Dunia yote inafahamu kuwa matatizo ni asili, tatizo unaloliona kuna nguvu nyuma yake unapo kuwa unaishi kuna nguvu inang’ang’ana kukuongoza katika vitu unavyo vifanya. Kila mtu unaemuona duniani anawakilisha nguvu fulani ya ki Roho au ya shetani kila mtu unamuona anatembea kuna mamlaka nyuma yake inayo msukuma kufanya jambo fulani au mambo fulani ukimuona mtu amesima ujue kunanguvu iliyo msimamisha ikiwa nguvu ya Mungu itamuongoza katika njiailiyo sahihi kuipita lakini kama ni nguvu ya kishetani ipo nyuma yake basi itamshusha chini
Kuna watu wamepewa macho yakuona biashara na macho yakuona
nguvu iliyo nyuma ya biashara kuna watu wanajua umekiribia kupata lakini kuna
watu wakaanza kukutumia vitu vya kukukwamisha. Mungu anaweza kukuvusha katika
matatizo yako yote unayo pita mchawi ukimtambua hana uwezo tena wakukumaliza
wala kukujalibu.
Biblia inasema mtu mwenye akili nyingi ndio mtawala shetani anapenda mtu anayesema hakuna uchawi iliapate kumroga vizuri, wachawi wakiona jambo limenyooka wanataka kulipindisha, mafanikio ya mtu haya andaliwi na urefu wa mtu au ufupi wa mtu. Kuna watu walijenga vibanda ili waanze biashara lakini hawakufanikiwa na wao wakaona kama ni kitu cha kawaida ulianza kwa huzuni utamaliza kwa heshima kuliko ndugu zako wote. kuna mambo mengine mtu anayaona ya kawaida lakini mtu mwingine kwake haoni kama ni mambo ya kawaida.
Matatizo hayaja ruhusiwa na Mungu ili ya kumalize ila matatizo ya ruhusiwa na Mungu ili ya kunoe kwaajili ya kesho yako. Dunia haikupi kile unacho kitaka ila inakupa kile unacho kipigania, Mungu anajua kile unachotaka lakini hawezi kukupa mpaka useme. Kuanguka kupo lakini tatizo ni kubaki pale ulipo angukia ukianguka simama upambane kupiga hatua nyingine .Vita ya maisha lazima upigane hadi mwisho Mungu anaweza kukutoa chini na kukuweka juu lipo jambo Mungu anakuwekea ili uje kulitenda shetani alikuwa mpendwa wa Mungu kila mtu aliye kusaliti atapigwa mpaka pande za mwisho kuzimu kama alivyo pigwa shetani mpaka pande za mwisho kuzimu sio kila wanaoitwa na Mungu hawana makosa Mungu awapa sifa wale wasiokuwa na sifa.
KANUNI YA USALITI:
1/ Kila unalolipanga kwaajili ya mtu unajipangia mwenyewe
2/ Wasaliti hufa wao kabla ya kukuuwa wewe
3/ Kila unayemuonea wivu unamkatia leseni ya kwenda juu,
wivu ni namna ya ndani ya ukili
4/ Kila wenye wivu uishi muda mfupi
Huwezi kusikia kama unausaliti au wivu ndani yako maana maumivu yanaweza kugeuka kuwa majeraha ndani yako kila mtu aliye na maumivu hawezi kuishi muda mrefu nyuma ya unaye mpenda kun amipango ya kukuteketeza.
1 Samweli 18:20-27
“Walakini Mikali, binti Sauli,
alimpenda Daudi; watu wakamwambia Sauli, na neno hilo likampendeza. Naye Sauli
akasema moyoni, Mimi nitamwoza huyu, awe mtego kwake, tena kwamba mkono wa
Wafilisti uwe juu yake. Basi Sauli akamwambia Daudi mara ya pili, Leo utakuwa
mkwe wangu. Naye Sauli akawaagiza watumishi wake, Zungumzeni na Daudi kwa siri,
na kusema, Angalia, mfalme anakuridhia, na watumishi wake wote wanakupenda;
haya basi! Na uwe mkwewe mfalme. Nao watumishi wa Sauli wakanena maneno hayo
masikioni mwa Daudi. Daudi akasema, Je! Ninyi mwaona kuwa ni shani mimi kuwa
mkwewe mfalme, nami ni maskini, tena sina cheo? Na hao watumishi wa Sauli
wakampasha habari, wakisema, Ndivyo hivyo alivyosema Daudi. Naye Sauli akasema,
Mwambieni Daudi hivi, Mfalme hataki mahari yo yote, ila anataka govi mia za
Wafilisti, ili ajilipize kisasi adui za mfalme. Basi Sauli alidhani
kumwangamiza Daudi kwa mkono wa Wafilisti. Na watumishi wake walipomwambia
Daudi; maneno hayo, ilimpendeza Daudi sana kuwa mkwewe mfalme. Na siku zilikuwa
hazijaisha bado; basi Daudi akainuka, akaenda yeye na watu wake, akaua katika
Wafilisti watu mia mbili; na Daudi akazileta govi zao, wakampa mfalme hesabu kamili,
ili awe mkwewe mfalme. Naye Sauli akamwoza Mikali, binti yake.”
Kuna watu wanatakiwa kufika mahali pazuri lakini wanakutana
na miiba njiani kila njia unapita hata kama kuna magumu kiasi gani simama chomoa
mwiba ili ufikie mafanikio yako, Mafanikio
hayaletwi kwenye sahani ya fedha ukitaka kuwapeleka watu mahali lazima uwe na
ujasiri vitu huja kwa kusema unaposema wewe ni tajiri kweli utakuwa tajiri
hatatokea mtu kukupenda mpaka kufa. Kuna wanaume hawawezi kuondoka kwao mpaka
wagombane. Usijaribu kushindana na mtu maana kila nyuma ya mtu kuna nguvu inayo
mlinda usijaribu kumtoa mtu mahali alipo kuwa maana ujui nani kamuweka hapo
alipo yupo shetani anaye kufatilia ili ushindwe katika mambo unayoyafanya.
BONYEZA HAPA👇👇 KUANGALIA IBAADA NZIMA YA JUMAPILI
BONYEZA LINK HAPA CHINI 👇👇 KUSIKILIZA LIVE IBAADA ZETU
UFUFUONAUZIMA RADIO is on Mixlr https://mixlr.com/ufufuonauzima-radio
0 Comments