google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

USIOGOPE WALIO PAMOJA NA WEWE NI WENGI KULIKO WALIO NA PAMOJA NA ADUI.

 

UFUFUO NA UZIMA UBUNGO CATHEDRAL.
IBADA YA JUMAPILI 7th MAY,2023.
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGE.
SOMO: USIOGOPE WALIO PAMOJA NA WEWE NI WENGI KULIKO WALIO NA PAMOJA NA ADUI.


Maisha ya duniani yana watu wanaokupenda nawaokuwazia mema ukioa wanafurahi, ukipata mimba wanafurahi lakini pia maisha kuna watu ukipata vitu wana kasirika ukijenga, ukioa, ukichumbiwa wanachukia, pia wanafurahi ukiaribikiwa. Usidhani kila mtu atakupenda hata uwe muovu vipi kuna watu watakupenda hata uwe mwema vipi kuna watu watakuchukia. Nani anamfahamu mtu mmoja mwovu? Hata mimi namfahamu mtu mmoja alikuwa na kikundi cha kigaidi anawaongoza watu alikuwa akipanga mipango anawafundisha watu wake wanavaa mabomu wanaenda mahali wanajilipua wanauwa watu maelefu. Nilidhania akifa watu watafurahi, lakini alipokufa watu wakaandamana namfahamu alikuwa anaishi kule Iraq. Ameuwa watu wengi sana ila siku alipouwawa watu wakaandamana watu wakakasirika ni muovu ila watu wanampenda, unaweza kuwa mwema ila watu wakachukia wakasema usulubiwe. Kabla Yesu kusulubiwa ilipigwa kura kati ya Yesu na Barba. Pilato akaitisha uchaguzi kuna wagombea wawili wa kifo na msalaba ule pale. Kuna Yesu wa Nazareth muhubiri wa injili, mponyaji, mfufua watu ana maneno yamejaa neema anasaidia watu hajawahi kumlaani mtu hata watu walipomuita ana mapepo aliwasamehe hajawahi kumtendea jambo baya mtu. Barba ni muuwaji, unahisi kati yao nani alitakiwa kupigiwa kura ya kufa? Yesu alipigiwa kura ya kufa asulubiwe, Pilato akawauliza anakosea nini, wakasema sio suala la kosa yeye afe tu sio kwamba amekosea kitu, furaha yetu akiwa amesulubiwa ndio furaha yetu. Pilato akasema yeye ni mtawala na kuna sheria na anaruhusiwa kuuwa ila wenye makosa, niambieni kosa lake nikimuhuku kifo niwe na uthibitisho kwamba mimi Pilato nimeagiza Yesu wa Nazareth ameuwawa kwa kosa hili na hili, wakasema sio suala la makosa ,Pilato akanawa mikono.

Katika binadamu hatari sana ni wanadamu, Yesu alitakiwa aishi miaka mingi lakini sio hivyo, nataka ujue kuanzia leo wote wanaokupiga vita kuna walioupande wao na wote wanaokurufahia kuna walio upande wao, hakuna aliye katikati asiyepamoja nami yu kinyume nami. Asiyekupenda anakuchukia huwezi kunipenda na kunichukia. Usiogope walio kinyume chako maana walio pamoja na wewe ni wengi kuliko walio pamoja na wao. Kuna mambo yanaonekana hayawezekani kwa kiwango kadri unavyokuwa kiroho unagundua kuna mambo yanwezekana kwasababu ushajua yote yanawezekana, sasa kanisani anakuja mtu aliyeokoka leo, jana, mwaka wote wako hapa inabidi ufundishe wote wakuelewe ndio maana Mungu lazima awe ili kila mtu aelewe.

