Bishop Josephat Gwajima |
MAOMBI YA KUMUOMBA MUNGU ALIAHIRISHE LILE JAMBO BAYA ALILOLIPANGA ATALILETA KWENYE MAISHA YAKO
Maombi haya yana uwezo wa kuleta matokeo makubwa Kwenye maisha ya mtu. Kwa kawaida mtu anapotenda uovu, Mungu huwa anapanga kuleta uovu juu ya mtu huyo, hata Kama Mungu alikuwa anakupenda, au amekutumia kwa kiasi gani, unapotenda uovu Mungu anakawaida ya kuruhusu mabaya yaje juu yako pale unapotenda uovu.
Imeandikwa: Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. (UFU. 3:19 SUV).
Mungu anaonyesha asili yake, wale anaowapenda huwa anawakemea na kuwarudi, ukiona Mungu hakukemei unapofanya maovu ujue Mungu hakupendi.
Mungu huwa anakemea watu, na kwenye kukemea kule ndio unaweza kuona mtu amepata jambo baya, kama ajali, magonjwa,shida na taabu mbalimbali.
Imeandikwa : tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye; Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye. Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? (EBR. 12:5-9 SUV)
Mungu anapokupenda, akiona unaanza kwenda Kwenye njia iliyoopo toka , Mungu anaruhusu jambo baya linakupata ili kukurudishia katika njia iliyonyooka.
Biblia inasema mabaya hayatakupata wewe, kwahiyo unapoona mabaya yanaanza kukupata unakua ni lugha ya Kimungu ya kukuonya uache hiyo njia unayoiendea,
Mungu anakurudi kwa kutumia tukio, anaruhusu tukio likupate ili kukurudishia katika njia unayoiendea, na Mungu anaweza kulirudi taifa, mchungaji au mtu yeyote kwa kuruhusu tukio limpate.
Ndio sababu Mungu anawaruhusu hata watumishi wake kukemea
Imeandikwa : lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. (2 TIM. 4:2 SUV)
Imeandikwa :Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote. (TIT. 2:15 SUV)
Imeandikwa :, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu. (UFU. 2:5 SUV)
"Kukiondoa kinara chako"maana yake ni kuruhusu mabaya yakupate, au nitaongea na wewe kwa njia ya matatizo.
Ni kama ambavyo sisi ni wazazi, wakati mwingine tuna wachapa watoto wetu, yamkini inaweza kana ukawa inauma, lakini tunakua tukijua kwamba ni kwa faida ya mtoto, ndivyo alivyo na Mungu pia
Mtu anaweza kufanya maovu tena na tena mpaka malaika wa huruma anaondoka, na malaika wa huruma anapoondoka Mungu anaruhusu mabaya .
Inaweza kana kuna mambo umetenda 2014 na Mungu amepanga kukupigania 2015, yawezekana hakuna mtu anayefahamu kuhusiana na mambo unayoyatenda, na Mungu amekua akiuonya Mara nyingi bila wewe kusikia, Leo tutamuomba Mungu ili kuahirisha lile jambo alilolipanga baya juu ya Yale uliyoyatenda.
Wana wa Israel Mungu aliwatoa kutoka katika nchi ya utumwa kwa gharama kubwa, na walipoingia katika nchi ya Ahadi walianza kufanya yaliyo mbele za Bwana, Mungu akaanza kuwaambia mabaya yatawapata, mtachukuliwa utumwani, mtachinjwa na mambo Kama hayo.
Mungu alikuwa anazungumza kwa vinywa vya watumishi wake,
Imeandikwa : Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je, ataishi? Katika matendo yake yote ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa lile alilolikosa, naam, katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa. (EZE. 18:24 SUV)
Hapa unaona mtu anaweza akaanza vizuri, lakini baadae akageuka na kuanza kufanya yaliyo maovu, biblia inasema utakufa katika uovu huo.
Kuna watu matatizo that aondoke pale tu utakapomuona kuacha njia ya uovu unayoiendea.
Imeandikwa :Nimwambiapo mwenye haki, ya kwamba hakika ataishi; kama akiitumainia haki yake, akatenda uovu, basi katika matendo yake ya haki, hata mojawapo halitakumbukwa; bali katika uovu wake alioutenda, atakufa katika uovu huo. (EZE. 33:13 SUV)
Kufa kuna hatua, kuna matukio yanaweza kukupata Kama magonjwa au ajali ilimuishie kufa, Mungu anayo kawaida ya kutotenda jambo bila kuwajulisha watumishi wake, ndio sababu amekua akikuonya tena na tena ili uache uovu Kabla hujafa
Imeandikwa :Maana BWANA asema hivi, Tazama, nitakufanya kuwa hofu kuu kwa nafsi yako, na kwa rafiki zako wote; nao wataanguka kwa upanga wa adui zao, na macho yako yataona hayo; nami nitatia Yuda yote katika mikono ya mfalme wa Babeli, naye atawachukua mateka mpaka Babeli, na kuwaua kwa upanga. (YER. 20:4 SUV)
Mungu alikuwa akiyazungumza haya Kabla hayajawapata ili waweze kutubu, na Yeremia alikuwa akiwaonya tena na tena lakini hawakusikia.
Hakuna mtu yeyote aliyemuona Mungu wakati wowote, na Mungu huwa anazungumza kwa vinywa vya watumishi wake. Na baadhi ya watu bila kufahamu wanakua na desturi ya kushindana na mtumishi wa Mungu akifikiri anashindana na mtu.
Hii inasababisha maovu yaje katika maisha yako.
Hakuna furaha katika dhambi. Dawa ya dhambi ni kutubu.
Nimeonyeshwa katika Roho Mtakatifu kwamba kutokana na maovu uliyoyatenda Mungu amepanga akukemee, lakini makemeo yake yanaweza Kuwa ya uchungu sana. Ndio sababu unatakiwa umuombe Mungu msamaha ili mabaya yaliyokusudiwa katika maisha yako yasikupate.
Waweza kusikiliza maombi ya siku ya kwanza kupitia link ifuatayo
https://www.youtube.com/watch?v=zoMuYl2a4jI&feature=youtu.be
0 Comments