na PASTOR JOSEPHAT GWAJIMA
Mwanzo 28:16-22
“..Yakobo akaweka nadhiri..”
Yakobo alimuwekea Mungu nadhiri hapa, kwa mtu ambae yuko
makini na mambo ya MUngu anaweza kuomba maombi haya, katika maombi yaha
unamuomba Mungu na kumuambia Mungu akama utanifanyia hivi na mimi nitakufanyia
hivi.
Yakobo alipokua safarini kwenda kwa Labani ndipo alipoiweka
nadhiri hii na baada ya kupita miaka mingi akayaona yale ambayo alimuomba Mungu
amtendee yameshatendeka karibu yote, ndipo Mungu akamtokea na kumkumbusha kuwa
ndie Mungu yule aliyemtokea Betheli
Mwanzo 31:13
Mungu ni Mungu atimizaye nadhiri, jina jingine la Mungu ni Mungu ashikaye
maaagano (A covenant keeping God)
Ukiagana na Mungu hawezi kukuangusha katika maagano yenu
kwasababu ni Mungu ashikaye maagano.
Ni kama unakubaliana na Mungu mkutane Mororogoro saa nane
mchana, hata kama Mungu anajua kuwa hautafika Morogoro yeye atakuwepo mahali
hapo kwasababu ni Mungu ashikaye maagano.
Nadhiri inaweza kukupandisha juu sana kama ukiwa mwaminifu
lakini pia nadhiri inaweza ikakuharibu endapo huta itimiza, kwasababu nadhiri
ina kawaida ya kupima moyo kwa kutumia dhamira ya Mungu.
Unapomuaambia Mungu ukinipa fedha nitakufanyia kitu fulani,
Mungu anakupa na inapotokea ukashindwa kuitimiza unakua umeharibu kila kitu
Walawi 22:18
Hapa Mungu alikua anaonyesha wakati mwingine unaweza
ukapitia maisha yenye misukosuko na kufikia hatua maombi yote unayoomba yanakua
kana kwamba hayatendi kazi hapo ndipo wakati wa kutumia maombi ya nadhiri, na
maombi hayo unapoyaomba ni vizuri ukaandika mahali ili usije ukasahau,
usiyaombe kama mtu anayeropoka ili baadae Mungu akishakujibu usije ukawa
umeyasahau.
Ndio maana ya yale maandiko ya umetegwa kwa maneno ya kinywa
chako.
Nadhiri unapoiweka unatakiwa kuikumbuka na ikiwezekana
kuiandika kabisa ili Mungu atakapokutendea haukawii kuitimiza mara moja.
Ndio sababu hata sadaka ya madhiri ilikua huruhusiwi
kupeleka kilema, maaana yake ulikua huruhusiwi kupeleka iliyopungua.
Kama ukisema Mungu naomba unibariki milioni tatu na nusu
yake nitakupa wewe, baada Mungu kukupa badala ya kupeleka milioni moja na laki
tano ukapeleka milioni moja na laki nne unakua umempelekea Mungu kilema.
Wakati tunaanza kanisa kuna mahali tulitakiwa kununua
kiwanja kwa shilingi milioni thelathini lakini wakati huo nilikua sina hela na
ndio kanisa lilikua linaanza , kwasababu nilimuwekea Mungu nadhri kabla
sijaanza kutafuta kiwanja Mungu alikua mwaminifu na tukafanikiwa kununua kile
kiwanja.
Unapoweka nadhiri Mungu hakawii kuitimiza ili auone moyo
wako ni wa namna gani.
Siku moja nilimuwekea Bwana nadhiri kwamba nikipata gari
nitampa mtumishi wako, siku moja akaja mzee mmoja kanisani kutoka Mbeya alikua
ameokoka na wakati naongea nae nikaikumbuka nadhiri niliyomuwekea Mungu,
nikaingiza mkono mfukoni nikampa funguo ya Marcedez Benz niliyokua nayo, yule
mzee hakuamini, nikamtafutia na dereva hapo hapo akamsaidia kuendesha kurudi
Mbeya.
Yeye alikua hajui kwanini nimempa lakini kulikua na nadhiri
ambayo nilikua nimemuwekea Bwana kwamba lazima niitimize.
