google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NJIA KATIKATI YA GIZA & KUTII SAUTI YA MUNGU


JUMAPILI YA TAREHE 28/9/2014

MCHUNGAJI JOSHIDA (JAPAN) NA MCHUNGAJI KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA

SOMO: SAUTI YA MUNGU

NA MCHUNGAJI YOSHIDA
Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima na mchungaji Yoshida kutoka Japani

Tunapomsifu Mungu, Mungu anatenda kazi, kupitia maombi Mungu atatenda kazi pia. Sisi wakristo tunatakiwa tuamini Mungu anatenda kazi sehemu yeyote bila kujali mazingira tuliyo nayo. Kwake Mungu hakuna kitu kisichowezekana na tunatakiwa kumwangalia Mungu aliye juu Mbinguni.

Sisi tunamwamini Mungu ambaye anatenda mambo yote, uraia wetu ni Mbinguni na ni lazima twende mbinguni. Kupitia maombi Mungu anatusikia, tunapata amani, tunakuwa pamoja na Mungu na tunatenda mapenzi yake. Kila wakati unapomuomba Mungu mlango unafunguliwa. Unaweza kupokea baraka nyingi ukisikia sauti ya Mungu na kuitii. Tunatakiwa tuitii sauti ya Mungu. kwa maana sauti ya Mungu inasikika. Mungu wetu ni Mungu  wa uponyaji, tukiwa na imani Mungu anatenda kazi.

Kwenye maisha yetu kuna matatizo mbalimbali na ili kuyakabili tunatakiwa tuombe na kwa uwezo wa Roho mtakatifu Mungu anatusaidia kupitia Roho mtakatifu kwa neno lake. Mungu anatenda kazi  kwa mbegu ya neno lake tunalo panda kwenye Roho zetu.

Mathayo17:26

26 Naye aliposema, Kwa wageni, Yesu alimwambia, Basi, kama ni hivyo, wana ni mahuru.

Tukitoa sadaka kwa moyo wote Mungu anakusaidia kulingana na haja ya moyo wako. Tukiomba kwa nguvu zetu zote Mungu anatenda kazi kwa maana baraka za Mungu hazina mipaka. Ni muhimu sana kuvunja mapenzi yetu binafsi na kufuata mapenzi ya Mungu. Kuna watu wengi wamefanikiwa kwa kuyafanya mapenzi ya Mungu. Mungu wetu ni Mungu wa ahadi,miujiza, Mungu anayetimiza ahadi zake ni Mungu wa Rohoni. Kuna ahadi Ishirini na saba(27) ambazo Mungu ametuahidi na kati ya hizo ahadi kila kitu tunachokihitaji kimo ndani ya hizo ahadi zake.

Kwenye kitabu cha mwanzo Mungu anasema iwe nuru na ikawa, maana yake Mungu anatupa mahitaji yetu kupitia neno laketunatakiwa kila wakati tuwe tunamwomba Mungu kwa kumaanisha kwa Roho na kweli. kwenye kitabu cha Yoeli Mungu amesema wakati unakujaatamimina Roho yake juu yetu na huo wakati ndio huu.

Yoeli 2: 28.

28 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;

 

 

NJIA KATIKATI YA GIZA

MCHUNGAJI JOSEPHAT GWAJIMA

Kutoka13:7

7 Mikate isiyochachwa italiwa katika hizo siku saba; mkate uliotiwa chachu usionekane kwako, wala chachu isionekane kwako, ndani ya mipaka yako yote.

Mungu alipowaondoa wana wa Israeli kutoka katika nchi ya ahadi kulikuwa kuna njia mbili, kwenye mafanikio ya maisha zipo njia mbili, fupi na ndefu

Kutoka15:3

3 Bwana ni mtu wa vita, Bwana ndilo jina lake.

Uwezo wako wa kupigana vita ndio uwezekano wa kumiliki  ulichoahidiwa. Wakati kwenye ulimwengu wa mwili watu wanalala na kuona ni amani, kwenye ulimwengu wa Rohoni vita imepamba moto. Lakini Daudi anasema ‘ jeshi lijapojipanga kupigana nami moyo wangu hautaogopa.’ Kila anayeshindana na Bwana hawezi kushinda kamwe. Muulize Farao wa Misri, muulize Nebkadneza, muulize Herode au muulize Lusifa juu ya ile vita iliyotokea mbinguni. Bwana ni Bwana wa vita na Bwana ndilo jina lake.

Kumiliki Baraka na kupigana vita kuna mahusihano, wapiganaji ndio wanaomiliki siku zote.

Waefeso6:12

Kuna majeshi mengine yanataka kupigana na kanisa lakini yapo kwenye ulimwengu wa roho, yamejipanga kupigana na wewe, na familia yako lakini kwetu yuko Bwana. Kwao kuna mikono ya watu lakini kwetu yuko Bwana.

