google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ULICHOBEBA NDIO SABABU YA VITA YAKO

UFUFUO NA UZIMA UBUNGO CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 23 APRIL, 2023
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGE
SOMO: ULICHOBEBA NDIO SABABU YA VITA YAKO


Kuna wakati kwenye maisha watu wanaweza kukuchukia na wamejiandaa kukukwamisha kabla hata hujaanza kufanikiwa juu ya nafasi fulani yaweza kuwa ni mafanikio kwenye biashara, elimu au familia. Ni kwa sababu kuna mambo makubwa Mungu amekuandalia hujayaona kwenye macho ya mwili ila rohoni yameishaonekana. Kuna vitu umevibeba na kwa bahati mbaya hufahamu kama umebeba kwa sababu sisi ni roho iliyobebwa na mwili,mambo ya Roho yanaonekana na walio rohoni na huona hata kabla hayajadhihirishwa.

“Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele” Yohana 10:10.

Wanakupiga vita sababu ya vitu ulivyobeba, wameona rohoni nyota ya biashara,elimu,Watoto.Mungu alitujua kabla ya kukuleta duniani na mafanikio yako hayahusiani na elimu yako.

“Maneno ya Yeremia, mwana wa Hilkia, mmoja wa makuhani waliokuwa katika Anathothi, katika nchi ya Benyamini; ambaye neno la BWANA lilimjia katika siku za Yosia, mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda, katika mwaka wa kumi na tatu wa kumiliki kwake.Tena lilikuja siku za Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, hata mwisho wa mwaka wa kumi na mmoja wa Sedekia, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; hata wakati ulipochukuliwa mateka Yerusalemu, katika mwezi wa tano. Neno la BWANA lilinijia, kusema,Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto.Lakini BWANA akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru. Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema BWANA.Ndipo BWANA akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; BWANA akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako; angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung’oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.Tena neno la BWANA likanijia, kusema, Yeremia, waona nini? Nikasema, Naona ufito wa mlozi.Ndipo BWANA akaniambia, Umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize” Yeremia 1:1-12.

Kuna mambo tumebeba yanayovutia vita. Hakuna kitu alichofanya mtu mpaka akachaguliwa ila ni Mungu pekee ndiye anayechagua. Wapo wanaonekana wana sifa ila hawachagui , Mungu ndiye anayechagua na akikuchagua unatosha katika nafasi hiyo. Kuna mambo tumebeba yanayovutia vita. Hakuna kitu alichofanya mtu mpaka akachaguliwa ila ni Mungu pekee ndiye anayechagua. Wapo wanaonekana wana sifa ila hawachagui , Mungu ndiye anayechagua na akikuchagua unatosha katika nafasi hiyo.

Maana, tazama, nimekufanya leo kuwa mji wenye boma, na nguzo ya chuma, na kuta za shaba, juu ya nchi yote; juu ya wafalme wa Yuda, na juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wa nchi hii.Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema BWANA, ili nikuokoe” Yeremia 1: 18-19.

Yeremia alipewa huduma ya unabii na watu fulani waliinuka kumpiga vita,alipigwa vita kwasababu alibeba kusudi la Mungu na nia ya Mungu ni kwa ajili ya kujenga ufalme wake na  kuharibu ufalme wa shetani.

“Basi BWANA wa majeshi asema hivi, Kwa kuwa hamkuyasikiliza maneno yangu,angalieni, nitapeleka watu na kuzitwaa jamaa zote za upande wa kaskazini, asema BWANA, nami nitatuma ujumbe kwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu, nami nitawaleta juu ya nchi hii, na juu yao wakaao ndani yake, na juu ya mataifa haya yote yaliyopo pande zote; nami nitawaangamiza kabisa, na kuwafanya kitu cha kushangaza, na kitu cha kuzomewa, na ukiwa wa daima.Tena, nitawaondolea sauti ya kicheko, na sauti ya furaha, sauti ya bwana arusi, na sauti ya bibi arusi, sauti ya mawe ya kusagia, na nuru ya mishumaa.Na nchi hii yote pia itakuwa ukiwa, na kitu cha kushangaza; nayo mataifa haya watamtumikia mfalme wa Babeli miaka sabini” Yeremia 25:8-11.

Nebukadreza ni mfalme wa nchi anaabudu mizimu, anaenda kwa waganga ni muovu muovu lakini, Mungu anamuita mtumishi wangu Nebukadreza Kwasababu anataka amtumie kuwapiga watu waliomuhasi Mungu.

“BWANA, mkombozi wako, yeye aliyekuumba tumboni, asema hivi; Mimi ni BWANA, nifanyaye vitu vyote; nizitandaye mbingu peke yangu; niienezaye nchi; ni nani aliye pamoja nami?Nizitanguaye ishara za waongo, na kuwatia waganga wazimu; niwarudishaye nyuma wenye hekima, na kuyageuza maarifa yao kuwa ujinga;nilithibitishaye neno la mtumishi wangu, na kuyafikiliza mashauri ya wajumbe wangu; niuambiaye Yerusalemu, Utakaliwa na watu, nayo miji ya Yuda, Itajengwa, nami nitapainua mahali pake palipobomoka;niviambiaye vilindi, Kauka, nami nitaikausha mito yako;nimwambiaye Koreshi, Mchungaji wangu, naye atayatenda mapenzi yangu; hata ataunena Yerusalemu, Utajengwa; na hilo hekalu, Msingi wako utawekwa” Isaya 44:24-28.

Isaya anazungumzia mtu aitwaye Koreshi,ambaye bado hajafika ulimwenguni,Isaya alikuwa anaona vitu ambavyo hata bado havijatokea ,alimuona hata Yesu kabla hajazaliwa, aliona pia wana wa Israel wakienda utumwani miaka mingi kabla ya hayo kutokea.Mungu anaona mambo kabla hayajatokea na huyasema kwa watumishi wake.

“Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza viuno vya wafalme; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa.Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma; nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.Kwa ajili ya Yakobo, mtumishi wangu, na Israeli, mteule wangu, nimekuita kwa jina lako; nimekupa jina la sifa; ijapokuwa hukunijua.Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu; nitakufunga mshipi ijapokuwa hukunijua; ili wapate kujua toka maawio ya jua, na toka magharibi, ya kuwa hapana mwingine zaidi ya mimi; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine. Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni BWANA, niyatendaye hayo yote” Isaya 45:1-7.

Kila kusudi ni kwa ajili ya watu fulani,Mungu alimuinua Koreshi ili ajenge mji wa Israel kwa ajili ya Yakobo mtumishi wake na Israel mteule wake.Mungu yupo hapa duniani na anafanya mambo yote kwa ajili yakujenga ufamle wake tu. Mungu anapokupatia mafanikio katika mambo yako yote usisahau kumtolea Bwana kwa ajili ya kujenga ufalme wake kama ni mchango wa kujenga kanisa ama kupeleka huduma mahali.

“Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la BWANA alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, BWANA akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema, Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi;BWANA, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia; naye ameniagiza nimjengee nyumba katika Yerusalemu, ulioko Yuda. Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, BWANA, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee mpaka Yerusalemu, ulioko Yuda, akaijenge nyumba ya BWANA, Mungu wa Israeli, (yeye ndiye Mungu), iliyoko Yerusalemu. Na mtu awaye yote aliyesalia mahali po pote akaapo hali ya ugeni, na asaidiwe na watu wa mahali pake, kwa fedha, na dhahabu, na mali, na wanyama, zaidi ya vitu vitolewavyo kwa hiari ya mtu, kwa ajili ya nyumba ya Mungu, iliyoko Yerusalemu” Ezra 1:1-4.

Mambo yanayo kufanya uwe maana sana mbele za Mungu ni kuishi kusudi lake na kutenda vile akuelekezavyo. Mfalme Koreshi aliwaagiza watu wote wa Israel kwenda kumjengea Bwana nyumba katika Yerusalemu ,hili lilikuwa kusudi la Mungu ndani ya mfalme Koreshi.

Kuna vita aina mbili;moja ni vita kutokana na kusudi ulilobeba kutoka kwa Mungu,pili, ni vita kutoka kwa Mungu kwa sababu umeshindwa kwenda vile allivyokuagiza na kutenda mapenzi yake basi Mungu anakupia vita mwenyewe.Mungu aliwaonya wachungaji wa Israel akawaambia ole kwa wachungaji wa Israel maana wanakula kondoo.

“Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; akitenda maovu nitamwadhibu kwa fimbo ya binadamu na kwa mapigo ya wanadamu” 2 Samweli 7:14.

“Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti, na wa mataifa BWANA aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda. Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo. Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa BWANA, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake. Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni. Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, wala hakumfuata BWANA kwa utimilifu, kama Daudi baba yake. Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni. Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu. Basi BWANA akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha BWANA, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili” 1 Wafalme 11:1-9.

Mfalme Sulemani alibadilishwa moyona wake zake akamwacha Bwana akaanza kuabudu vitu, ndipo Bwana akamuamshia Mfalme Sulemani adui.

“Ndipo BWANA akamwondokeshea Sulemani adui, Hadadi Mwedomi; yeye alikuwa wa wazao wake mfalme wa Edomu. Naye Hadadi aliposikia huko Misri ya kuwa Daudi amelala na babaze, na Yoabu, jemadari wa jeshi, amekufa, Hadadi akamwambia Farao, Unipe ruhusa, niende mpaka nchi yangu. Farao akamwambia, Umekosa nini kwangu, hata, tazama, unatafuta kuirudia nchi yako? Akajibu, Hakuna, lakini unipe ruhusa tu. Tena, Mungu akamwondokeshea adui mwingine, Rezoni mwana wa Eliada, aliyemkimbia bwana wake Hadadezeri mfalme wa Soba, Naye akawa adui wa Israeli siku zote za Sulemani, zaidi ya madhara yake Hadadi; naye akawachukia Israeli, akamiliki juu ya Shamu. Na Yeroboamu wa Nebati, Mwefraimu wa Sereda, mtumwa wake Sulemani; ambaye jina lake mamaye aliitwa Serua, mwanamke aliyefiwa na mumewe; yeye naye akainua mkono wake juu ya mfalme” 1 Wafalme 11:14,21-26.

Lile jambo ambalo Mungu ameweka ndani yako ukilipuuzia Mungu atakupiga vita mwenyewe,pia na ukilitimiza hilo jambo shetani nae atakupiga vita,maandiko yanasema watashindana nawewe lakini hawatashinda.

Nini maana ya kutimiza kusudi lililo ndani yako kwa uaminifu? Mungu anapokupa kusudi kwa ajili ya watu fulani ni kasababu anataka atukuzwe kupitia hilo jambo.Na unapotimiza kusudi hilo kwa uaminifu ,Mungu anatukuzwa sana.Kuna changamoto fulani unazipitia katka Maisha yako sio zinatoka kwa shetani ila nikwa sababu umeliacha kusudi la Mungu ndio maana Mungu akaanza vita na wewe, acha kupata visingizio vya kutokufanya kusudi la Mungu kwa sababu ya familia,kazi au Watoto.Jitoe kwa moyo na akili na muda wako upate nafasi yakulitumikia kusudi la Mungu uache kupuuzia mambo ya Mungu. Haya Maisha unafanikiwa ni kwasababu Mungu anakusaidia.

BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA NZIMA YA JUMAPILI

Post a Comment

0 Comments