Baada ya siku chache rafiki yangu mmoja akanipa Land cruiser
VX, nikashanga sana na baada ya kunipa hiyo land cruiser na mimi nikaitoa kwa
mtu mwingine na nikawa napanda daladala, lakini ni kwasababu ya nadhiri
niliyomuwekea Mungu.
Mtu mwingine anaweza kufikiri nikiwanavyo kumi hapo ndio
ninaweza kumtolea Mungu ili nibaki navyo nane, lakini Mungu anapenda kuuona
moyo.
Watu wengine wanafikiri kuinuliwa na Mungu mpaka ufunge tu
na kuomba peke yake, lakini kuna Zaidi ya hapo, kuna nadhiri na uaminifu mwingi kwenye maisha ya watu wa Mungu mpaka
uwe wa tofauti.
Watu wengine wamewahi kufunga na kuomba sana ili na wao
warudishe misukule kama sisi lakini hawajafanikiwa ni kwasababu ya maisha yao
ya ubinafsi na kutokuwa waaminifu mbele za Mungu.
Ni bora kutokuweka nadhiri kabisa kuliko kuweka halafu
usiiondoe.
NAMNA NADHIRI LIVYO YA THAMANI MBELE ZA MUNGU
Mfano wa Yefta
Wafalme 11:30
Yefta aliweka nadhiri kwa Bwana kuwa kama Mungu akiwatia
adui zake mikononi mwake wakati anarudi nyumbani chochote kitakachokuja
kumpokea cha kwanza atamtolea Bwana kama sadaka ya kutekektezwa.
Alipoenda vitani Mungu akampa ushindi mkuu, aliporudi
nyumbani binti yake wa pekee akaja kumpokea wa kwanza. Ikambidi amtoe binti
yake kama sadaka ya kuteketezwa mbele za Bwana
Ingekua leo mtu angetafuta namna ya kutoroka, lakini hapa
huyu binti wa ajabu akamuambia baba yke umtimizie Bwana nadhiri yako.
Mfano wa Hanna
Samweli 1:1
Hanna alikua hazai na alikua akichekwa na Penina mke mdogo
wa mumewe, Hanna ameolewa kama mke mkubwa lakini alichelewa kupata motto ila
mke mdogo alipoolewa akazaa bila matatizo nae akaanza kumdhihaki Hanna mke
mkubwa.
Hanna alipoenda hekaluni kuomba akaweka nadhiri akasema
Bwana kama utanipa motto mmoja tu nitamtoa awe mali yako Bwana, nitamuweka
hekaluni akulie huko huko.
Siku moja nilifanya mkutano kule kampala kwenye kanisa moja
linaitwa Kasubi kawala, akaja mama mmoja akiwa na shida kubwa na Mungu
akamfungua katika shida yake, baadae nikamuuliza mama Mungu amekutendea haya
utampa nini? Yule mama akasema mchungaji mimi ni masikini sina cha kumpa
Mungulakini namtoa mwanangu awe mali ya Bwana nikamchukua motto nikamuweza
kwenye kapu kubwa( nilitaka nione kama anamaanisha au anatania) nikasema
mpelekeni ofisini tutamtafutia mahali pa kuishi na kula awe wa kanisani.
Baaada ya mkutano yule mama akabaki mahali pale hakuondoka
kwenda nyumbani nikajifanya kama simuoni akawa anapita huku anaongea mwenyewe,
baadae akasema namuomba mwanangu nikamlishe, tukamwambia ulishamtoa awe mali ya
kanisa tutamlisha sisi yule mama akaanza akulia sana akasema nilimaanisha
atamtumikia Mungu akiwa mtu mzima sio sasa hivi, ikabidi tumrudishie motto wake
na kumsaidia.
Watu wengi wanasema tunampa Mungu maisha lakini wanakua
hawamaanishii.
Unaposhindwa kuitimiza nadhiri inakuletea matatizo makubwa
Kumbukumbu la torati 12:11
Unapotaka kuweka kuitimiza nadhiri ni vzuri kuipeleka mahali
pale ambapo bwana ameweka jin alake
Kumbukumbu 23:21
Mtu asiyetimiza
nadhiri ni mpumbavu
Muhubiri 5:4
Unaposhindwa kuitimiza ahadi ya Mungu, Mungu anaanza
kuiharibu kazi ya mikono yako.
