Monday, August 4, 2014

UFUFUO NA UZIMA YANUNUA HELIKOPTA KWAAJILI YA MIKUTANO YA INJILI INAYOANZA MWEZI WA NANE.

Katika ibada maalumu ya kumshukuru Mungu kwa mambo aliyotenda ikiwa ni pamoja na kufanikiwa kununua helikopta kwaajili ya mikutano ya injili  iliyofanyika katika viwanja vya Tanganyika packers ambapo ndipo lilipo kanisa  la Glory Of Christ(T) Church maarufu kama Ufufuo na Uzima  ilipendeza kwa namna ya ajabu sana.

Ibada hiyo iliyohudhuriwa na maelfu ya watu pamoja na waimbaji mbali mbali wa nyimbo za injili ilishuhudia kanisa la Ufufuo na Uzima likijitolea kununua madawati nakusaidia kuweka umeme katika shule za msingi zilizo Kawe, akizungumza katika ibada hiyo Mheshimiwa Halima Mdee alisema ukiona mahali ambapo watu wa Mungu wameweza kutumia rasilimali zao vizuri hadi kufikia hatua ya kununua helikopta kwaajili ya kazi ya Mungu ni jambo zuri na la kuingwa.

Mheshimiwa Halima Mdee wakati akizungumza alisema wakati chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimeanza kuzunguka na helikopta maarufu kama chopa, kilishutumiwa kufuja mali kutokana nagharama za uendeshaji wa chombo hicho, akifafanua alisema "Chopa ni chombo ambacho gharama zake ni nafuu kuliko chombo kingine cha usafiri kutokana na  uharaka wake na uwezo wake wa kufika maeneo ya mbali hata mahali pale ambapo watu hawajawahi kusikia neno la Mungu.

Katika ibada hiyo mheshimiwa Halima Mdee alichangia kiasi cha shilingi milioni kumi kwaajili ya ununuzi wa madawati hayo.

Ibada hiyo ilipambwa na waimbaji mbali mbali wa nyimbo za injili miongoni mwao ni John Lisu, Upendo Nkone, Rose Muhando, Munishi, Christina Shusho, Bonny Mwaitege,Mahanaimu Sound na wengine wengi.

Katika ibada hiyo moja ya mabo ambayo yaliwagusa watu kwa namna ya kipekee ni pale ambapo Mchungaji Gwajima alimzawadia gari mpya muimbaji John Lisu, aliamua kumpa baada ya John Lisu kumaliza kuimba wimbo wake Wewe ni Mungu, akifafanua alisema John Lisu ni kama Don Moen wa Tanzania na ni vizuri kujifunza kuwabariki na kuwatendea mema watu wanaotumiwa na Mungu kugusa maisha yetu kwa namna ya ajabu, ni jukumu letu kuhakikisha wanaishi vizuri, wanakula vizuri, wnalala pazuri na wanakua na maisha mazuri baada ya hapo alimuambia baada ya wiki tatu akaichukue gari yake kanisani hapo.

PATA PICHA ZA MATUKIO HAYO HAPA

Mchungaji Josephat Gwajima 


Sehemu ya wtu waliohudhuria ibada ya jumapiliMchungaji Josephat Gwajima akiwa amekaa na mkono wake wa kulia ni ,mbunge wa jimbo la Kawe Halima Mdee, aliyesimama kushoto ni mke wake Grace Gwajima

Maelfu wakimshangilia Mungu kwa furaha

Mheshimiwa Halima Mdee akizungumza


Mheshimiwa Halima Mdee akifafanua jambo
Muimbaji wa nyimbo za injili Rose Muhando akimsifu Mungu

Flora Mbasha akimuimbia Mungu

Flora Mbasha


Baadhi ya wachungaji kutoka Japanio ambao walifanikisha ununuzi wa helikopta hiyo 
John Lisu akimuimbia Mungu


Halima Mdee akiteta jambo na Mchungaji mwandamizi Yekonia Bihagaze (RP) baada ya kuwasili kanisani hapo

Brass Band ya Jeshi la magereza ilipowasili kanisani

Mchungaji Maximillian Machumu "Mwanamapinduzi" pamoja na Upendo Nkone

Munishi

Munishi akiwasalimia watu

Malebo( aliyeimbwa kwenye wimbo wa Munishi na kuokoka) akisalimia

John Lisu na Jackson Bent

Flora Mbasha na Ruth 

Brass Band ya Jeshi la Magereza 

Saraphina Urio wa Mahanaimu Sound akiimba

Rose Muhando

Christina Shusho


Mchungaji Gwajima akipita kuombea wenye shida mbali mbali


Sehemu ya watu waliokua na mapepo wakiwa wameangusha chini na Nguvu za Mungu 

Sehemu ya watu waliohudhuria ibada


Ruth kutoka Mahanaim Sound akiimba 

Bonny Mwaitege akiimba


Vijana wa Yesu wakicheza mbele za Mungu

Munishi akitoa ushuhuda


Mmoja wa watu waliohudhuria Ibada akimwabudu MunguAdd caption

1 comment:

  1. safi sana mungu anasikika Tanzania mungu ibariki Tanzania mungu bariki ufufuo na uzima amina yesu anasuka tanzania

    ReplyDelete