Basi, mfalme wa Shamu alikuwa akifanya vita na Israeli. Akafanya mashauri na watumishi wake, akasema, Kituo changu kitakuwapo mahali fulani. Yule mtu wa Mungu akapeleka habari kwa mfalme wa Israeli, kusema, Jihadhari, usipite mahali fulani; kwa sababu ndiko wanakoshukia Washami. Mfalme wa Israeli akapeleka watu mpaka mahali pale alipoambiwa na yule mtu wa Mungu, na kuhadharishwa; akajiokoa nafsi yake, si mara moja, wala si mara mbili. Basi mfalme wa Shamu moyo wake ukamfadhaika sana kwa ajili ya jambo hili; akawaita watumishi wake, akawaambia, Je! Hamtanionyesha, ni mtu yupi miongoni mwenu aliye upande wa mfalme wa Israeli? 2 Wafalme 6:8-19

Mfalme anapata picha kuwa kuna wafanyakazi ambao hawako upande wake, hata wewe unaweza kuwa na mtu au rafiki una mwambia siri zako halafu baadae unazisikia upande wa pili. Mfalme wa shamu anaulizia mipango wa vita anapanga na watu wake inakuwa je mfalme wa Israel kila akienda anamkuta, ingekuwa ni mara moja au mbili ningesema ni bahati. “Mmojawapo wa watumishi wake akasema, La, bwana wangu, mfalme; lakini Elisha, yule nabii aliye katika Israeli, humwambia mfalme wa Israeli maneno uyanenayo katika chumba chako cha kulala. Akasema, Enendeni, mkamwangalie aliko, nipate kupeleka watu kwenda kumchukua.Akaambiwa ya kwamba, Tazama, yuko Dothani. Kwa hiyo akapeleka huko farasi, na magari, na jeshi kubwa; wakafika usiku, wakauzingira mji ule pande zote. Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka, na kwenda nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari, wameuzingira mji ule. Mtumishi wake akamwambia, Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje? Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao. Elisha akaomba, akasema, Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote. Na walipomtelemkia Elisha akamwomba Bwana, akasema, Uwapige, nakusihi, watu hawa kwa upofu. Akawapiga kwa upofu sawasawa na neno la Elisha. Elisha akawaambia, Njia hii siyo, na mji huu sio, nifuateni mimi, nami nitawapeleka kwa mtu yule mnayemtafuta. Akawapeleka Samaria”. 2 Wafalme 6:8-19

Elisha hakuitaji kwenda kuwaona ili achungulie wako wangapi akasema haijalishi wako wengi kiasi gani ila najua walio upande wetu ni wengi kuliko walio upande wao, hapa nataka unielewe hapa, Elishi haongei Habari za watu walio mzunguka, farasi walionao, haongeichochote kuhusu hawa adui waliotumwa na mfalme wa Shamu, akijilinganisha yeye na wao ataogopa na hilo ndio kosa alifanya Gehazi. Elisha akipima wenzake na wenzao adui wanzake niwengi kuliko wenzao. Kuna mambo tukiyasoma kwenye biblia tunahisi hivi watu wazamani walikuwa sio wakawaida, ukimsikia Eliya, Elisha, Daudi, Daniel ni watu hatari, hapana walikuwa watu kama sisi. Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi ni watu wakawaida ila ni watu waliomuamini Mung una maneno yake, sitaki udhani wala kufikiri kwamba Elisha aliona rohoni halafu akaona jeshi, hapana aliamini kile Mungu amesema alikuwa anasoma biblia ya wakati ule ni ile ambayo kitabu hiki cha wafalme hakikuwepo, maana hii imeandikwa baadae sana unaelezea habari ya mtu tayari ashafanya , zamani biblia ilikuwa na vitabu vitano tu, hakuna Waefeso, wala Mathayo hapa kuna Mwanzo, Kutoka, Mambo ya Walawi, Hesabu na  Kumbukumbu la Torati . Elisha alisoma ile kumbukumbu ya torati 20 inasema utokapo kwenda vitani ukaona adui zako ni wengi kuliko wewe na magari yao ni mengi kuliko yako usiwaogope, ukitoka ukaona kuna watu wengi kinyume chako wana elimu kubwa  kuliko yako, uzoefu wakazi kuliko wewe, wana vifaru vikubwa kuliko wewe usiwaogope. Huwa nasema tusipoamini maneno ya Mungu, basi Mungu hana msaada kwetu hawezi kutusaidia maana Mungu akitaka kukusaidia hakupi fedha ila hulituma neno lake. Hata leo amekuja akusaidie ametuma neno usiogope. “ Utokapo kwenda vitani kupigana na adui zako, na kuona farasi, na magari, na watu wengi kuliko wewe, usiwaogope; kwa kuwa Bwana Mungu wako, yu pamoja nawe, aliyekukweza kutoka nchi ya Misri. Na iwe, msongeapo mapiganoni, kuhani na akaribie na kusema na watu, awaambie, Sikizeni, enyi Israeli, hivi leo mwasongea mapiganoni juu ya adui zenu mioyo yenu na isizime; msiche, wala msiteteme, wala msiingiwe na hofu kwa ajili ya wao; kwa maana Bwana, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi”.Kumbukumbu la Torati 20: 1-4. Maisha ya duniani ni Maisha ya vita kila siku unapotoka kwenda kazini au biasharani lazima ukumbuke kuwa unatoka kwenda vitani.

