Sunday, December 7, 2014

MALAIKA WA KUZIMU


 

 

 
SOMO; MALAIKA WA KUZIMU

NA MCHUNGAJI KIONGOZI: JOSEPHATI GWAJIMA

TAREHE: 07-12-2014

Neno malaika maana yake ni mjumbe wa Mungu hana jinsia, anaweza kuwa katika mwili au la. Neno kuzimu limeandikwa mara 73, na kwa namna nyingine limeandikwa kama shimoni mara 41. Maadui kulekule wanakokupoleka ilikukutendea mabaya, ndo huko huko unaenda kukutana na BWANA.  Kweli ni Mungu lakini kweli inaghalimu.Mungu hakutupa roho ya woga bali moyo wa kiasi na uthabiti. Imeandikwa;

 usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.    Isaya 41:10

 

Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu.
Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni.  Nzige wakatoka katika ule moshi, wakaenda juu ya nchi, wakapewa nguvu kama nguvu waliyo nayo nge wa nchi.
Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya nchi, wala kitu cho chote kilicho kibichi, wala mti wo wote, ila wale watu wasio na muhuri ya Mungu katika vipaji vya nyuso zao.  Wakapewa amri kwamba wasiwaue, bali wateswe miezi mitano. Na maumivu yao yalikuwa kama kuumwa na nge, aumapo mwanadamu.  Na siku zile wanadamu watatafuta mauti, wala hawataiona kamwe. Nao watatamani kufa, nayo mauti itawakimbia. Na maumbo ya hao nzige yalikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao kama taji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama nyuso za wanadamu. Nao walikuwa na nywele kama nywele za wanawake. Na meno yao yalikuwa kama meno ya simba. Nao walikuwa na dirii kifuani kama dirii za chuma. Na sauti ya mabawa yao ilikuwa kama sauti ya magari, ya farasi wengi waendao kasi vitani.
Nao wana mikia kama ya nge, na miiba; na nguvu yao ya kuwadhuru wanadamu miezi mitano ilikuwa katika mikia yao.
 Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni.
Ufunuo 9:1-11

Utajiuliza kwanini ufundishwe malaika wa kuzimu na sio malaika wa Mungu?Inashangaza sana kuona  malaika kutoka mbinguni anaufunguo na wa kuzimu na akafungua mlango wa kuzimu moshi wa shimoni ukatanda juu ya anga.Abadoni maana yake mharibifu-mharabu. Hivyo kazi yake ni kuharibu ndoa, familia, afya, nchi na kila kitu. Na pia anaharibu makusudi. Imendikwa;

Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. Yohana 10;10.

Hakuna mtu anayewekuzuia kwenda kwenye safari yangu ya mafanikio uliyopangiwa na BWANA.Nyota ni alama ya malaika,kwa kalenda ya Mungu,Mungu ameweka mitihani ya kukufikisha katika ngazi nyingine.Imeandikwa;

 Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.Ufunuo 1:20

Mungu kila akitaka kukuvusha anaruhusu mitihani ili aone utakavyoikabili. Mitihani ya kulogwa, balaa lakini Mungu ametupa roho mtakatifu atupaye kushinda kwa damu ya Mwanakondoo.  Imendikwa;

 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. Ufunuo 12:11

Kabla wana wa Israel hawajaingia nchi ya ahadi, ulikuwepo mto jordani, Mungu anaweza kuondoa kila kitu na aone kama utaendelea kumpenda? Mungu anatengeneza njia katikati ya bahari, Mungu atabaki kuwa Mungu tu hata pasipo mwili utamuona  BWANA. Matatizo sio matatizo kila siku, lakini kwa namna unavyoitikia kwenye matatizo waweza kutengeneza matitizo mengine. Hakuna tatizo lakudumu katika kuishi kwako, bali kila tatizo lipo ili kukupigisha hatua ya maisha yako.

Mtu anayesema kuzimu haipo anamatatizo makubwa. Kuzimu ni makao makuu ya shetani hapa duniani, ndiko kiti cha enzi cha shetani kilipo.Imeandikwa;

Kama vile wingu likomavyo na kutoweka, Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa Ayubu7:9,

Maana mautini hapana kumbukumbu lako; Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?  Zaburi 6:5,

Tuwameze hai kama kuzimu, Na wazima, kama wao washukao shimoni.    mithali 1:12

 

Kuna viumbe wa kiroho wanafanya mambo katika ulimwengu wa roho, unapata matatizo katika ulimwengu wa mwili. Uwezo wako wa kushinda katika ulimwengu waroho, ndio uwezo wako wa kushinda katika ulimwengu wa mwili. Kabla ya aibu ya mwilini, inaanzia aibu ya  rohoni, magonjwa ya mwilini yanaanzia rohoni. Lakini Yesu alikufa ili tupate kuwa huru.Imeandikwa;

 Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako na kukuinamia; Nao wote waliokudharau Watajiinamisha hata nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa Bwana, Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli.     Isaya 60:14

Ezekieli31:15, Amosi 9:2 Yona 2:2, Habakuki 2:5 watumishi wa Mungu hawa katika agano la kale walijua kuwa kuzimu ipo. Na pia katika agano jipa Mungu Yesu Kristo alijua kuwa kuzimu ipo. Imeandikwa;

Mathayo 16:18

Mchawi ni mtu anaweza kuwa mwanaume au mwanamke, anaenda kuzimu na kupokea uchawi na nguvu kutoka kuzimu kilipo kiti cha enzi cha shetani. Mshetani waliotoka kuzimu walikuwa na sura ya wadudu, wanadamu, wanyama, hii ni alama kuwa shetani kwa lengo moja la kuharibu atajitokaza katika sura mabli mbali.|Na silaha ya shetani kubwa ni kujificha usimjue, ili apate kuharibu. Kuna kundi la watu na sio watu wa kawaida na wameelekezwa ili wapate kuharibu maishs yako, lakini Mungu naye amaefungua mbingu apate kuwaokoa watu wake.

Unaweza kumuona mtu anavazi la kondoo, kumbe ni mbwa mwitu, anasura ya kibinadamu lakini kumbe ni waharibifu.

Mawazo ya watu duniani ni kuwa usiyemwabudu Mungu ndo mwenye mafaniko, jambo hili sio kweli. Mungu anasema katika mithali nawapenda wale wanipendao na o wanitafutao kwa bidii wataniona naamu na mali idumuyo ni yao. Mungu akikupa maekupa, lakini shetani akikupa ukikiuka mashsrti yake anakunyanganya. Kuna watu kilia wakianza kiti cha mafanikio wanaharibikiwa maana shsetani yule aharibuye anafanya kazi ya kuharibu kila unachokitengeneza.Imeandikwa;

Ayubu 9:31

Ayubu 33:8

Zaburi 28:31

Mithali 1:12

Isaya 22:42

Inawezekana shetani asikuchukue mzima mzima,  akachukua mikono ya mtu au vipawa, muonekano, upendeleo, navyo viksenda shimoni.Imeandikwa;

 Ili kurudisha roho yake itoke shimoni, Ili atiwe mwanga kwa mwanga wa walio hai.  Ayubu 33:30,

 Kwa namna hii inaonesha kuwa hata kama mambo yanaweza kupelekwa shimoni bado yanaweza kurudishwa toka shimoni. Kuna mashimo madogo madogo, na binadamu hawezi kufanya kitu chochote pasipo kupewa na Mungu. Kuna eneo la mtu limebarikiwa na kupitia eneo hilo apate kuingia kwenye hatima yake.Shetani hajawahi kuumba kitu chochote, kazi yake ni kuchukua vitu vya watu walivyopowa na Mungu anawapelekea wachawi, nao wanatumia kana kwamba wametengeneza wenyewe. Kuna amabaye siri yake ni ujasiri, ndani ya moyo wake, wachawi wanaweza kutumia ujasiri wako wanatisha watu. Na walio barikiwa miguu yao, kila anakokwenda anafanikiwa, lakini kama imeibiwa waweza kujikwaa mara kwa mara, na ukaanguka mbele za watu.

Shetani anaweza kugeuka na kuwa kitu chochote. Utajiuliza kwanini mtu akitaka kumloga mtu ahawezi kusema ntaenda London, au Kenya? Hii ni kwa kuwa shetsni amechagua maeneo na huko ameweka madhdbahu yake mfano kama unavyosikis Sumbawanga.

 

 

Ukiri

 Kwa jina la Yesu nakataa mahali popote kitu changu chochote kinapotumiwa na shetani. Naamuru miguu, biashara, akili, na maisha yako yaliyowekwa kwenye madhdbahu ya kishetani katika jina la Yesu. Na mashetani wote mlioniweka hama kwajina la yesu, toka katika jina la yesu.Kuanzia sasa chochote kila kilichowekwa kwenye shimo nakirudisha katika jina la Yesu.

Kwa damu ya yesu, macho yangu, moyo wangu kinywa changu, nyota ya kazi,  nyota ya umahiri, utawala, ndugu wa karibu, aliyeiba nyota ya maisha yangu teketea kwa jina la Yesu. Nyota yangu njoo kwa jina la Yesu. Nyota ya kupendwa njoo kwa jina la Yesu, nyota ya ndoa, safari, uso, njoo kuanza leo. Nawaamuru muondoke leo kwa jina la Yesu. Amina.

