google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

THIS IS MY STORY: Ushuhuda wa Kichaa cha Naomi

THIS IS MY STORY   -  JUMAPILI  07.09.2014

Mwalimu Malinga na mke wake, wameokoka muda mrefu sana na ni wakazi wa Bigwa Morogoro. Kabla ya tukio hili, Mzee Malinga alikuwa Kiongozi (Mzee wa kanisa) katika Kanisa la TAG - Moria (lililopo Mtaa wa Kola B - Morogoro).


Mzee Malinga (katikati), mkewe (kushoto) na Baba
(SNP Dr. Godson), wakati familia hii  ikishuhudia
matendo makuu ya Mungu kwa mtoto wao Naomi.
Familia hii wana mtoto anayeitwa Naomi, ambaye alifaulu vizuri form 4, na
tarehe 27 March 2014 ilikuwa birthday yake. Hata hivyo, Jioni ya hiyo siku ya tarehe 27 March mwanae alianza kuona watu ambao walikuwa wanamfuata sebuleni ingawa baba yake alikuwa hawaoni. 


Katika wale watu aliokuwa anawaona miongoni mwao ni  majirani za familia hii, na ambao miongoni mwao watoto wao hawakuwa wamefaulu kama Naomi. 


Usiku ule Naomi (mwanae) alikuwa anakimbia kimbia ovyo, na kumgongea mlango baba yake akisumbuliwa na wale wachawi. Maajabu Naomi alikuwa na macho ya kuona watu ambao wasioonekana kwa baba yake waliokuwa wanamvizia. Ndiposa Baba yake aliwaza pengine ni malaria imepanda kichwani kwa mwanane. 


Kuna wakati baadae baba alitaka kumsaidia mwanae, lakini looh, Naomi akamwambia baba yake kuwa amechelewa na huyo  mtu aliyekuwa anamfuata akimvizia kutaka kumchinja na kisu na keshaondoka zake.


Mama mzazi wa Naomi alikuwa ameenda Moshi kipindi hiki cha kuanza kwa hili  tatizo. Baba yake Naomi alimpeleka kwa Mchungaji wa TAG ambapo anaabudu, na akafanyiwa maombi na kuazimia kumuacha kwenye hii nyumba ya mchungaji. Hata hivyo mwanane kuanzia siku ile alikuwa halali kabisa usingizi wowote.


Siku moja Naomi alitoroka na alipopatikana alipelekwa hospitalini, ingawa alikutwa hana tatizo kubwa la malaria, kwani hakuwa na vimelea vya malaria vyenye kuhitaji matibabu. 



Siku iliyofuata alipatiwa tiba nyingine ya 'quinine' na kila mara akawa anaongezewa dozi. Madakatari walikiri aina hii  ya malaria haijawahi  kufahamika au kuwepo kwenye taaluma zao. Madaktari  walipendekeza pengine aanzishiwe dozi ya wenye vichaa. 


Dozi ilianza lakini pia wazazi na madkatari wakapendekeza kuwaona watumishi wa Mungu. Muhimbili ikawa sehemu ya mwisho, na ambapo madaktari walishauri kama wazazi wanataka kwenda kwa waganga wa kienyeji sawa, au makanisani kuombewa sawa, wafanye hivyo. 


Wazazi walimpeleka Majumba Sita  Dar es Salaam akaombewa penye kanisa la TAG, na baada ya maombi, Naomi akawa ametulia na kulala. Walimuacha mwanae mahali pale akiombewa, na huku ile hali inamrudia kila baada ya  siku. 


Muda wa mwanae kwenda shuleni  ukawadia,  na wazazi wakaenda kumchukua kutoka huko Dar es Salaam. Hata hivyo fujo ziliendelea  kuwa kubwa zaidi, na Naomi alikuwa akitaja majina ya watu wakubwa serikalini, na hata wasanii kama akina Kanumba n.k. alipotajiwa kwenda shule,  ndipo kabisa aligoma katakata  na kusema hana mpango wa kwenda shuleni tena.