Vita haimanishi utakutana na mtu akuambie tupigane vita, wewe siuna Yesu  yeye anamapepo mpigane vita, hapana Maisha yetu ni maisha ya vita unapoamka asubuhi ukumbuke unatoka kwenda vitani. Ni nani anataka kwenda vitani halafu afe, unahisi hauna vita uko kazini maana unafanya kazi Dawasco maana unawasaidia watu kupata maji vita inatoka wapi?

Ukiwa na akili kila siku ni vita hutatoka bila kujipanga, kabla hujatoka nyumbani ni lazima unene kwa lugha hata lisaa limoja, mkiomba kila wakati katika roho hiyo ni silaha ya vita, nena angalau lisaa limoja halafu nenda kazini. Kwasababu wenzako nao wanatoka wanakuja vitani usipofanya hivyo utashangaa boss wako anakuchukia na wewe nimfanyakazi bora, ni kwasababu wenzio wanatoka wakienda vitani, wana ufahamu huo ndio maana hawaanzi biashara bila kuwa na ufahamu huo hata akienda dukani kuna kitu anachoma na asubuhi ameomba na moja wapo ya maombi yao ni kuwalaza makafri na wewe ni mmojawapo wa kafri.

Wewe unaamka saa mbili unaanza kukimbia kuwahi mwendokasi  na ulilala saa mbili jana ndio maana una umaskini wakutosha. Biblia inasema mtu anaye lala sana naumaskini wa kutosha. Siku anachelewa kulala alikuwa anaangalia movie au anachat mambo ya kijinga na mchumba wake. Anakesha anachat na alisema hawezi kuja mkesha kwasababu kesho anaenda kazi lakini mpaka mkesha unaisha yupo anachat tu hajalala. Haiwezekani ulale saa 10 alfajiri halafu asubuhi uamke uombe atamka saa mbili asubuhi na kuwahi mwendokasi kuwahi ofisini. Ni hatari kuwa vitani na usijue uko vitani kila ambacho unacho kuna ambaye anakitaka hata kama ni chako kihalali kuna mtu anataka. Hata kama mumeo ni Sherphed shetani anazungukazunguka akimtafuta ammeze, anasema Yesu shetani anawataka mitume, ana kazi gani na mitume je anataka kufungua huduma, ila Yesu anasema shetani anawataka ili awapepete kama ngano, nini maana ya kupepeptwa ni kile kili mpta petro baada ya kuppetwa ni yue aliyesema wewe ni mana wa mungu aliyehai alipopepetwa akasema simjui mtu huyu. Mume alipokuoa siku ya kwanza nilipokuona ndio siku niliyoanza kuishi wewe ndio furaha ya maisha yangu na ibarikiwe siku ambayo mama yako alitunga mimba, ibarikiwe siku ulipoitwa Happy na siku mama yako aliyokuzaa hapo bado hajapepetwa. Ndio maana vijana wasiku hizi nirahisi kukupetwa. Wamtumainia Bwana ni kama mlima wadumu hawaondoshwi, unafanya mizaha na mambo ya msingi wa maisha huna muda wa kuombe na ibada.