 
MAOMBI

Kila mzimu, jinni, pepo uliyechukua nyota yangu, uso wangu, utawala wangu, tumbo langu, akili yangu naamuru teketea kwajina la Yesu. Kila maisha bandia, maishs yasiyoyangu naamuru kazi za kichawi juu yangu ziteketee kwa jina la Yesu. Natangaza vita kwa jina la yesu. Kwa jina la yesu mahali popote ambapo nyota ya maisha yangu, kazi yangu au uso wangu umechukuliwa na kuwekwa kwenye mashimo ya kichawi rudisha leo kwa jina la yesu, rudisha uso, rudisha ndoa, rudisha tumbo kwa jina la Yesu.

Kwa jina la yesu mtu yeyote aliyechukua chochote cha maishs yangu, naamuru akili yangu, afya yangu, kazi yangu

Yawezekana hujui kama ungekua zaidi ya ulivyo leo na bahati mbaya hujui kama umeibiwa, umetekwa, au kiungo chako kama kimeibiwa naamuru mashetsni wadhdihirike na akujulikana katika jina la yesu. Naamuru moto wa BWANA uwake na ujue kuwa umeibiwa na kila kilichoibiwa kirudishwe leo katika jina la Yesu.Nakataa kwa jina la Yesu. Kuanzia leo nazima moto wa shimoni, uliowashwa kinyume na afya yangu kinyume na uzima  wangu kwa jina la laYesu. Kwa jina la Yesu ninazima moto wa shimoni uliowaka kinyume na maisha yangu, naamuru kuanzia sasa jini kutoka baharini namuwasha kwa moto wa Mungu.Mzimu wa ukoo, uliotumwa kuniua kabla ya wakati wangu kamba za mauti katika kwa jina la yesu. Kamba za mauti katika kwa jiana la Yesu.


Kwa damu ya mwana kondoo narudi kwenye asili yangu. Nakataa asili ya kishetani nilivishwa na wachawi. Narudi kwenye asili yangu kwa jina la yesu. Kila uchawi na ushsirikina uliopandwa kwenye famila yetu naurudisha kwa damu ya ya Yesu. Narudisha moyo wangu, ndoa yangu kwa damu ya Yesu, narudisha akili yangu iliyoibiwa na mashetani walionijia wakati niko usingizini, naamuru kuanzia sasa asili bandia rudi ulikotoka kwa jina la Yesu. Narudi kwenye asili yangu asili ya afya asili ya Baraka, asili ya ndoa, asili ya huduma, asili ua amani, asili ya amani, asili ya mafanikio katika jina la  Yesu. Imeandikwa nimepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na ng’e, nakanyaga kila adui aliyeniibia asilis yangu kwa jina la yesu.narudi kwenye asili yangu leo asili ya utawala, asilis yautajiri, asili ya kupambanua katika jina la yesu. Kila moyo ulioibiwa, tumbo lililoibiwa, ufahamu, kazi, ndoa kino famila iliyoibiwa achia kwa jina la yesu  nnoo kwa jina la yesu, naamuru uso wangu nnjoo kwa jina la yesu.naamuru koto war oho mtakatifu uwake uteketeze kila aliyeshikilia maishs yangu, famila yangu kazi yangu nyota yangu, huduma yangu afya yangu, hatiama yangu huduma yangu katia jina la yesu. Naamuru kila kilichooharika ndani ya maisha Yangu kiwekizima sasa katika jina la Yesu. Miguu iliyowekwa kwenye viwanja vya wachawi  naamuru irudishwe katika jina la yesu. Kuanzia leo uwe mwanzo wa ushindi katika jina la Yesu.USHUHUDA.
 Binti huyu alikuwa ameibiwa akili kwa muda mrefu na yule mharabu. Alipokuwa shule alikuwa akisumbuliwa na  mapepo mara kwa mara. Hali huzidi kuwa mbaya wakati wa mitihani. Hali hii ilipelekea yeye kufeli mitihani yake ya taifa ya darasa la saba na kidato cha nne.  Amefanikiwa  kujiunga na chuo cha ualimu lakini baada ya maombi na kufunguka amegundua kuwa alikuwa kwenye usingizi mzito na kuwa hakupaswa kuwa hapo alipo leo. Baada ya kufunguliwa ana ari mpya ya kufika pale ambapo Mungu amempangia kufika.

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment