UFUFUO
NA UZIMA UBUNGO CATHEDRAL.
IBADA
YA JUMAPILI 30TH APRIL,2023.
ASKOFU
BARAKA THOMAS TEGGE.
SOMO:
WAMEIONA NYOTA YAKO.
“Yesu
alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama,
mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, Yuko wapi yeye aliyezaliwa
mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja
kumsujudia. Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia
pamoja naye”. Mathayo2: 1-3
“Kisha
Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu
ilipoonekana ile nyota. Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkaulize
sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende
nimsujudie. Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile
nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali
alipokuwapo mtoto. Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno.
Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka
wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na
uvumba na manemane”. Mathayo 7-11
“Maana
kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme
utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye
nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani”. Isaya 9:6
Biblia ni kitabu
cha kiroho na ukiweza kuamini tu biblia ile mwanzo 1:1 basi mambo mengine yote
baada yahapo unaweza kuamini. “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi”.
Mwanzo 1:1 ina maana kuna Mungu
ukiona mbingu na nchi kuna aliyeziumba unaanza kuona kuna aliyeziumba yeye
asiyeonekana ndiye anaitwa hapo mwanzo aliyeziumba mbingu na nchi, na ilikuwa
ukiwa tupu na giza ndipo Roho wa Mungu akatulia juu ya maji, Mungu akasema iwe
nuru ikawa nuru, kuanzia hapo Mungu
anasema vitu na vikawa vinatokea,biblia sio kitabu cha mantiki au logic ,ni
kitabu ambacho haonekani anasema na vinatokea , ni kitabu ambacho nyoka
anaongea na mtu, Mungu asiyeonekana anasema wanyama watokee na wanatokea, ardhi
ilikuwepo imefunikwa na maji Mungu anasema pakavu paonekane na pakavu pakaoneka
a, Mungu akasema iwe na angaa maji yagawanyike
,angaa likagawa maji sio kwa mujibu wa sayansi bali kwa neno la Bwana , kwahiyo
dunia hii kuna maji ya juu na ya chini, maji yaliyo chini yakusanyike pamoja
,na akaongea na pakavu paonekane sehemu moja, na maji yale yatoe ssmaki na
yakatoa. Utakuwa na maisha yaliyojaa msongo wa mawazo, uwe kanisani au usiwe
kanisani kama huamini biblia utakuwa na msongo wa mawazo, kama huamini biblia
utajaa msongo wa mawazo kuna mambo yatakupata utachanganua kwa degree yako na
usipate majibu ila kwenye neno la Mungu kuna majibu.
Watu wengi wenye
akili nyngi ila hana Mungu ana changanyikiwa, dunia imejaa watu waliochaganyikiwa
hata wakivaa suti wana msongo wa mawazo, ana degree ila ana msongo wa mawazo,
kuna mtu mmoja hana degree wala cheo ila anamuamini Mungu. Mtu mwenye Mungu
hatakama hana akili nyingi hana msongo wa mawazo, wewe unawaza vitu vingi kama mabadiliko
ya tabia ya nchi, elimu imekufundisha na haina majibu, kadri unavyotafuta elimu
dunia ndio unazidi kuchanganyikiwa, nakushauri baki hapo hapo. Anasem mfalme Sulemani
wenye hekima nyingi kuna huzuni sana kuna mtu hafahamu kule Ukraine kuna vita
,vita pekee anayoifahamu ni ya rohoni,wana amani kama nini waipendao sheria ya Bwana
hakuna kitu cha kuwakwaza, ameolewa au hajaolewa ila ana amani kama nini, amekula
haja, hakuna kitu cha kumkwaza.
Kila ukiwaza
hupati jibu msongo wa mawazo unakuja ila pesa unayo na elimu unayo, unapokuwa
na vitu na havina msaada hapo ndipo msongo wa mawazo, pressa, kisukari vinaanza
, hasa kugundua havina uwezo kukuletea
furaha , furaha ya kweli ipo kwa njooni ninyi nyote msumbukao na nakuelemewa na
mizigo na mimi nitawapumzisha, jitieni
nira jifunzeni kwangu nanyi mtapata raha nafsini kwenu.
Kama kweli
amesema njooni kwangu, kuna raha basi watu wa dunia wanadhania tunajifanya wala
hatujifanyi, walihisi ulivyoachika nitakonda, nitakuwa wakulia, hapana kwake
kuna furaha. Mumgu anamwambia Musa uso wangu utaenda na wewe nami nitakupa
raha.
Wanao ongoza
kujiua sio maskini, kuacha wake sio maskini ni matajiri ulidhania alipolewa na tajiri
atakuwa na furaha maana kuna pesa ila ameachika. Billionea ndio wanaongoza
kwakuacha mke, pesa zake hazia uwezo kukupa furaha, furaha ya kweli inapatikana
kwa Mungu wana amani kama nini wapendao sheria ya Mungu. Maisha kwa asili ni ya
rohoni ukIjaribu kuleta mantiki utachanganyikiwa ila kama unaamini mwanzo 1
utaamini hayo mengine.
Yesu alipozaliwa
mamajusi wa mashariki waliona nyota wakasafiri. Mpaka wamesafiri ina maana wana
uhakiki hawaja pigiwa simu wala kusoma vitabu ila kuna kitu cha rohoni waliona
wakiwa mbali, biblia ni kitabu cha rohoni na wewe ni wa rohoni, Maisha ukiyakabili
kimwili utaumia.
Mamajusi
walipelewa kwa mfalme Herodi, zamani mfalme anazaliwa na mfalme na kuwa mfalme
lazima atokee kwenye familia ya kifalme. Ni mtoto mmojawapo wa mfalme baada
atakuwa mfalme hakuna uchaguzi. Mamajusi waliona nyota taifa la Israel kuna
mfalme amezaliwa, wakachukua uvumba na manemane kwenda kumuona, wakasafiri
wamebebea dhahabu pia kumpelekea yule mwenye nyota ya mfalme, wakafika Israel
nyota ikapotea. Kuna jambo limetokea kwenye ulimwengu wa roho nyota ikapotea, wakaanza
kuuliza watu hii nchi mfalme anakaa wapi maana bila shaka kwenye familia yake
mtoto amezaliwa, Lakin Herodi akasema hakuna mtoto kwake aliyezaliwa, mamajusi
wakamwambia kuna mtoto amezaliwa mfalme wa wayahudi, Herodi akawauliza viongozi
wa wayahudi kuwa anazaliwa wapi mfalme? Wakamjibu Herodi kuwa mfalme atazaliwa
Bethlehemu, kwa mujibu wa vitabu. Walipotoka pale ile nyota ikaonekana, nyota
yamtoto ikiwaongoza watu wazima mpaka kwenye nyumba aliyekuwepo mtoto,
Bethlehemu bila kuuliza walipomuona mtoto wakasujudu wakatoa uvumba na manemane
mbele ya mtoto.
Haya mambo kwenye
sayansi hayapo na haitumika hapa hatutumii elimu. Kanisani unakuja kumsikia Mungu
aliye roho, Isaya inasema kwa ajili yetu mtoto mwanaume amezaliwa na uweza
wakifalme utakuwa begani mwake, Isaya alimuona kabla na akamtaja kabla
hajazaliwa miaka 600 alitoa unabii atazaliwa na manamke aliye bikira na akaona
juu yake kuna nyota yakifalme inaitwa uweza wa kifalme. Kila mtu aliyezaliwa
juu ya uso wanchi ni roho , kila mtu ametoka kwa Mungu, na kila mtu amepewa
zawadi alipokuwa anakuja alipewa zawadi au kamara,kila mtu ana asili ya kiuungu
ndani yake kila mtu sio aliyeokoka tu bali kila mtu ana Uweza wa kiungu wa
kufanya mambo fulani maana Mungu anaweza mambo yote ameweka uwezo kidogo kidogo
kwa kila mtu, kila mtu ana uwezo wa
kiungu ndani yake na kwenye eneo hilo unafanya kama Mungu yaani unafanya mambo
ambayo Mungu angekuwa mtu angefanya hivyo hivyo.