Siku moja tulikua na mkutano Marekani na baada ya mkutano
tulikua hatujui tatafikia wapi, lakini mimi nilikua nimemuwekea Mungu nadhiri.
Wakati tunatoka nikakutana na mchungaji ambae nilikutana nae
Dar es salaama miaka mingi sana na nilimuozesha binti mmoja ambae nilikaanae
nyumbani kwangu, hapo hapo mchungaji
akaniomba nikakae nae kwake na nikamuone binti yule ambae nilimuozesha kwake,
tukawa temekwepa gharama za kuishi hotelini na Mungu akaonekana kwetu kwa namna
ya ajabu.
Usiweke nadhiri na kushindwa kuiondoa ni bora usiweke.
Mtu mmoja alikua akaniambia anamuomba Mungu apate milioni
sita na akasema akipata milioni mbili ataitoa kanisani, nikaomba nae na baada
ya siku mbili Mugnu akambariki yule mtu milioni sita,,yule mama akanipigia simu
akasema mchungaji nimepata ile hela sasa ile milioni mbili nikupe, nikamwambia
hapana uilete kanisani siku ya ibada. Siku hiyo ya ibada nikamwambia mchungaji
mmoja leo kuna mtu atatoa milioni mbili akiitoa nenda ukanunue viti, baadae
mchungaji akaniambia baba ile hela uliyoniambia haipo. Bbada ya siku chache
yule mama akapiga simu akasema alipata matatizo kwenye duka lake akaitumia ile
milioni mbili kutengeneza duka lake na ataileta akishapata faida.
Baada ya siku chache yule mama akaachana na mumewake,
akapoteza kila alichokuanacho na akaacha mpaka wokovu, hii ni kwasababu ya
laana ya kutotimiza nadhiri
Paulo aliweka nadhiri
akaitimiza
Matendo 18;18
MAMBO YANAYOSABABISHA NADHIRI YA MTU ISITIMIE
Ø
Wakati unapomuwekea Mungu nadhiri unatakiwa
kuendelea kuwa mwaminifu
u mbele za Mungu, unakuta mtu ameweka nadhiri lakini
anaanza maisha ya dhambi, anaendelea na uzinzi na uongo na kutokua mwaminifu,
unapifanya hivyo unafunga milango ya Mungu kuitimiza nadhiri hiiyo
Ø
Wakati mwingine Mungu anakua haruhusu jambo
litokee kwasababu anakua anataka ukue, mrithi inahesabika kuwa kwama mtumwa
ijapokua ni bwana wa yote akiwa bado motto, kuna watu wengine Mungu anajua
akiwabariki leo wanamuacha, kwahiyo Mungu anakawia kuitimiza ili amtengeneze
mtu vizuri ili awe chombo chema mbele za Bwana. Hivyo ndivyo Mungu anavyotenda
kazi
Unapokubali kuwa chombo cha Mungu na kuyatenda mapenzi ya
Mungu ziko Baraka zinazifuatana na wewe, ni kama ukiweka maziwa ya mtindi
kwenye glasi baada ya kunywa yapo maziwa ambayo lazima yabaki kwenye ukuta wa
glasi ndivyo ilivyo kwa mtu anayemtumikia Mungu unapofanyika Baraka kwenye
maishaya watu wengine na kuwa mwaminifu kwenye mambo ya Mungu ziko Baraka
ambazo ni lazima zifuatane na wewe.
“KATIKA JINA LA YESU
BWANA UNISAIDIE KUTOKUWEKA NADHIRI, LAKINI NIKIWEKA NADHIRI NIITIMIZE”
Kwa masomo mengine kwa mfumo wa audio, vitabu na DVD
wasiliana nasi kwa namba
0716671440
0714729805
0718104333
0717727206
Kwa masomo mengine kwa mfumo wa audio, vitabu na DVD
wasiliana nasi kwa namba
0716671440
0714729805
0718104333
0717727206
0 Comments