Kutoka17:8-5

1 Mkutano wote wa wana wa Israeli ukasafiri, kutoka bara ya Sini kwa safari zao, kama Bwana alivyowaagiza, wakatua Refidimu; napo hapakuwa na maji, watu wanywe.
2 Kwa hiyo hao watu wakateta na Musa, wakasema, Tupe maji tunywe. Musa akawaambia, Kwani kuteta na mimi? Mbona mnamjaribu Bwana?
3 Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung'unikia Musa, wakasema, Mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa kiu?
4 Musa akamlilia Bwana, akisema, Niwatendee nini watu hawa? Bado kidogo nao watanipiga kwa mawe.
5 Bwana akamwambia Musa, Pita mbele ya watu, ukawachukue baadhi ya wazee wa Israeli pamoja nawe; na ile fimbo yako ambayo uliupiga mto kwayo, uitwae mkononi mwako, ukaende.
6 Tazama, nitasimama mbele yako huko, juu ya lile jabali katika Horebu; nawe utalipiga jabali, na maji yatatoka, watu wapate kunywa. Musa akafanya hivyo mbele ya wazee wa Israeli.
7 Akapaita mahali pale jina lake Masa, na Meriba; kwa sababu ya mateto ya wana wa Israeli, na kwa sababu walimjaribu Bwana, wakisema, Je! Bwana yu kati yetu au sivyo?
8 Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu.
9 Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu.
10 Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima.
11 Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda.
12 Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa.
13 Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga.
14 Bwana akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu.
15 Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi;

16 akasema, Bwana ameapa; Bwana atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi.

Wana wa Israeli wameambiwa na Mungu tokeni Misri nendeni kwenye nchi niliyowaonyesh njiani walikutana na mataifa mbali mbali wakayapiga na walipofika katikati  walikutana na kataifa ka waamaleki. Taifa hili likasema hata kama mmepita bahari ya Shamu hapa hampiti, hatujali mmefanya miujiza kiasi gani huko njiani hapa hampiti, wala hatujali Mungu wenu ni nani.Musa akamwambia Joshua achague watu watakaokwenda kupigana  na Amaleki, lakini Musa akaenda mlimani na vita ikapiganwa na Israeli wakashinda. Vita ilipokwisha Mungu akaapa kwamba atakuwa na vita na waamaleki kizazi hata kizazi. Musa akasema nataka nijenge madhabahu ya vita na Amaleki.

Leo na sisi tunajenga madhabahu ya vita na Amaleki  kwa maana yupo Amaleki kwenye maisha yetu leo, hata Tanzania Amaleki yupo pia.Lakini Bwana ameapa atakuwa na vita naye kizazi hata kizazi.

AMALEKI NI NANI HATA TUMJENGEE MADHABAHU YA VITA?

Mungu aliwaambia wana wa Israeli nendeni kwenye nchi niliyowapatia, nchi ya ahadi halafu wakatokea watu wakawa wanawazuia wasiende. Amaleki ni mtu yeyote anayezuia usiende ambapo Bwana Mungu anasema uende. Amaleki ni yule anayezuia afya yako wakati imeandikwa kwa kupigwa kwake sisi tumepona, yule anayezuia ndoa yako, anauzia uzao wako. Amaleki amekaa pale. Leo tunajenga madhabahu ya vita na Amaleki ili kila aliyezuiwa naye aje kupigania kwenye madhabahu hii.

 

Maombi:

Katika jina la Yesu, ninamfuata kila Amaleki wa maisha yangu kwa maana imeandikwa Bwana ni mtu wa vita na Bwana ndilo jina lake, nami kwa mamlaka ya jina la Yesu leo ninawafyeka wote wale waliopanga vita nami katika habari ya mafanikio yangu. Kwa maana imeandikwa mimi ni rungu la Bwana na silaha za vita vyake,  nami kuanzia sasa kwa mamlaka niliyopewa navunja kila madhabahu iliyowekwa hapa kama ya Amaleki leo ninaivunja kwa moto wa Bwana. Kwa maana Imeandikwa  mtapokea nguvu  akishawajilia Roho mtakatifu, nami naanzia katika nchi yangu ninafyeka wale wote waliofunga mafanikio  ya nchi yangu kwa jina la Yesu. Ninampiga na kumtupa nje kuanzia sasa. Ninafyeka majoka kwenye ulimwengu wa roho na wote ambao wamenivurugia maisha kwa nia ya kupindisha kusudi la Mungu kwenye maisha yangu. Kwa maana imeandikwa nao wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo, nami ninapiga mikataba yao kwenye ulimwengu wa roho na majoka yote yaliyofunga maisha yangu na kila mmoja aliyenifunga ninamponda kwa rungu la Bwana.  Kwa maana imeandikwa kulikuwa na ita Mbinguni na yule joka akatupwa nje, nami kwa mamlaka ya jina la Yesu kila aliye nifunga ninampiga, na kila aliyeifunga nchi ya  Tanzania  ninamchinja kwa jina la Yesu.

Baba katika jina la Yesu  Asante kwa maana wewe umefanyika daraja la ushindi kwa mama huyu na baba huyu pamoj na kaka huyu. Kuanzia sasa ninatangaza ya kwamba ameshInda vita na kila aliyemloga mtu huyu ninamtumia moto kokote alipo, yale mapepo yaliyoleta maneno ya aibu au magonjwa ya kumfunga leo ninayasambaratisha kwa jina la Yesu. Natangaza ya kwamba mtu huyu ameshinda vita na hakuna uharibifu tena juu yake  kwa jina la Yesu.

AMEN.




 


Post a Comment

0 Comments