google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ROHO YA UDANGANYIFU

 

UFUFUO NA UZIMA UBUNGO CATHEDRAL.
IBADA YA JUMAPILI 21 MAY, 2023.
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGGE.
SOMO: ROHO YA UDANGANYIFU.

Silaha kubwa ya shetani ni udanganyifu ili shetani akupate lazima akudanganye, shetani ni muongo, mlaghai, yeye alikuwa wakwanza kudanganywa, silaha kubwa shetani utumia kuharibu watu, kuharibu maisha watu ni kwa kuwadangnya. Imeandikwa vaeni silaha za Mungu ili mpate kuzishinda hila za shetani, silaha yetu ina nguvu ili tuweze kushinda ulaghai wa shetani. Shetani nisawa na mwanaume muhuni ili ampate binti lazima amdanganye maana akija kama alivyo hakuna atakaye mpata anajigeuza na kuwa  malaika wa nuru, akija na mapembe hakuna atakaye mkubalia, ni sawa na muuza chuma lazima akudanganye anakuambia zimedondoshwa na wazungu sijui ni dhababu, na unaamini na unaenda atm kutoa pesa na kununua ukidhania ni dhahabu kumbe ni chuma ametumia udanganyifu kukuaminisha, ili kuolewa na mwanaume mdanganyifu lazima akulaghai, je angekuambia anataka kukuoa na kukuacha baada ya miaka miwili utamkubalia, hapana lazima akulaghai. Anakudanganya kuwa amesafiri dunia nzima hajaona mwanamke kama wewe, kumbe ni kwenye ulimwengu wake huu wote ni udanganyifu, maisha ya mwanadamu yalikuwa sawa kuna mahali Mungu alitaka mwanadamu awe, ila amedanganywa mpaka maisha yakawa magumu, hatukosi kuzijua fikra zake ili asipate kutushinda.

 

Huwezi mshinda shetani kama hujui njia zake za udanganyifu, kuna watu ni waongo na uongo wake unafanya kazi katika eneo analokaa kama anaishi kijijini anaweza kudanganya wa kijijini ila wa mjini asiweze, akivuka nje ya nchi hawezi danganya ila shetani anaweza kudanganya watu wote wa mjini na kijijini, wasomi na ambao hawajasoma.

Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake”. 2 Wakorinthro2:11

Shetani anaitwa nyoka wa zamani mbinu zake ni zile zile. Watu wa zamani wanaweza kubashiri baadae yako maana wameishaona unayopitia mwisho wake utakuwa je maana yeye aliwahi kuishia pale ambako anakuambia utaishia. Anaweza kuwa mshauri nzuri wa ndoa maana yeye ndoa yake ilimshindaga kwa hiyo ni mshauri mzuri. “Iko njia ionekanayo sawa machoni pa mtu lakini mwisho wake ni njia ya mauti “. Mithali 16:25. Ni vizuri kuwasikiliza watu wazamani maana ile kukaa muda mrefu imempa hekima. Ni sawa na mtu aliyewahi kuibiwa hawezi kuibiwa tena maana anajua hizo mbinu. Wasikilize watu wazamani maana wana siri ambazo zitachukua muda kuzijua maana hazijaandikwa kitabuni wala popote.

 

Shetani ni wazamani na mbinu zake ni za zamani kwanini zinafanya kazi, sio kwa sababu umesoma kitabu cha kuwa na ndoa nzuri kitakusaidia maana aliyeandika ameandika kwa uzoefu wake na maisha aliyopitia yeye haimanishi wewe kitakufaa kwenye ndoa yako uliyonayo au utaishi maisha kama yake. Wewe unahitaji hekima kutoka kwa wazee wa kwenu. Ayubu anasema waulize kizazi cha zamani watakuambia. Shetani anaitwa nyoka wa zamani audanganye ulimwengu wote ili uwe salama inabidi uijue kweli ya neno la Mungu, mambo hayako kama yanavyoonekana waweza kuona mazuri kumbe nyuma yale kuna ubaya, Mungu akisema kweli ndio inakuwa hivyo. “ Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala, Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo. Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone. Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha. Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala”. Mwanzo 3: 1-13

Huu mti sio mti mgeni maana anauona siku zote na anajua akila matunda yake hapo atakufa kwa hiyo kila akiuona anaona ni mauti ila aliongea na mtu akamwambia unafaa na mwanamke akaona kinatamanisha. Zamani ilikujua upo uchi lazima uambiwe na Mungu ndiye atakayekuambia, maisha yangekuwa raha sana maana sasa hivi kuna kununua nguo ni gharama. Kwahiyo Mungu pekee ndiye anayeweza kukuambia upo uchi au ule kitu ambacho Mungu amekuzia kula.