Wapo ndugu waliomshauri ampeleke Moshi kwa sababu kuna sehemu ya maombi mazito. Mzee Malinga kwa kujali alifunga safari  kwenda Moshi na Naomi. Ilibidi amfunge miguu mwanae ili asimtoroke. Njiani alipata shida sana kumepleka, kwani alikuwa anakataa kufuatana na baba yake na hata kunyanyuka  kwenye kiti cha basi  na kuanza kucheza nyimbo za TV ya lile basi mbele ya abiria wote.  


Mbaya zaidi,  Naomi akiwa njiani alikuwa anasema baba yake  anataka kumtoa kafara, jambo ambalo lilifanya abiria waingilie kati na kujua kulikoni? Walipofika Moshi,  mzee huyu alikodi Guest House yenye double beds ili kuhakkikisha kuwa mwanae hatatoroka, lakini  mwanane akagoma kulala akipiga makelele kwamba baba yake amefanya hivyo ili apate nafasi ya kumbaka. Baba huyu alijisikia vibaya sana na aibu ikawa inampata. Palepale  Baba yake  alipewa wazo la kutafuta hosteli ya masista pale Moshi na
ambapo  mwanane alikubali kulala pale hosteli.


Kesho yake alimpeleka mwanae  kwa 'Yule  Mtu wa Maombi'. Mzee Malinga anakiri kuwa toka amekulia wokovu hakuwahi kukutana na aina hii ya maombi. Kwa nini? Anasema ni aina ya  maombi ambayo mwanae aliambiwa aizunguke madhabahu,  na kisha kunyweshwaa maji ambayo hakufahamu yana kitu gani. Hata hivyo maombi yale hayakumsaidia mwanae.


Alirudi Morogoro, ikabidi wampeleke upya Naomi Hospitalini, na ambapo madkatari walishauriana kumuanzishia huyu mtoto dozi ya kutuliza watu wenye kichaa.  Pale hospitalini hata hivyo, alikuwepo Dr. Loice wa Hospitali ya Saba saba (Majeshi Majeshi) ambaye aliwashauri wazazi hawa wampeleke Naomi Kanisani Ufufuo na Uzima Morogoro,  kwani alibaini kuwa tatizo kama hili tiba yake siyo ya Hospitalini tena. Hata hivyo, wazazi walikuwa na taarifa hasi dhidi ya Kanisa hili. Walijishauri sana juu ya  wazo hilo, wakisema endapo makanisa yote waliyokwenda shida ya Naomi haikutatuliwa,  je, Kanisa la Ufufuo na Uzima watawezaje? Hata hivyo  walitii na kesho yake wakafika kanisani ambapo walipokelewa vizuri na maombi kwa Naomi yakaanza rasmi. Kuanzia siku ile, Naomi alianza kufunguliwa na kuanza kurudiwa na ufahamu wake. haikuchukua muda mrefu, wazazi wakiwa wanamleta Naomi kwenye Mkesha na Ibada za katikati ya wiki, Naomi akawa mzima kabisa.



Baba na Mamawa Naomi Malinga wakitoa sadaka ya
Shukrani na Dictionary ya Biblia kumshukuru Mungu
aliyemponya Naomi kutoka kwenye Maradhi /
Ukichaa wa kutengenezwa  07/09/2014.
Wazazi wa Nomi kwa pamoja  wanakiri kuwa Naomi amepona kabisa na sasa amejiunga na shule ya Sekondari Mpanda na hata walimu wake wanakiri kuwa Naomi ni mzima kabisa. Baba na mama wa Naomi wameamua mchana kweupe  kujiunga na Kanisa la Ufufuo na Uzima Morogoro. Wanahuzunishwa sana na tuhuma zilizokuwa zinafanywa dhidi ya Kanisa hili kulichafua kuwa ni mojawapo ya 'frremasno'. Wazazi hawa kwa pamoja  wameamua  kuwa  wapo tayari kumtumikia Mungu wa Ufufuo na Uzima kwa matendo ambayo wameshuhudia Mungu huyu akifanya, na zaidi sana kwa kumponya Naomi.

Post a Comment

0 Comments