Ukiwaleta watu
wengi kwa karibu utagundua wana uwezo wakiungu, ndani ya mtu kuna uwezesho wa
mtu kufanya mambo ya kiungu hiyo ndio inaitwa zawadi, unaweza kufanya mambo tofauti.
Umezaliwa nayo nahii ndio inaitwa nyota ndio sababu ya mtu kufanikiwa, nyota inapooneka
kuna watu wanawezo wakuja kwa nia mbaya ua nzuri. Uweza wakiungu kifalme upo
begani mwake wachawi wa mashariki wakale wakaona ni nyota ya kifamle.
“Kipawa
ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho;
Kila kigeukapo hufanikiwa”. Mithali 17:8
Kito cha thamani
ni kama zilivyo almasi au dhahabu, Karama ni kito cha thamani. Kuna dhahabu,
almasi na rubi hivyi ni vito vya thamani, kipawa ni kito cha thamani kwake yeye
aliye nacho kila kigeukapo yeye hufanikiwa. Inaonyesha mafanikio haya ni kwa
kipawa sio elimu na watu wanaofanikiwa ni watu wenye kipawa sio elimu, kipawa
cha kuongea au kuingiza sauti ya mtu,kuna mtu akikusikia ndani ya dakika chache anaongea
kama wewe, hata uende shule huwezi fanya kama yeye, Ronaldo ana kipawa cha
kucheza mpira ndio maana anafahamika sana hata wewe unacho kipawa kikafahamika
na wewe utafaamika sana tu.
“Zawadi
ya mtu humpatia nafasi; Humleta mbele ya watu wakuu”. Mithali 18:16
Lugha nyingine ya
kipawa ni zawadi, unaweza ukawa hujasoma shule ila uko karibu na watu wakuu ili
ufanikiwe lazima watu wakuu wakufahamu ndio ufanikiwe. Nyota yako inakupatia
nafasi sio elimu itakupatia nafasi na kipawa unacho kikionekana nafasi yako itaonekana tu
hata kama ni kampuni hakuna nafasi yako itabidi watengeneze nafasi kwa ajili
yako. Kijana mdogo anachunga kondoo kule Bethlehemu hana maana hata kwa ndugu zake wa babaye, akiwa
kule anatumia kipawa chake ila hawamlipi fedha, endelea kutumia kipawa chako,
kijana anapiga kinanda pale Bethlehemu ila hafahamiki na wakuu.
“Basi
Sauli akawaambia, Vema, nitafutieni mtu aliye stadi wa kupiga kinubi,
mkaniletee. Ndipo akajibu mmoja wa watumishi wake akasema, Tazama, nimemwona
mwana mmoja wa Yese, Mbethlehemi, aliye stadi wa kupiga kinubi, tena ni mtu
shujaa, hodari wa vita, anenaye kwa busara, mtu mzuri, ambaye BWANA yu pamoja
naye. Basi Sauli akampelekea Yese wajumbe, akasema, Nipelekee Daudi mwanao,
aliye pamoja na kondoo. Yese akatwaa punda, wa kuchukua mikate, na kiriba cha
divai, na mwana-mbuzi, akampelekea Sauli kwa mkono wa Daudi mwanawe. Basi Daudi
akamwendea Sauli, akasimama mbele yake, naye akampenda sana; naye akapata kuwa
mtu wa kumchukulia silaha zake. Kisha Sauli akapeleka watu kwa Yese, akasema,
Tafadhali, mwache Daudi asimame mbele yangu; maana ameona kibali machoni pangu.
Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi
akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile
roho mbaya ikamwacha”. 1Samweli 16:17-23
Huyu ni mfalme wa
nchi anasema atafutiwe mtu anaye juu kupiga kinanda. Mtu mmoja anakaa na wakuu
na kuna mahitaji ya mkuu yamesema nayeye ana mfahamu mtu ambaye si mkuu. Hapa
unaona kipawa cha mtu na tabia ya mtu huyu, mpaka mtu anaweka dhamana maisha
yake ili huyu mtu akiharibu, mpaka mtu akutaje kwa wakuu tabia zako ni muhimu ili
zisiharibu mambo, asema mtu huyu ana Mungu na ananena kwa busara,.