Kuna mambo Mungu hajakuambia ili uwe na amani, ajakuambia kuwa wanataka roho yako kesho ili uwe na amani.  Kabla ya udanganyifu Adamu alipomuona Eva alisema wewe ni nyama katika nyama zangu wewe ni mfupa katika mfupa wangu ila baada ya udanganyifu akasema ni huyu mwanamke uliyenipa. Kila mwanamke mwenye miaka 25 kwenda juu aliishawahi kuambiwa maneno mazuri sana ila kuna siku mambo yalibadilika akasema ni huyu mwanamke niliyepewa na Pastor Baraka. Kuna mtu aliniambia nyuma ya mwanamke mwenye majonzi au msongo wa mawazo sio kwamba ni biashara ina mchanganya wala masomo hapana ila ni mwanaume aliyewahi kumpenda akamseme maneno makali. Imeandikwa enyi wanaume wapendeni wake zenu, ghafla siku moja akaja mgeni na kumkuta mwanamke na kuanza kuuliza maswali, shetani anajua ukweli ila hawezi kusema ukweli, anaitwa baba wa uongo anapoulizwa maswali sio kama hajui ila anataka kukuuliza ili akudanganye, mwanamke alipoulizwa habari ya kula matunda akasema Mungu amewakataza wasile matunda ya mti huo, ila shetani akacheka akamwambia sio kweli ila mti huu unaleta kujua mema na mabaya. Yule mwanamke akaona kumbe mti wafaa kula matunda yake, aliposema nami roho ikaniingia unapomsikiliza shetani roho itakuingia, unaanza kuona mambo yale uliyoona sio sawa ila unaanza kuyazoea na kuona ni ya kawaida, siku zote uliamini kuwa mwanamke anapaswa kumtii mume wake ila baada ya kuangalia tamthilia sana ukabadilika, unakuta katika tamthilia hiyo hakuna kipande chochote kinaonyesha mwanamke anapaswa kumuhudumia mume wake. Hapo ndipo nyoka alikusemesha, kuna watu ndoa zinasumbua maana anaishi maisha ya kwenye tamthilia anasubiria mumewe amlete mauwa, umfungulie mlango wa gari hayo ni maisha ya tamthilia. Unapomuoa binti wa hivyo itakusumbua. Namna ya kuona mambo ya ndoa ishaharibiwa na shetani.

Binti mmoja alikuja ofisini anataka tuongee akasema pastor unaweza kuamini mpaka saa hizi saa sita mchumba wangu hajanitakiwa heri ya kuzaliwa kwenye kikundi cha vijana kanisani hajatuma ujumbe huko, pia hajamuweka status, niliona ni upuuzi mtupu. Ila kwakuwa mimi ni mchungaji nikamsikiliza, nikamwita kijana, akasema nimemtumia meseji ndefu ya mapenzi saa sita usiku, amepanga maneno, ikamfikia binti muda huo huo kwenye simu yake binafsi,  binti akasema ameiona ila anataka atume ujumbe kwenye kikundi cha vijana kanisani. Lakini haya yote ni mambo ameona kwa mabinti wenzake au kwenye tamthilia  ndio anaamini nikupedwa huko. Hiki nikizazi cha maonyesho. Maisha yako ya sirini unataka uyaweke hadharani ila hii ni kwasababu ameonyeshwa, amesikia, ameona mahali kupitia kwa nyoka wa kwenye tamthilia. Kuna mambo ukianza kuyasikia mtazamo unabadilika kile ulichoona mwanzoni kinafaa unaanza kuona tofauti, aliposema nami roho ikaniingia ni hatari kuwasiliza baadhi ya watu ni hatari amejaa sumu kuhusu viongozi wakanisani, maana uongo unaanza na mtazamo , ulisema bila baba usingekuwa hapo ulivyo, alinitoa msukuleni ila sasa unasema Gwajima  ni nani na uliamini baba ni mkuu kuliko wote ila siku ulivyoongea na nyoka ndipo ulibadilika. Uongo hauna madhara kama ukisikia usiamini ila ukiamini pale pale mtizamo wako unabadilika.

