Wednesday, August 13, 2014

NILIAIBIKA MLIMANI NITATUKUZWA MLIMANI - Pastor Josephat Gwajima

                                                                  
Na: Pastor Josephat Gwajima

1 Wakorintho 1:18- Kwasababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuuzi bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.
“UJUMBE WA MSALABA NI NGUVU YA MUNGU” nilikua najiuliza sana neno la msalaba maana yake nini, nikajiuliza hivi ni kwanini Yesu alisulubiwa msalabani, kwanini asingepigwa mawe au makonde mpaka akafa.?

Tunaanza kuona msalaba ni wa muhimu sanandio sababu biblia inasema katika 
Yohana 19:17  “Akatoka hali akijichukulia msalaba wake mpaka mahali palipoitwa fuvu la kichwa au kwa Kiebrania goligotha”

Yesu alipoonekana anatakiwa kusulubiwa alitolewa nje ya mji akasulubiwa kwenye mlima mmoja mahali palipoitwa kalvari ambapo palikua ni mlimani,  na si Yesu peke yake aliyesulubiwa mahali hapo bali walikuwepo wanyanganyi wawili, aliyekua mtakatifu akasulubiwa pamoja na wanyang'anyi

Mahali hapo palikua si bondeni bali ni katika mlima na ilikua karibu na njia, na wakati huo wayahudi walikua wakisherekea sikukuu ya pasaka, yeye naye akasulubiwa katika sikukuu hiyo ya pasaka.
Wayahudi waliokua wanaingia mjini wote kwasababu ya sikukuu walimuona njiani hapo akiwa ametundikwa uchi mbele za watu wote kwasababu mahali hapo palikua ni njiani.

Mtu ambaye alikua anafufua, mtu ambaye alikua anaponya, mtu ambae alikua analisha watu maelfu leo amevuliwa nguo  na ametundikwa katika mti kwa misumali.
Waliona mtu huyu ametusumbua sana tukimuua hivi hivi aibu yake haitaonekana vizuri ni bora tumuinue katika mti ili aonekane na watu wote, watu wengine waliokua wakipita njiani kila walipomuona walikua wakitema mate chini, na wengine wakisema aliokoa wengine basi na ajiokoe mwenyewe.
Na zaidi ya hapo wakamvisha taji ya miiba na kumchapa sana, mgongoni alipigwa viboko thelathini na tisa, ukimuangalia amejaa damu na yuko uchi.
Wanafunzi wake wakimuangalia aliyekua kiongozi wao mbele ya askali waliokuia wakimdhihaki mbele ya watu wote, na watu wakasema amekomeshwa, wakasema amewezwa na kila mtu akasema aliyoweza kwasababu ulikua ni wakati wa aibu.

Kwenye maisha Mungu anaweza akaruhusu wakati wa aibu, ukaaibika na ukakosa msaada, wale wanafunzi waliotembea na Yesu walimuona akiaibika lakini walikua hawana msaada, Lazaro aliyefufuliwa alikuwepo lakini alikua hana msaada, wanaume elfu tano aliowalisha hawakuweza kutoa msaada, wale wakoma kumi aliowatakasa walikuwepo lakini walikua hawawezi kutoa msaada.

Na wote waliokua wakimtakia mabaya wakafurahi wakaona tumemkomesha na tumemuweza. Na Mungu wa mbinguni alipoona mwanae ameaibika amebeba dhambi za ulimwengu akamgeuzia mgongo, yeye ambae alimtegemea amsaidie naye akamgeuzia mgongo, akabaki  peke yake, ndio sababu akalia akasema BABA YANGU BABA YANGU MBONA UMENIACHA

Wakasema alisema yeye ni mwana wa Mungu lakini hata baba yake amemuacha, na amesema mwenyewe. Bwana Yesu alikufa huku analalamika kwenye aibu mlimani.
Na alipokua katika hiyo aibu Mungu wa mbinguni hakuweza kuvumilia akaweka akaamua kulifunika jua na giza likaingia duniani ili kuificha aibu.
Baada ya kuona ameitimiza aibu yote akapaza sauti akasema imekwisha na akakata roho.
Yawezekana umepata jambo likakuletea aibu ya asilimia mia moja na wale wote niliokua nikiwategemea wameniacha, wewe sio wa kwanza hata Yesu alipitia katika hali hiyo.
Baada ya hapo Yesu akazikwa, na katika msiba wake hakuzikwa na watu wengi alizikwa na mtu mmoja aliyekua anaitwa Yusufu, mtu ambae alienda kuuomba mwili kwa pilato ili akauhifadhi.