Hii ya kujiona watu wakawaida ila wenzetu hawako hivyo kila siku kabla ya kwenda kazini lazima aombe hata mvua inyeshe iwe radi au laah. Acha mizaha na mambo ambayo ni ngome yetu. Bwana ni ngome yetu na nuru yetu tumuogope nani watenda mabaya waliponikaribia wanile nyama yangu watesi wangu walijikwaa wakaanguka. Wanakukaribia ili wale nyama yako maana mume wako ni nyama katika nyama yako, na watesi wanapenda nyama yako.

Shetani huwa anazunguka zunguka na alipomuona Ayubu, alipomtaka ndani ya siku moja Ayubu hana mali tena, hana watoto, mali wala ndoa imara ila ametikiswa. Wewe huna muda kanisani mvua ikinyesha huendi ila kazini unaenda. Msikitini wanaenda kusali Allah yukopale huwezi kuchat mbele yake ila mbele ya Jehovah Nisi unachat, yeye anaongea na wewe unaongea na simu. Nawapenda waislamu maana wanajua maisha yao yanamuhitaji sana mungu wao akiwaambia waombe mara tano kwa siku awe maskini au Tajiri, ana pesa au hana pesa, amekula au hajala. Ila sisi hatujui unampenda Mungu au ni shida tu unalala kanisani, siku ukipata kazi ukalipwa laki tatu na ukapanga chumba Bonyokwa na kina feni atakuambia kanisani kuna joto. Lakini wenzetu waislamu wanakaa chini na hawabaguani na wanaongozwa na imamu hajasoma shule na hawamuongelei maana ni mtu wa rohoni, akiwa na kazi hawezi kukuajiri wewe maana ni kafri, wanapenda  wanakaa pamoja  wanadumu katika fundisho la imamu.

Sisi vitu vidogo ambavyo tumevibatiza ni mafanikio na sio mafanikio, yaani tunadanganyika sana na vitu vya kidunia yaani mtu akijenga tu kijumba akinunua gari ashakuwa mtu mkubwa sana. Hutakikuelekezwa na kiongozi wako kwasababu unamuona amependa mwendokasi amebanana na wewe uko kwenye gari yako. Akisema tusome neno la sadaka unasema moyoni huna pesa ndio maana unaongea suala la sadaka. Kuna watu wanaongea kinyume na mhubiri ni vile tu hajapewa kipaza sauti. Wanaongea zaka ni hawa wasio na pesa, nitoe kanisani million moja ya nini, yaani vitu vidogo unaona vikubwa hutaki kuonywa, kukaripiwa ili mtu akukaripie lazima uwe china yake kama mnalingana hapana hii ndio leoalikuwa nayo Sauli, maana alijikuza akawa kama Samweli. Samweli akimwambia hivi nay eye anaongea kinyume chake anamrekebisha, kuwa tumeona hivi tutunze kondoo wengine kwa ajili yadhabihu, Sauli umehasi sauti ya Bwana ila akakata na kusema nimetii.

Ukiwa mkubwa baba yako na mama yako hawezi kukuonya sababu ushakuwa mkubwa huwezi kuonywa unakuwa mkali sana sababu una wagerasi, hata mambo watu wanakuzidi wanakuonya unakata kusikiliza, umekuwa mkubwa mtu yeye yote anayekuzidi umri hata kama unamzidi mfanikio anakuzidi maarifa kwahiyo anapokuambia jambo msikilize.