Sauli anaambiwa na Samweli ulikuwa mdogo machoni pako mpaka siku ulipopakwa mafuta ila sasa naongea na wewe unaongea, ndivyo walivyo watu walikuwa wadogo mpaka siku walivyosikia sauti nyingine, ulikuwa na heshima unawaheshimu baba, mama, ila siku roho ilipoingia ukaacha kumuheshimu. Watu wengi wakorofi ni watu wasiojua mamlaka maana hawajawahi kukaa chini ya mamlaka. Mtu yeyote anayemuheshimu baba yake mzazi hatapata shida kumuheshimu mchungaji wake. Tulikuwa na baba zetu wa kimwili tukawastahii, je ni jambo gumu kujiweka chini ya baba wa kiroho? wale watoto wako katika kuheshimu mamlaka.

Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele; kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa. Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima”. Mwanzo 3:22-24

Mahali walipokuwa wamewekwa wakafukuzwa maana wamemsikiliza mwingine na sio yule aliyewaweka. Yule mwanamke mwanzoni aliogopa lakini ghafla akaacha kuogopa. Nimtende Mungu huo  uovu mkubwa namna hii. Zamani ulikuwa unaogopa kutenda dhambi, kuongea na mwanamke ambaye hujamuoa, ila sasa unajisifika na kusimulia hii ni kwasababu umesikia sauti ya nyoka, mshahara wa dhambi ni mauti Mungu ameishasema wawe wamekuona au hawajakuona dhambi inaitwa dhambi haijalishi umefanya na nini,. Msidanganyike chochote apandacho mtu atakivuna amesema Paulo.  Waheshimu baba yako na mama yako ili uishi miaka mingi, Mungu akisema jambo hiyo ni sheria, azinineye na mwanamke anaiangamiza nafsi yake mwenyewe hata kama sio leo itatimia, alisikia sauti ya Mungu akiambiwa asile haya matunda na ana ujasiri wakusema kabisa Mungu alisema usile matunda haya, ila roho ya udanganyifu ili pomuingia akaona yafaa, akaona  kumbe kuna siri kuwa anaweza kuwa Mungu hakuwaza dunia yake ataiitaje na pia akapata ujasiri wakumshawishi na Adamu, roho ya udanganyifu ndivyo ilivyo unadanganyika na unapata ujasiri wa kumdanganya mwenzake. Yeye aliamini akiolewa nje yakanisa atakuwa sana ila hakuwa sawa na anapata ujasiri wakuwaambiwa wengine waolewe ni sawa ila hayuko sawa.

 

Roho ya udanganyifu inafanyakazi kwa kuaminisha kuwa dhambi haina madhara, inakuambia ukiishazini utubu maana dhambi zetu zijapokuwa nyekundu kama damu atazisafisha na kuwa nyeupe kama lethuji. Binti mmoja alikuwa anaishi maisha ya ndoa kabla hajaolewa, nikamwambia Yesu akija leo utasema je, na unafahamu kabisa hii ni dhambi. Akasema pastor niko makini sana anasema siku zote akiwa anazini huwa anatubu pale pale, nikashangaa haya ni masomo gani, alisoma.

Ila haya mambo ni kwasababu mtu ana mtizamo mwingine anao na hauji hivyo hivyi ila kuna roho ya uovu inakudanganyika. Neno linasema Mungu hadhihakiwi, ukipanda uovu utavuna uovu. Shetani anakujaza moyo wako uongo, Petro anamwambia Anania kwanini shetani amekujaza moyo wako, mtu anakuwa mbishi anakutwa amezini ila anataka ushahidi. Maneno hutoka na kile kilichojaa moyoni ili useme uongo lazima moyo wako ujae uongo ndipo useme, watu wanaishi maisha ya uongo anataka kuwa furahisha watu  anadanganya kwasababu anaishi maisha yasio yake.

