yuda alitumika kama chombo.
Shetani hawezi kutenda kazi mpaka apate mahali pa kuingilia, ndio sababu kuna watu wanakupinga bila sababu lakini ni kwasababu shetani anatenda kazi ndani yao.
na shetani anaamua kukaa kwenye mkono wako wa kuume au mkono wakjo wenye nguvu, eneo lile unalolitegemea likutoe katika umasikini ndio shetani anakaa hapo, au unakua na mtoto wako unategemea afanye vizuri katika masomo hapo ndipo shetani anashambulia.
Hii ndio sababu kuna watu baadhi ya mambo wanaweza kufanya, anaweza kuhudhuria harusi, ndoa anaweza kufunga lakini hata afanyeje nyumba hawezi kujenga, hii inamaana lile eneo unalolitegemea analikalia kwa nguvu kutokana na mavazi ya uchafu yaliyo katika maisha yako.
zamani palikua na watu waliokua wakimtegemeza mfalme na wao walikua wakiiitwa mkono wa kuume, mfalme alikua akitaka kufanya jambo kwa kumtumia mtu huyo anakua na uhakika jambo litafanyika vizuri. Nae shetani anapoliona eneo hilo la maisha yako anakuja na kulikalia, Mungu anaweza akawepo na malaika wake wanaweza kuwepo lakini bado shetani akapata nafasi ya kuendelea kukaa hapo kwasababu ya mavazi ya uchafu ambayo ndio mlango.
ukitaka upenyo huyu aliye mkono wa kuume anasimama ili apingane nawe, ndio sababu Mungu alipomuona mtumishi wake anapigwa akaamuru avuliwe nguo zake za uchafu, hakuna namna ya kumuokoa, na yule aliye mkono wa kuume amepata nafasi kwasababu ya nguo zenye uchafu.
Nguo za uchafu zilipotolewa ndipo likamjia neno kuwa yeye ni kinga( kaa la moto kutoka madhabahuni kwa Bwana) cha Bwana.
Ni maombi yangu leo Mungu akuondolee vazi lako la uchafu na uwe kama moto kwa wale adui zako na wale wanaokuwazia mabaya washindwe kukugusa kwa jina la Yesu.
NINI MAANA YA NGUO ZA UCHAFU?
Nguo za uchafu ni yale mambo yasiyompendeza Mungu mtu anayotenda nayo yanampa shetani nafasi katika maisha yake. Hakuna mtu hata mmoja aliyewahi kusema shetani karibu ndani ya moyo wangu uwe muharibifu wa maisha yangu.
Shetani anatumia milango ambayo tunafungua katika maisha yetu na anapoingia ndani ya maisha yetu anasababisha matatizo ambayo yanakua vigumu kujitoa mpaka tuondoe milango hiyo.

MILANGO SHETANI ANAYOTUMIA KATIKA MAISHA YA WATU
1) Mlango wa Mila
Mila ni desturi ambazo watu wamezoea kuzitenda kil asiku na zikawa sehemu ya maisha yao. Kuna mila nyingi sana zinazotengeneza milango ya shetani maishani mwao.
mf. Mila ya kumaliza msiba. Kwenye tamaduni za kawaida kumaliza msiba ni siku ya arobaini tangu marehemu afariki watu wanatumia kusherekea na kucheza,
mf.2. Ni kunyoa nywele wakati wa msiba, nikupe historia kidogo utaratibu wa kunyoa nywele ulitokea mashariki ya kati kutoka sehemu inaitwa mesopotamia, kwasababu watu walianzia hapo kuwa na tamaduni za kuishi pamoja( Socialization) na kutokea hapo watu wakaanza kusambaa duniani.
Ndio sababu watu wa Ethiopia wanafanana na watu wa Rwanda na wairaki wa Tanzania kwasababu wote wanaasili moja, na hizo tamaduni walitoka nazo huko walikokua.
Watu walikua wakinyoa nywele na kuziweka katika makaburi na kusema mahali huko ulikokwenda na sisi tutakuja huko huko, walikua wanaamini mtu anapokufa anaenda mahali panaitwa Sheol(Kuzimu)
Hii ndio sababu unakuta familia inakua na vifo vya kufanana, wote wanagongwa na magari, au ugonjwa wa aina moja.
nilikutana na baba mmoja akaniambia mchungaji tarehe 3/8 ambayo ni kesho nafariki, nikashangaa sana  nikamuuliza kwanini, akasema nilikua na kaka yangu mmoja alifariki tarehe 3/8 kwa ajali ya gari, baada ya miaka mitatu mingine dada yetu mkubwa akafa tarehe 3/8 kw aajali pia, kaka yetu mwingine alikua uingereza baada ya miaka mitatu mingine ilipofika tarehe 3/8 akafa katika ajali ya ndege, nimebaki mimi tu na imepita miaka mitatu tayari nakesho ni tarehe 3/8. nisaidie mchungaji.
Laana haiji katika maisha ya mtu isipopata nafasi. Mithali 26:2. Laana ni ya rohoni lakini inadhihrika mwilini.
Milango hiyo ndio nguo za uchafu
Kuna mambo yanayofanana katika familia, mfano Ibrahimu alipokua mtu mzima akaenda Misri na alipofika huko akadanganya mkewe ni dada yake, na Isaka nae alipokua na mke njaa ilipotokea wakakimbilia nchi ya jirani nae akadanganya kuwa mkewe ni dada yake.
Ndio sababu Daniel na wenzake walikataa kula chakula cha mfalme nebukadneza kilichotolewa kwa sanamu, waliacha kufuata mila zisizofaa.
 ITAENDELEA

KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI:
0714729805
0716671440
0718104333
0717727206No comments:

Post a Comment