UFUFUO NA UZIMA UBUNGO CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 16 APRILI 2023
ASKOFU JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: KUSUDI LA KUCHAGUA LITASIMAMA
Swali; Kwanini mimi nipo hapa?
kwanini mimi ni mtu na sio mnyama? Kwanini mimi niko kama nilivyo?
Jibu;
Ni kwa sababu
Mungu amekuchagua kutimiza
kusudi fulani hivyo ulivyo ili siku moja utoe hesabu ya kusudi lako hapa duniani.
“Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana
alikuwa tasa. Naye BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba. Watoto
wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini?
Akaenda kumwuliza BWANA. BWANA akamwambia,Mataifa mawili yako tumboni mwako,Na
kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako.Kabila moja litakuwa
hodari kuliko la pili,Na mkubwa atamtumikia mdogo.Siku zake za kuzaa
zilipotimia, tazama! Mapacha walikuwamo tumboni mwake.Wa kwanza akatoka, naye
alikuwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita jina lake Esau. Baadaye
ndugu yake akatoka, na mkono wake unamshika Esau kisigino. Akaitwa jina lake
Yakobo. Isaka alikuwa mwenye miaka sitini mkewe alipowazaa.” Mwanzo 25:21-26
“(kwa maana kabla
hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame
kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia
yake aitaye), aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo. Kama ilivyoandikwa,
Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia. Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa
Mungu? Hasha! Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia
yeye nimhurumiaye. Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala
wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu. Kwa maana maandiko
yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe
nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote. Basi, kama ni
hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu.”
Warumi 9:11-18.
Mungu anampatia mtu kusudi
sio kwa sababu kuna jambo zuri amelifanya ila ni kwa mapenzi yake yeye achaguaye.
Mafanikio hayapo katika yeye apigaye mbio, ila ni kwa uwezo wake Mungu
mwenyewe. Uwezo wako wa kuamua umesukwa na Mungu, ndiye anayekuongoza katika
kufanya maamuzi. Esau na Yakobo hawakutenda baya wala jema ila ili kusudi la Mungu
la kuchugua lisimame alimchagua Yakobo.
Duniani watu wanatabia ya
kuhukumu mtu anayepitia shida au mabaya kuwa ni muovu. Kusudi la Mungu la
kuchagua halijalishi umetenda ubaya au uzuri, japo kufanya matendo mema ni muhimu
na mabaya sio yakufanya. Unakwenda mahali na utafika salama, ili kusudi la
Mungu la kuchagua lisimame. Mpango na nia ya Mungu haiwezi kueleweka na
mwanadamu.
Sasa kuna watu wanakupiga
vita maana wanaona ulichonacho hukustahili bila kufahamu ni kusudi la Mungu
kukuchagua sio kwa uweza wako bali ni kwa sababu kusudi la Mungu la kuchagua
lisimame.
Hakuna sababu ya kusema
jambo hili siliwezi au sina uwezo wa kutimiza jambo hili, yeye aliyekuchagua
atakupata uwezo wa kulitimiza. Kabla kusudi lako halijatimia hakuna kitu wala
mtu anayeweza kukuondoa duniani. Unapotoka mbinguni kuna kusudi umepewa na
Mungu, na lazima hilo kusudi litimie kabla hujarudi.
Unaweza kumuona mtu
anatabia mbaya ukamkataa kumbe ndio Mungu aliyemchagua na kumuita. Rahabu alikuja
duniani kwa kusudi la kuficha wapelelezi wa Israeli ndani ya Yeriko na kupitia
Salmoni aingie kwenye ukoo wa Mfalme Daudi mpaka Yesu, japo alikuwa kahaba.
“Yoshua, mwana wa Nuni,
akawatuma watu wawili kutoka Shitimu kwa siri, ili kupeleleza, akawaambia,
Enendeni mkaitazame nchi hii, na Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani kwa kahaba
mmoja jina lake aliitwa Rahabu, wakalala huko. Mfalme wa Yeriko akaambiwa, kusema,
Tazama, watu wawili wa wana wa Israeli wameingia humu leo usiku, ili
kuipeleleza nchi. Mfalme wa Yeriko akatuma watu kwa Rahabu, akasema, Watoe watu
wale waliokuja kwako, walioingia ndani ya nyumba yako, maana wamekuja ili
kuipeleleza nchi. Yule mwanamke akawatwaa wale watu wawili, akawaficha,
akasema, Naam, wale watu walikuja kwangu, lakini sikujua walikotoka; ikawa kama
wakati wa kufungwa lango la mji, kulipokuwa giza, watu wale wakatoka, wala
sijui walikokwenda; wafuateni upesi, maana mtawapata. Lakini yeye alikuwa
amewapandisha darini, akawaficha kwa mabua ya kitani, aliyokuwa ameyatandika
juu ya dari.” Yoshua 2:1-6
Yesu aliwekwa kwa ajili ya
kuinuka kwa wengi na kuanguka kwa wengi. Safari yako inaanza ikiwa imemalizika,
ndio maana Mungu anaitwa Mungu wa miisho kabla ya mianzo. Maisha yako yalishaamuliwa
kabla hujazaliwa.
“kumbukeni mambo ya zamani
za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana
aliye kama mimi; nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo
yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi
yangu yote.” Isaya 46:9-10.
Mambo yote hayapo kwenye
uwezo wake atakaye, umesoma, hujasoma, hapo ulipo kuna jambo umechaguliwa, wale
wanaozuia wanakuwaisha. Umepewa uwezo wa kugonga kila anayekuzuia na asikuzuie.
Kesho yako imeshaamuliwa na Mungu.
Ukikosea na kutenda uovu,
amka omba msamaha endelea, safari yake iko pale pale.
“Avikomesha vita hata
mwisho wa dunia; Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari. Acheni, mjue ya
kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi. BWANA wa
majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.” Zaburi 46:9-11.
0 Comments