Kulazimisha mambo kuhusu maisha yako inabidi udanyanye na kutenda dhambi, Mungu ni wa hatua kwa hatua baki hapo ulipo, anzia hapo hapoo wewe sio wa kukaa Sinza nyumba nzima wewe ni wa Msewe chumba kimoja. Utaishi maisha ya furaha sana na kuwa na amani hatakama watu hawakuelewi ukiishi maisha yako Mungu aliyoamuru, baki pale pale mpaka Mungu atakapo kuambia, kaa hapo jangwa utapita na utaikumbuka maana bwana alikuongoza, mwanadamu hataishi kwa mkate, ni maisha magumu ila bwana anataka akufundishe, utapita jangwani ila bwana alitaka uone njia, Mungu aliwaacha jangwani na kuwalisha mana kwa sababu alitaka wajifunze.

Hata mimi nimewahi kukaa jangwani, nakula mchele, mchele una tofauti na wali, nimekaa kwenye pagale la mtu, sikuwa na kitu, sina pesa, siku inaisha hata sijui imeishaje, sikuwa na chochote ila nilichumbia mchumba nikiwa jangwani ila nilikuwa na maneno mazito. Nilikuwa nampanga mke wangu na mwambia mimi nitakuwa mtu mkubwa sana, hakikisha una passport utakuwa unapeleka watoto marekani kusoma ila sasa hivi wanasoma goba, kila mtu ana wakati wake wa jangwani hata kama upo jangwani kuna wakati wa wakutoka. Mabinti wanaharibikiwa kwenye Maisha yao, maana aniga maisha ya wale marafiki zake wa chuo. Kuna mtu mmoja ana mafuta na amekaa jangwani miaka 15 na anasema ilikuwa vema kukaa jangwani ili kujifunza njia za bwana. Unakuta binti ana madeni kanisani na hawa ndio wanaongoza kuwaumiza wengine unakuta kuanzia juu mpaka chini amekopa, anadanganya atalipa mwisho wa mwezi wakati hana kazi, anaishi maisha ya kuwafurahishwa watu, maisha ya ulaghai, msubirie Bwana kuna wakati wako wakutoka, roho ya udanganyifu inakujaza moyo.

 Namna ambavyo roho ya udanganyifu kufanya kazi.

Mtu wa kwanza Mfalme Ahabu amekaaa kwa amani miaka 3 siku moja akapata wazo la kwenda kupigana Ramoth-Gileadi na akaenda kuuliza kwa manabii ambao wamejazwa na roho ya uongo. Akauliza kwani hakuna mtu wa bwana maana yake wale hawakuwa wa Bwana. Shetani akitaka uharibikiwe anakupandia chuki unawachukia watu ambao unawahitaji. Wakakaa miaka mitatu pasipo vita kati ya Shamu na Israeli. Ikawa, mwaka wa tatu Yehoshafati mfalme Wa Yuda akamshukia mfalme wa Israeli. Mfalme wa Israeli akawaambia watumishi wake, Je! Hamjui ya kuwa Ramoth-Gileadi ni yetu? Nasi tumenyamaza tusiitwae mkononi mwa mfalme wa Shamu?”1 Wafalme 22:1-3

Mikaya akasema, Sikia basi neno la Bwana; Nalimwona Bwana ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kuume na wa kushoto”. 1Wafalme 22:19

Akaitwa Mikaya, Mikaya akasema mimi mfalme Ahabu nimemuona Bwana ila hawa manabii zako wanaongea mambo ya kukufurahisha kwa sababu wamepewa posho, akasema ameona kifo cha ajabu. Mungu ana namna ya kuongoza watu, Mungu anaongoza watu kwa kutuma mamlaka. Shetani akitaka kumuua mtu anampa jambo litakalompelekea kifo. Unaambiwa hiki acha utaharibikiwa lakini hutaki. Shetani anaweza kuvuvia watu wako wa karibu ili wakuvuvie ukaolewe ufe. Petro alipokuwa anahubiri waliposikia maneno Kornelio na wenzake wakajaa roho, kwa nini? kwa sababu maneno ni roho. Mtu yeyote aliye kinyume cha Baba hata kama ni rafiki yako kaa naye mbali. Mtu yeyote anayeongea vibaya kuhusu kanisa kaa naye mbali bila kujali beji yake. Ukijifanya mwerevu kuliko Mungu utaharibikiwa, Mungu mwenyewe alimtupa shetani nje baada ya kuharibikiwa. Hutafanikiwa kwenye maisha kama hutajua kanuni, mtu akimuasi Baba ameasi watu wote wa Baba, kuambatana kuna gharama.

