google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUSUDI LA MAISHA YAKO

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 21.07.2024
ASKOFU DR JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: KUSUDI LA MAISHA YAKO

Kila mtu anakusudi lake la maisha aliloletewa duniani kama Mungu alivyoona yafaa kwa wakati husika. 

“BWANA alikuwa nami katika mwanzo wa njia yake, Kabla ya matendo yake ya kale”. Mithali 8:22

Kusudi lako la maisha linaweza kuchelewa lakini hata hivyo haimaanishi kuwa Mungu amekusahau. Kuna wakati mwingine kwenye maombi yako unamuonesha Mungu udhibitisho wa jambo fulani zuri ulilomfanyia, mfano unatoa fungu la kumi zile risiti zako unaenda mbele za Mungu kumuonesha risiti zako maombi hayo yanakuwa na nguvu sana.

Kuna mtu mmoja alikuwa analima pamba marekani, mwaminifu, anatoa fungu la kumi, umefika wakati wa pamba  kuanza kutoa watoto (vinaitwa tumba), yeye ana hekta elfu moja anashangaa mashamba ya jirani yametoa tumba ndogo nyeupe kasoro kwake. Akaenda kwa Mchungaji, Mchungaji akamwambia chukua risiti zako za fungu la kumi, wakaenda shambani, Mchungaji akakaa katikati ya shamba akasema ee Bwana ulisema mtu akitoa fungu la kumi utamkemea yeye alaye na hatapatikana mtu wa kumuangamiza. Kesho yake asubuhi walipofika shamba likawa limejaa pamba nzuri nyeupe ikimaanisha nini laana imeondoka kwa udhibitisho wa risiti zake za fungu la kumi.

Kwa nini Yesu alisurubishwa na kuwekwa msalabani? alikuwa anatufikiria sisi, ili dhiki yako ikome. 

Kwenye maisha uvumilivu ni wa maana sana, kwa nini Yesu alivumilia alikuwa analenga mbele, kwa ajili ya wokovu.

Kati ya wezi wale wawili waliosulubiwa nae, mwizi mmoja yuko msalabani lakini anatukana, kuna wengine hapa, hata Yesu akiwa hapa, wengine hata ufanyeje watamkataa Yesu. Cha kujifunza hapa ni watu wengine hata kama uwasaidiaje watakukataa tu.

"Yesu akawajibu, Je! Mimi sikuwachagua ninyi Thenashara, na mmoja wenu ni shetani?" Yohana 6:70

Kila kumi na mbili ukiwaita na shetani yupo, unapoomba Mungu akikuonesha maono au jambo utulie, usianze kusema sema kwa kila mtu.

Hauwezi kujua kuwa una kitu chema mpaka utakapokipoteza. Unaanza na mtu vizuri akipata kitu anakwambia Baba nimepata kazi kibororoni, hapo unajua tu ndo umeshaaachwa. Anayeenda na wewe mpaka mwisho ndio wa muhimu sana. Heri mwisho wa jambo kuliko mwanzo.

Ogopa sana mtu wa Mungu anapokwambia pumzika sana umechoka, hii inamaanisha anataka kukuacha. Eliya alitafuta njia zote za kumuacha Elisha lakini Elisha aligundua na kung'ang'ania hadi mwisho na kurithi sehemu ya Eliya. Hatima ya mtu imeungana na mtu mwingine yaani wewe utakuwa nani kuna mtu fulani umeungamanishwa nae. Mungu anamchagua huyo mtu na ndani yake anawieka kitu ndani yake ambapo anapopanda basi anapanda na wanaomfuata.

"Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu". Yohana 12:32

Kanuni ya kufanikiwa ni lazima mmoja aende ili awavute wengine na wamfuate.

Alipokuwa msalabani akazungumza maneno saba tu ya muhimu. 

“Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” Mathayo 27:46.

Yesu akamwabia Baba yake mbona unaniacha. Yesu alikuwa amebeba dhambi za ulimwengu na tunajua Mungu ni mtakatifu, Mungu akageuza mgongo ili litimie neno aliloandikiwa. Usiwe mwepesi kusema wameniacha jamani, aliyekuacha anaweza kuwa na mpango mwingine juu yako.

Kusudi lako lipo pale pale kwenye maisha yako haijalishi unapitia nyakati gani, USIKATE TAMAA, AMEN.

Post a Comment

1 Comments