MCHAWI ANASWA KATIKA MKUTANO WA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Ikiwa ni siku ya tatu ya mkutano wa ufufuo na uzima
unaoendelea katika viwanja vya vya shule ya sekondari ya morogoro mchawi mmoja
aliyejulikana kwa jina la Fatuma amekamatwa katika mkutano huo akiwa yuko
katika shughuli zake za kila siku za kichawi.
Dada huyo aliyekamatwa na Nguvu za Mungu alielezea akasema alikuwa
na wenzake ambao walitumwa na bosi wao ambaye ni mchawi na mganga wa kienyeji
maarufu kutoka mjini Bagamoyo wilaya ya pwani kuja katika mji wa Morogoro
kuchukua miili ya watu waliokufa katika nyumba za kuhifadhia maiti za hospitali(mochuari)
kwa ajili ya kitoweo.
Akizungumza alisema yeye na wenzake walipoteana walipofika
karibu na hospitali ya rufaa ya mji wa Morogoro ambapo ni eneo la jirani na
sehemu mkutano unapofanyika, alipofika maeneo hayo alisikia nguvu inamvuta kwa
nguvu na kumpeleka asipotaka yeye ndipo alipojikuta ametua katika viwanja shule
ya sekondari ya Morogoro ambapo ndipo mkutano unapofanyika
Dada huyo aliyeonekana kuwa na wasi wasi alisema tulikuja
mimi na wenzangu kwa usafiri wa njia ya fisi lakini tulipokaribia hospitali
sijui nini kimetokea na mimi nikasikia nguvu zinanivuta nikajikuta niko mahali
hapa
ALIANZAJE UCHAWI
Akielezea jinsi alivyoanza uchawi alisema miaka kumi na tano
iliyopita alikua anaumwa ndipo alipoamua kuondoka kwao Babati(Manyara) kwenda
kutibiwa mkoani Pwani kwa mganga aliyejulikana kwa jina la Idi. Alipofika kwa
mganga aliambiwa akachume pilini dawa Fulani na aitafune, alipofanya sawasawa
na maelekezo ya yule mganga ndipo alipojiona anaanza kuingiwa na ukatili usiokuwa
wa kawaida na akaanza kupata hamu ya kula wanadamu wenzake, kuanzia siku hiyo
ndipo alipoanza kuagizwa na Idi kwa ajili ya kufanya shughuli za kichawi pamoja
na wenzake.
NAMNA ALIVYOKUWA AKITENDA KAZI
Yeye na wenzake walikuwa wanawashughulikia hasa watu ambao
waliokoka na baada ya hapo wakarudi nyuma, akieleza jinsi walivyokua wakiifanya
kazi hiyo alisema mtu yeyote aliyewahi kuokoka na baada ya hapo kumuacha Yesu
anakuwa na majini mawili wanaotumwa kukaa ndani yake, na wachawi hawa
wanapomfuata mtu huyo wanaongea nayale mapepo na wanayaagiza yamnyonge mtu huyo
na mtu huyo anakufa mara moja
Katika utendaji kazi wake yeye ndiye aliyekuwa kiongozi wa
kikundi chake hicho walichokuwa wanatenda shughuli hizo za kichawi.Alisema mimi
niliwekwa kuwa kiongozi wa wenzangu kwasababu mimi nilikua nimefanikiwa kuwaua
watu watatu waliokua wameokoka na kurudi nyuma. Kule kwenye uchawi mtu
aliyefanikiwa kuwaua watu waliorudi nyuma ndie anakua na cheo kuliko wengine,
mimi niliua watu ambao walikua hawajawahi kuokoka zaidi ya thelathini na
waliokua wameokoka na kurudi nyuma watatu alisema dada huyo.
Akielezea alisema sisi tulikuwa na uwezo wa kuwaua watu kwa
matukio tuliyokua tunayatengeneza, unaweza ukakuta mtu anatembea njiani alafu
akawa kama ameumwa na nyoka lakini nyoka mwenyewe hamuoni, mtu huyo baada ya
masaa machache atakufa na sababu itakuwa kwamba aliumwa na nyoka lakini sivyo
tunakuwa ni sisi tumemtengenezea kifo ili tukamle nyama.
WATU ALIOWAHI KUWAUA
Alisema anakumbuka miaka mitano iliyopita alimuua mdogo wake
aaliyekuwa anajulikana kwa jina la Udiyomboli, watu watatu ambao waliwahi
kuokoka na kasha kurudi nyuma pamoja na wengine Zaidi ya thelathini
aliowaangamiza kwa kutumia uchawi
Baada ya hapo dada huyo akiongea kwa huzuni aliomba msaada
akasema, nimechoka kufanya uchawi siyapendi maisha haya na sitaki tena kurudi
kule Bagamoyo.
Dada huyo tayari ameshaachana na mambo ya uchawi na
amempokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yake.
0 Comments