Huwezi kwenda na mtu mwovu usiwe mwovu, wawili hawawezi kwenda pamoja isipokuwa wamepatana. Mtu yeyote anayeasi kanisa ana sumu kuhusu viongozi, udanganyifu unahisi kwamba unaweza kwenda kinyume na kanuni na bado ukawa uko sawa. Mtu akiwa rafiki yako kuna mambo utamuuliza sio Mchungaji. Maandiko yanasema kuna watu wameharibika akili zao, watu huwa wanaharibika, Sauli alipoharibika Mungu alimkataa, chakula hata kama ni kizuri kikiharibika unakitupa. Mtu yeyote anayeongea vibaya kuhusu kanisa, kuhusu viongozi hafai kuwa rafiki yako. Roho ya udanganyifu inamfanya mtu hata kama Baba aliwahi kumsaidia lakini hawezi kuona kama alisaidiwa. Ni udanganyifu kuanza kupambana na mtu aliekuzaa. Tena shetani akasimama juu ya Israeli, akamshawishi Daudi kuwahesabu Israeli. Basi Daudi akamwambia Yoabu, na wakuu wa watu, Nendeni kawahesabu Israeli toka Beer-sheba mpaka Dani; mkanipashe habari, nipate kujua jumla yao. Naye Yoabu akasema, Bwana na awaongeze watu wake mara mia hesabu yao ilivyo; lakini, bwana wangu mfalme, si wote watumishi wa bwana wangu? Mbona basi bwana wangu analitaka neno hili? Mbona awe sababu ya hatia kwa Israeli? Lakini neno la mfalme likawa na nguvu juu ya Yoabu. Kwa hiyo Yoabu akaenda zake, akapita kati ya Israeli wote, akafika Yerusalemu “. 1 Mambo ya Nyakati 21:1-4

“Neno hilo likawa baya machoni pa Mungu; kwa hiyo akawapiga Israeli. Naye Daudi akamwambia Mungu, Nimekosa sana, kwa kuwa nimelifanya jambo hili; lakini sasa uuondolee mbali, nakusihi, uovu wa mtumwa wako; kwani nimefanya upumbavu kabisa. Naye Bwana akanena na Gadi, mwonaji wake Daudi, akisema, Nenda ukanene na Daudi, ukisema, Bwana asema hivi, Nakuwekea mambo matatu; katika haya ujichagulie moja, nikutendee hilo. Basi Gadi akamwendea Daudi, akamwambia, Bwana asema hivi, Kubali upendavyo; miaka mitatu ya njaa; au miezi mitatu kuangamia mbele ya adui zako, ukipatwa na upanga wa watesi wako; au siku tatu upanga wa Bwana, yaani tauni katika nchi, na malaika wa Bwana akiharibu kati ya mipaka yote ya Israeli. Haya basi ufikiri ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma” 1 Mambo ya Nyakati 21:7-12

Shetani akitaka kuleta uharibifu kwa mtu anamfanya mtu aone jambo baya aone jema, baada ya kufanya uharibifu unagundua kuwa umefanya jambo la baya. Mashetani ya kudangaya unaweza kuyazuia, unaweza kuyafunga. Ukidanganyika hata huu ujumbe unaona ni wa uongo, mambo ya kweli unaona ya uongo, mambo ya uongo unaona ni ya kweli.

Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.  Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake; naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala”. Ufunuo 20:1-3,7-9

Shetani akifungwa hawezi kudanganya japokuwa huwezi kumfunga shetani mwenyewe kwa sababu muda wake bado ila mapepo yake unaweza kuyafunga. Ili upigane na mtu lazima uone kwanza mnalingana, akija Mandonga hamuwezi kupigana nae kwa sababu sio saizi yako. Kupigana na mwenye mamlaka ni lazima ujiinue kwanza ila ni kazi ya shetani anakudanganya. Omba kumfunga mdanganyifu, roho iliyotumwa, mashetani waliotumwa, huwafunga wafalme wao kwa minyororo ya chuma AMEN.

 

Post a Comment

0 Comments