Mchungaji Kiongozi:
Josephat Gwajima 23.9.2012
UTANGULIZI:
Huu ni mwendelezo wa somo la Nyota na Maisha mtu aliyonayo. Mathayo
2:1; Kama tulivyoona tangu mwanzo kuwa nyota ni kipawa, uweza, hatma au hali ya
mtu ya baadaye. Tukaona nyota ya Yesu ilionekana kabla Yesu hajazaliwa na
mamajusi wa mashariki walimwona kama Mfalme.
MAANA YA NYOTA:
Kama tulivyooa sehemu ya kwanza kuwa nyota ni kiashiria cha
rohoni, kinachoonesha mtu atakuwa nani baadaye, mafanikio ya mtu au hatma ya
mtu. Viashiria hivi ndivyo vinavyoitwa nyota.
NYOTA KATIKA BIBLIA:
Hesabu 24:14-17 Baraki alikuwa mfalme, na alipoona kuwa
wanaisrael wanakuja ili kushambulia ufalme wake, akamtafuta Balaam amtabirie.
Hayo ni maneno ya Balaamu aliyoona, Hivyo Balaamu alipoangalia taifa la Israel akaona
nyota, kimsingi nyota ya mtu inaonyesha jinsi mtu atakavyokuwa baadaye. Hivyo
balaamu aliweza kumuona Yesu tangu mwanzo na ndio maana mamajusi wa mashariki
nao pia walimwona Yesu kama nyota.
Nyota yaweza kuonyesha kusudi la maisha ya mtu, na ndio maana
ingawa Suleimani alizaliwa na mke wa Huria ambaye Daudi alimuua mumewe ili
ampate lakini kwasababu nyota ya kujenga hekalu ilikuwa juu yake (yaani
Suleimani), Mungu alimchagua kujenga Hekalu. Daudi alikuwa na watoto wengine
wengi, lakini aliyechaguliwa kujenga ni Suleimani kwasababu ndio mwenye nyota
ya kujenga yaani tangu anazaliwa
Isaya 47:8-12; Hapa biblia inataja neno “wajuao Falaki”, hii
ni elimu inayohusu mambo ya nyota ambayo wachawi husoma. Katika Mathayo 2:1-
Biblia inataja mamajusi, wao ni wasomaji wa nyota ambao waliiona nyota ya Yesu
kabla ya Yesu hajazaliwa. Nyota ya Yesu iliwafanya mamajusi kumfuata kutoka
mbali, na wakati huohuo Herode alifadhaika. Kumbe nyota ya mtu ikionekana watu
wanaweza kuifuata na kukuletea unalohitaji. Watu wengi wapo katika vifungo
mbalimbali kwasababu nyota zao zimefunikwa.
MAMBO 15 AMBAYO
UTAYAONA KAMA NYOTA YA MTU HAIPO:
·
Umahiri
na utendaji kazi wa mtu hauonekani; kama mtu hana nyota ule umahiri wa wake na
utendaji kazi hauwezi kuonekana. Hata ajitahidi kufanya kazi kwa bidii umahiri
hawezi kuonekana.
·
Hawezi
kuwa mbunifu katika maisha; nyota huleta ubunifu sasa kama haipo basi ubunifu
wa mtu hautaonekana. Mtu huyo atakuwa anashindwa kubuni kitu cha kufanya ili
kupata mafanikipo katika maisha.
·
Hawezi
kufanya kazi zake kwa ufanisi; nyota huleta ufanisi katika kazi, mtu akikosa
nyota basi ule ufanisi wake hauwezi kuonekana, mtu huyo atakosa ufanisi katika
kazi zake.
·
Hukosa
mvuto; nyota huleta mvuto hivyo mtu nyota yake haipo, anakuwa anakosa mvuto
hata wa watu kuomuona tena.
·
Hukosa
kibali; nyota humfanya mtu awe na kibali hivyo mtu anapochukua nyota, kimsingi
anakuwa amechukua kibali chako.