Kijana mdogo
anakaa na kondoo hajasoma shule ila ana nyota, mfalme ameongea na watu wake wa
karibu wamtafutue mtu, kuna baadhi ya mambo hutayatafuta kwa sababu nyota yako
imeonekana, nyota yako ikaonekane wakutafuta. Hii ili mfanya Daudi kwa mara ya
kwanza kwenda ikulu kwa mfalme, ni kipi kina mpeleka ikulu? Ila ni nyota yake.
Kuna watu wanaona yeye na mungu inatosha hapana haitoshi, kuna watu wana ukaribu
na watu wakuu. Kuna watu wa kawaida wana
fahamia na watu wasio wa kawaida na hao watu wa kawaida wanahitaji kukusema kwa
wakuu. Chunga tabia zako zinaweza kukwamisha nyota yako kufanikiwa.
Kuna watu
wanaamini kuwa wanachukiwa hata kwenye familia anaamini baba ama mama yake
hawampendi ,husema tangu nizaliwe sijawahi kupumzika kazi zote ni zake hata
akisemeshwa kidogo basi anachukiwa, sisi hatumpendi shetani kwani wewe ni
shetani? Kuna watu wanapenda amani anapokuona wewe ni mtu wa shari, unakaa kwa
mtu na anakusaidia ila unaishia kulalamika tu inabidi ushukuru sana kwa kuweza
kukupatia mahali pakukaa na hakuna bili yoyote unadaiwa unakuta una nyota na mtu ameona akusaidie ila kwa tabia yako
ina haribu nyota. Niliwahi kudhamiria
kumchukua kijana mmoja akae kwangu nimsomeshe maana nina uwezo wakumlipia
kidato cha kwanza hadi cha nne ila yeye tabia zake ni kaona ni za ugombanishi,
nikamwacha akae kanisani na malaika wa
kanisa la Ufufuo na Uzima.
Kipawa chenyewe
kina kutengenezea nafasi kwenye moyo wa mtu na itamtaka akusaidie. Tumeona
nyota yake na imetuvuta kwake, kuna mtu nyota yake inakuvutia kumchumbia,
wakati mwingine hakuna anayekupiga vita unajipiga vita mwenyewe. Unaweza kukaa
kwenye dhiki kwa muda fulani ila Mungu atakutoa kwa wakati wake. Naongelea nyota
na nafasi, zawadi ya mtu humfanyia nafasi mbele ya wakuu. Wakuu wanaongea na
wachache wa karibu yao wamletee mtu fulani. Watu wote wanao msaidia mkuu wa nchi
wanakaa alipokuwa mkuu wa nchi sio kwa sababu ya elimu ila waliona nyota yake.
Kuna siku nilimuona
mtu anayemnyoa raisi nywele nikaambiwa anakaa ikulu na sio kwamba kila siku
anamnyoa ila anakaa karibu tu kusubiria ziote nywele amnyoe, hii ni kwa sababu
ya kiusalama. Waione nyota yako, Sauli aliandika barua kwa Yese babaye Daudi, kuwa
Daudi abaki ikulu maana amepata kibali machoni pa Sauli, nyota yako ya biashara
ionekane.
Siku ya kwanza
baba alimuona Pastor Paul kule Maragalasi, Pator Paul ni mchungaji kwelikweli
maana amewahi kuchunga kondoo, mbuzi hata mbwa, baba alipomuona akaniambi kuna
kijana nimemuona. Siku moja nikaenda Kigoma nilipomuona Pastor Paul, ila
sikujua ndio baba alimzungumzia nikasema nitaongea nae muda wa chakula cha
mchana, nilipewa wali na migebuka, nikamuuliza una mipango gani ya maisha
akasema nataka kusoma sheria, nikamwambia mbona wewe ni mchungaji, maana alikuwa
SNP wa Maragalasi ila anachapa gombo kama wale wa cathedral Ubungo. Baba akasema
tupeleke mwangalizi Maragalasi. Kwa mara ya kwanza akapokea wito akaja Ubungo,
fanya kazi ya Mungu kwa bidii hata kama uko porini wataiona nyota yako. Baba
akasema aitwe mara moja na baba akikuita ujue kuna vitu vitakusindikiza.