Baadae wakaamuru kabuli lake lilindwe, hata baada ya kufa wakataka kuendelea kuilinda aibu yake.
Kumbe unaanza kujifunza kuna aibu unaweza ukawa umeipata katika maisha yako, aibu ya ndoa, au ya masomo au aibu ya aina yoyote wako walinzi wa rohoni ambao kazi yao ni kuendelea kukulinda katika aibu hiyo hiyo ili uendelee kuabika.

Napenda kukupa habari njema ULIABIKA MLIMANI, UTATUKUZWA MLIMANI PIA.
Wapo watu wanaoendelea kuilinda aibu yako ili iendelee vile vile, ila leo napenda kukuambia uliaibika mbele ya watu wote na utukufu wako utaonekana mbele ya watu wote pia .
Yawezekana ulichumbia na mahali ikatolewa lakini kabla ya ndoa uchumba ukavunjika, au ulikua mfanya biashara mzuri lakini baada ya muda ukapoteza kila kitu na unaona aibu kuwaambia watu kuwa biashara imekufa, pale pale ambapo shetani anakazania uaibikie hapo Mungu naye anataka usiabike kwa jina la Yesu.

Baada ya siku tatu tukio moja likatokea wakati walinzi wanailinda ile aibu, panapo majira ya asubuhi wakaanza kuhisi tetemeko la nchi wakamuona malaika akishuka mwenye sura kama umeme akashuka na wale walinda aibu wakaanza kutetemeka na kuwa kama wamekufa.
Leo ni maombi yangu kila wanaoilinda aibu yako waanze kutetemeshwa na wawe kama wamekufa kwa jina la Yesu.
NINAIONA AIBU YAKO INAANZA KUONDOKA KWA JINA LA YESU
WALE WANAOILINDA AIBU YAKO WAOGOPE WATETEMKE NA WAWE KAMA WAFU KWA JINA LA YESU
Baada ya malaika kushuka Yesu akatoka kaburini na baada ya kutoka kaburini yule malaika akalikalia lile jiwe, hii ni kwasababu baada ya aibu kuna uthibitisho baada ya unaokuwepo.
Baada ya Yesu kufufuka alikaa na wanafunzi wake siku arobaini na akawachukua wanafunzi wake akaenda nao katika mlima wa mizeituni akapanda nao mlimani akiwa na mwili wa utukufu, akiwa amejaa utukufu mwingi akapaa kwenda mbinguni.
Aliabika mlimani na alitukuzwa mlimani, mahali pale ambapo kila mtu alimuona wakati anaaibu wakamuona akiwa katika utukufu mbele ya watu wote.
Yawezekana tatizo lako limejulikana na watu wote wakati unaaibika lakini kama yesu alivyoaibika nba kutukuzwa mlimani n akwako pia utatukuzwa mbele ya watu wote.
UKIAIBIKA WAZI WAZI UTATUKUZWA WAZI WAZI.
Yesu aliwaambia watu ni mwana wa Mungu wakampiga na kumuua mbele ya watu wote, Mungu akadhihirisha mbele ya watu wote kwa kulituma wingu kutoka kwake lije kumchukua mbele ya watu wote.

Yawezekana umeaibishwa sana na kufedheheshwa sana lakini mungu nae anaompango wa kukutukuza mlimani mbele ya watu wote
Aibu uliyoipata itaondoka kwako na furaha yako itarejea tena kwa jina la Yesu.

Musa alishindwa kuingia katika nchi ya ahadi na watu wakawa wanajua Musa ameaibika kwa kushindwa kuirithi nchi ya ahadi lakini wakati Yesu yuko duniani katika nchi ile ile ya kanani Yesu alitokewa na Musa na Eliya wakiwa katika utukufu mwingi.

Kuna wakati Mungu anaruhusu unapitia katika mambo makubwa magumu ambayo yaaonyesha ni fedheha ya nmana ya ajabu  lakini napenda ufahamu kadiri tatizo lako linavyozidi kuwa kubwa ufumbuzi wako nao unakua mkubwa na wenye utukufu mwingi.
Ndio sababu ujumbe wa msalaba kwao wanaopotea ni upuuzi bali sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu, neon la msalaba hilo ni ile aibu ya msalabani, mateso ya msalabani fedheha ya msalabani  na Mungu alipoona ameaibika vya kutosha akamtukuza kwa kumtumia wingu mbele ya watu wote na utukufu wake ukawa mkuu.


Ninaomba leo kila wanaokulinda kwenye aibu yako waaibike na wawe kama wafu , na wewe utukuzwe juu sana kwa JIna la Yesu

No comments:

Post a Comment