·
Huwezi
kusikilizwa katika jamii; kwasababu nyota huleta kusikilizwa, mtu akichukuliwa
nyota hawezi kusikilizwa katika jamii.
·
Hawezi
kuthubutu;
·
Anakosa
uthubutu wa kutenda;
·
Anakosa
ujasiri wa kusema; mtu akikosa nyota anakosa ujasiri wa kusema.
·
Anakosa
uthubutu wa kutoa maamuzi magumu; mafanikio ya mtu ni matokeo ya maamuzi magumu
aliyowahi kuyafanya.
·
Anakosa
ujasiri wa kudai unachojua ni kweli;
·
Huwezi
kutumia hata kile ulichonacho; ndio maana ya lile andiko utajenga nyumba na mtu
mwingine atalala ndani yake”.
·
Anakuwa
na matatizo;
·
Anakuwa
na hofu ya kutenda mapenzi ya Mungu; nyota ikichukuliwa mtu aweza kuwa na hofu
ya yajayo, yaliyopo au yaliyopita.
·
Kukosa
uaminifu kwenye mambo ya Mungu.
Kwahiyo wachawi au waganga wanapochukua nyota yako kimsingi,
mambo hayo yanakuwa hayapo kwenye maisha yako.
JINSI WACHAWI WANAVYOCHUKUA
NYOTA NA MATUMIZI YAKE:
Utajiuliza ni wakina nani wenye uwezo wa kuiona nyota; biblia
inathibitisha kuwa waganga na wachawi wana uwezo wa kuiona nyota na kuifuata.
Na kama nyota haina ulinzi wa Mungu waganga wanaweza kuichukua nyota. Kuna watu
wanadhania kuwa uchawi haupo na kutokujali uwepo wake, lakini uchawi upo
kwasababu biblia imetaja kuwa uchawi upo.
Wanachuaje; kwasababu wachawi wanaweza kuiona nyota ya mtu na
kuifuata, hivyo wakigundua kuwa nyota ni nzuri wanaweza kuichukua na kumuuzia
mtu mwingine; na ndio maana mtu anaweza kuzaliwa nyota ya uongozi, ujasiri,
upendeleo, ubunifu au kupata kibali mbele za watu, alafu ikachukuliwa na kupewa
mtu mwingine. Na ndio maana kuna watu ni matajiri kwasababu ya nyota za watu;
na wakati huohuo mtu Yule ambaye nyota yake oimechukuliwa anaanza kuwa na
matatizo; kile kibali au upendeleo aliokuwa nao awali hawezi kuwa nao tena.
Mtu aliyechukuliwa nyota; anakuwa na mafanikio mwanzoni
lakini ghafla yanabadilika baada ya kuchukuliwa nyota. Kimsingi; Mungu akikupa
kutu huwa kinadumu lakini kama maisha ya mtu yanaashiriwa na nyota pale nyota
inapochukuliwa mtu huyo upendeleo wake unaanza kuondoka. Rudisha nyota yako kwa
Jina la Yesu.
Maombi ya kuamuru
aliyechukua Nyota yako arudishe:
Baba katika Jina la Yesu leo nimetambua kuwa nina nyota, nayo
yaweza kuchuliwa na kunitia katika matatizo; hivyo ninaamuru ila aliyechukua
nyota yangu arudishe katika Jina la Yesu. NInapokonya nyota yangu
iliyochukuliwa katika Jina la Yesu, naamuru mahali popote ilipowekwa na
kutumika ninaamuru irudi kuanzia sasa katika Jina la Yesu.
Ninaamuru umahiri wangu, ufanisi, uwezo wangu wa kutenda na
uwezo wa kuthubutu ninaurudisha katika Jina la Yesu. Ninaamuru kibali, afya,
ujasiri na mvuto wangu urudi katika Jina la Yesu; nataka nyota yangu katika
Jina la Yesu.
UFUFUO NA UZIMA {THE GLORY OF CHRIST (T) CHURCH}
TANGANYIKA PACKERS,
KAWE, DAR ES SALAAM.
1 Comments
Mungu awabariki sana
ReplyDelete