Alikuja akafikia pale Hai moshi akawa muhubiri mjini, wilaya ya Kilimanjaro
karibu na Moshi, nyota ikaonekana. Fanya
kwa bidii hata kama ni fundi viatu au muimbaji hata ikulu wapo hawakai Msewe. Mtu
anapokupa kazi fanya kwa biddi watakutaja mahali hata kama huwafahamu wakuu,
mtu atakutaja kwa wakuu.
Siku moja
nikaongea na baba, yule kijana anapiga gombo mpaka moshi mjini alikuwa analala
kanisani, na wengine watu wa kanisani
wakamwambia hawa kutunzi, unalala kanisani kama wana thamini huduma yako
wakupangie nyumba, wewe una moto ila hawa kutunzi ungepangiwa chumba chenye AC
, nikamuonyesha baba clip yake , baba kasema huyu sio wa Moshi aje mzimuni,
wewe pia una nyota yako inaweza isiwe kuomba,kusalisha,ila una nyota, huhitaji
kujitangaza. Nyota yeyewe itakupatia nafsi, ni kito cha thamani ni zaidi ya
dhahabu. Kuna kitu unacho ni cha ki-Mungu hata kama hulipi kuna siku utatajwa
mahali.
Yusuph mwana wa
Yakobo alikuwa gerezani ana tafsiri ndoto na halipi, nyota ikifika mahali itajilipa yenyewe nachukia mtu
anayefanya mambo mpaka alipwe. Kuna mabo unayaona kawaida ila ni mabaya, unawaombea
watu na kuwaomba pesa ndio una nyota ya kuombea watu. Juzi niliambiwa ni peleke
watu watano nyumbani kwa mtu mkubwa wakae siku 5 wamuombee, je nikikupeleka
ukaanza kuomba pesa si utaniambisha, kuna watu ni wakuu hawahitaji uwaombe pesa
ila wao watakupatia kuliko uliyofikiri kuomba, usiwe na tabia yakuenda pesa na
kuweka pesa mbele kwa kila jambo.
Nimeshuhudia hapa
kanisani baba anaombwa apeleke watu mahali kuomba ila wanaenda kuharibu ni
kwasababu kuna mambo wameyaozea , utaeda kwa mtu mkubwa na baada ya maombi
unaomba elfu 50,kumbe yeye alitaka kukupa 3m anaona una njaa sana na kuhisi
unaweza muibia tv, kipawa cha mtu kina kupatia nafasi kwa watu kwa kutumia
kipawa alichokupatia kama zawadi, tabia sasa. Nyota ya Yesu ilipotea maana yake
kuna vitu ulitakiwa uletewe ila vikapotea, shetani hawezi kumuibia nyota
aliyeokoka ila anaifunika haiwezi kuonekana kwa wakuu wakaona, na kifuniko
kikubwa kwa nyota ni tabia, wanaogopa kukaa karibu na wewe kwa sababu ya tabia.
Na hizi tabia ambazo ni kifuniko cha nyota ni tabia zenye uvuvio wa shetani, siongelei
tabia za mwilini ila za rohoni, mtu ni muimbaji mzuri ila tabia sasa, kila mtu
mwenye mapepo akipagawa kuna tabia ataonyesha ambayo sio yake anaweza kuanza
kupiga kareti au kutukana, unakuta ni mdada tena ila unagundua sio yeye. Shetani
hahitaji udhihirishe tabia mbaya muda wote, ni mpaka ufike kwenye fursa ndio
ana jidhihirisha.
Unaweza muona binti,
ukatamani upeleke jina kwa Pastor Msimbe unataka kuoa binti, sasa jumapili
unamkuta amekaa mbele madhabahuni na sio mahali pake pakukaa, anaomba mara
anaambiwa na kiongozi asikae madhabahuni, anaanza kumfokea kiongozi, unaenda
kwa mzee Msimbe anakuambia yule mbona ni kichaa, umesema unataka mke au
umsaidie kumpeleka milembe.
Kila jambo la ki-Mungu
lina wakati wake, ikifika muda wake shetani anakupanda kichwani unakuta mtu
muda wake umefika, ukiwa kiongozi ina bidii uwa hurumie watu kuna mtu ni jeuri
na kiburi ni kwa sababu ana nyota na muda wake umefika, Stephano anasema ili pokaribia
wakati wa Mungu , ndipo Farao akazidi kuwatesa wana wa Israel, kuna wakati
unafikia ndio mashetani yanaibuka kifuniko kikubwa cha nyota ni tabia zenye
uvuvio wa shetani, nyota ni kitu cha rohoni na kuna tabia ni matokeo ya tabia
za rohoni, kama iIlivyo Roho Mtakatifu akiwa ndani ya mtu ana matunda au
matendo. Tunda la roho ni upendo, furaha, utu wema, amani, fadhili, uaminifu ni
tabia mambo sio asili ya mtu. Kuna mtu ni mkorofi ila akijaa Roho anakuwa mpole
,mkaribu nini hiki ni kwakuwa Roho ameingia ndani yake na kumpa tabia nzuri. Likewise
shetani anaweza kufanya kazi akiwa ndani ya mtu au nje anamvuvia maana yake
anampa hisia mawazo juu ya tabia fulani ukorofi, uasi na matusi.
Mtu ni mkorofi
mbishi, ila ukimkuta anaabudu na kusifu unaweza muona mke bora ila akiweka mic
chini ni mkorofi kama ibilisi. Ila sio yeye kuna tabia watu wanazo ila sio
tabia zao za asili ni wakati umefika shetani anamfunika na tabia ili asionekane,
mtu ana tabia ya mahusiano, biashara na inaonekana ila tabia japokuwa nyota ipo
hapa nyota haijaibia ila imefunikwa.
Yesu nyota ilipotea
na kama isingeonekana wangerudi kwao na uvumba, dhahabu na manemane, kuna mtu
wakati umefika uanze biashara, familia ila shetani anakuletea tabia hata kama unanena
ila hawakutaki tena. Binafsi mtu asiyeheshimu mamlaka simtaki hata aweje
itabidii nitumie neno. Mtu kumvunjia heshima mtu mzima hata kama amekukosea.
Paulo anamwambia Timotheo usiana na wazee kama baba zako ama mama zako
muheshimu mzee. Kuna mambo hutakiwi kumfanyia mtu aliyekuzidi umri hata kama una
mzidi vipawa ule utu uzima wake unahitaji kuheshimiwa sio ishu ya cheo chake.
Kuna nabii
nilimuona anachapa wazee Pastor Mwagela ukienda pale utachapwa viboko, hata
kama una mafunuo ndio mpaka wazee una wachapa.
Ni kama lile neno
nzuri Mungu alisema nimependa Yakobo nimemchukia Esau, kwasababu alidharua kitu
cha Kiungu, mamlaka ni kitu cha Kiungu Mungu aliweka badala yake, itabdi nisome
neno na kuomba Mungu anisaidie nikupende huheshimu watu wazima. Watu wengi
waovu, waasi, kudharau mamlaka sio wao ni shetani anawavuvia. Shetani anafanya kazi
na wewe, ile kudharau mamlaka ni kifuniko shetani anaweka ili nyota yako
isionekane.
Nakuahidi kuwa muda
niliopo hapana usipo heshimu mamlaka nitahakikisha haustawi nitakumwagia
chumvi, sipendi mtu astawi kama haheshimu mamlaka maana atanisumbua ni heri afe
na ina ruhushiwa ili wengine wapone. Nyota imeonekana ila tabia nyingine za
watu ni zile zenye uvuvio wa kishetani. Shetani anaona na anakutumia wachawi
wanaingia ndani yako au anakuvuvia unaanza jiona wewe ni maalumu sana au wakipeeke wa aina yako ni wewe
tu. Kanisa lazima liheshimiwe kuwa na adabu wazee waheshimiwe. Kama huwezi hama
kanisa.
“Wakafika ng’ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi. Na alipokwisha
kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo
mchafu; makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza
kumfunga tena, hata kwa minyororo; kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa
pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala
hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. Na sikuzote, usiku na mchana,
alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikata-kata kwa mawe. Na
alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia; akapiga kelele kwa sauti
kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa
Mungu usinitese. Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina
langu ni Legioni,
kwa kuwa tu wengi. Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile.
Na hapo milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, wakilisha.
Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao.
Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo
kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili;
wakafa baharini. Wachungaji wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na
mashambani. Watu wakatoka walione lililotokea.
Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili
zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa. Na wale waliokuwa wameona
waliwaeleza ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na habari za nguruwe.
Wakaanza kumsihi aondoke mipakani mwao. Naye alipokuwa akipanda chomboni, yule
aliyekuwa na pepo akamsihi kwamba awe pamoja naye; lakini hakumruhusu, bali
alimwambia, Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawahubiri ni mambo
gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu. Akaenda zake, akaanza
kuhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote
wakastaajabu”. Marko 5:1-20
Huyu ni mwenye
pepo ni muhubiri na Yesu hawezi kumwambia mtu akahubiri kama hana kipawa, sasa
ameingiwa na mashetani baada ya mapepo kutoka akaenda kuhuburi na baadae alikuja
kuwa na makanisa 10 Dekapori alikuwa askofu. Mtu mkorofi asikilizi watu
wafahamu shetani anakifunika kwa kumvuvia na tabia au anaingia ndani yako, huyu
ni muhibiri mwenyewe uwezo wakuhubiri
ila anakaa makaburini anajeshi la mapepo ndani yake ,amefungwa minyororo.
Unakuwa na mtoto ana tabia mbaya ya wanaume umechapa na ukachapa akasema
hatarudia na kuapa ameapa na kusema nikifanya uzinzi ardhi ipasuke niingie kama
Kora ila ukiingia ndani tu unakuta anaongea na mwanaume atume nauli ataenda
tena. Utagundua huyu sio wakuchapa ila anahitaji maombi maana hiyo ni tabia ya
shetani amepanda Roho iwe tabia anasema nitawaingia washauriwa Rahabu waongee
uongo. Ni uvuvio wa kishetani ulipovunjika wakamuona ana akili timamu amevaa
nguo anahubiri kotekote Dekapori na watu wakashangaa. Mtu anaye hasi mamlaka
ana uvuvio wa kishetani yuko nje au ndani,
“Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na
vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale
Thenashara walikuwa pamoja naye, Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka
katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu;
na wale Thenashara walikuwa pamoja naye, na Yoana mkewe Kuza, wakili wake
Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao”Luka 8:1-3
Mariam Magdalena
alikuwa na nyota ya fedha, pia alikuwa na mapepo saba alipofunguliwa akaanza biashara
na kutoa fedha kwenye huduma ya Yesu ina maana asingetokwa na pepo asingeweza
kufanya biashara, kuna mtu hapa anatakiwa kufanya baishara apate pesa awezeshe
kanisa, kuwa na pepo saba ni sawa na kuwa na watu saba wasio na miili ndani
yako. Mungu anataka waione nyota yako ili akuketishe na wakuu.
Kuna mtu ni muongo
hata kwenye mambo yasiyo ya kudanganya anadanganya, ni muongo tu ili kipawa
kifunikwe asionekane kuna mtu anatakiwa akupetenda. Kuna mambo usidanganye
unakaa wapi, umri au kabila lako, kuna kitu mtu anataka akupatie ila anajiuliza
kama kanisani umemdanganya je akikupa tenda ya kumjengea si utaiba hadi tofali.
Uvuvio wa shetani unampatia mtu tabia na kuna uvuvio wa ki-Mungu humpatia mtu
tabia. Tabia za ki-Mungu ambazo roho akikaa ndani analeta matunda ambayo ni upendo,
kuvumilia, kufadhili, utu wema, upole kiasi. Kuna roho zikikaa ndani ya mtu ni
mkorofi anatukana. Tabia mbaya watu
ambazo adui amewavuvia ili nyota isionekane watu wakulete. Leo vunja kwa Jina la
Yesu ili nyota yako ionekane ,wakuletee yale Mungu amepanga uyapate. AMEN.
0 Comments