Mtu kwenye ndoa miaka 30 ameona mengi wewe una uchumba wa siku 30 acha ubishi, kwakuwaulisoma kitabu cha mambo 7 ya kuwa na ndoa yenye furaha. Kwahiyo wenzetu Maisha kwao ni vita ndio maana hawawezi kupuuzia, ikifika muda wa ibada hata kama umekujakununua bidhaa za duka zima hata kama una billion moja atakwambia muda wa swala lakama Allah amenipangia hiyo riziki nitaikuta. Kama sio riziki yangu sio riziki kisicho riziki hakiliki anafunga duka mbele yako. Ila wewe mkristo unasema Pastor muda ule ule wa ibada wateja wakafuruka bwana akaleta wateja kama mafuriko. Hii ni vita na niya rohoni hata kama amesoma bado kuna vitu vya rohoni anafanya hata kaka ni bilionea.

Mo Dewji alikuwa anahojiwa atoe ratiba yake kwa siku, akasema siku yake inaanza saa 11 kwa saa nzima ya sala, haombiili apate chakula cha mchana maana anacho , akienda kazini ile saa saba msikitini, jioni pia msikitini analala saa nne usiku.  Nataka tuamini maisha ni vita popote ulipo uwe bisharani, gengeni ni vita utaona wenzako ni wengi wanafanya vile vile kama wewe. Usiwaogope maana mimi Bwana naenda mbele zako inatakiwa Bwana anende mbele yako ili usiwaogope na ili Bwana aende mbele yako kuna mambo natakiwa kuyafanya. Maana wenzako wanao aliyepamoja nao maana kuna jambo wamefanya asubuhi maana hakuna mambo yaroho ambayo wenzako wanafanya na yasijibiwe. Maombi yoyote kwa Mungu yeyote huachilia viumbe wa rohoni kuja kuyatekeleza kwa hiyo hawa viumbe waoachiliwa ndio hao wapo Pamoja nawewe na wao.

Watu wengi wanadhania maombi ya watu wasio na Mungu hayana maana hapana yana maana, maana yanawavuta watu wa rohoni kwa upande wao, mtu yeyote anayeomba ujue anafanya shughuli za rohoni na anaongea na roho nazinachiliwa kuna mashetani yanakuja kumsaidia mtu maana amesema maneno kila siku asubuhi. Yeye ndio maana ana akili ambayo haitokani na elimu yake, huyu mtu ukiwa nae kwenye biashara moja na wewe hujafanya ya rohoni huwezi mshinda maana anao walioupande wake na wewe hauna huwezi kufanikiwa. Maisha ni ya rohoni, utokapo kwenda kazini, biashara, shuleni hata shuleni pia, ndio maana kuna mtu akifika shuleni haoni ubao mwalimu akiwa anafundisha anasikia anaimbiwa nyimbo ni vita. Unaweza kuona unafanya biashara na watu wanakupiga vita inaonekana wanamuunganiko mkubwa, mitaji mikubwa kuliko wewe usiogope maana hawawezi kukushinda maana huwezi kumshinda mtu mwenye Mungu kama anajua chakufanya. Hata kama una mtaji kidogo maana atainuka hatua kwa hatua maana Bwana mwenyewe anatoka mbele yake, huwezi mshinda mwanamke aliye na Mungu kwenye ndoa yake maana atamlinda mume wake tazama naumba jambo jipya mwanamke atamlinda mume wake. Huwezi mlinda mume kwakukagua simu yake ila kwa maombi. Bwana asipoulinda mji walindao wanakesha bure. Bwana ni mlinzi ongea nae akulindie wanao, Isaka anataka kumlinda Yakobo anaongea na Mungu alaaniwe mtu yeyote ambaye atamlaani Yakobo halafu Laban akawaza kumlaani akatokewa na Mungu wa Isaka anamwambia aache hayo mambo. Laban akamwambia nina uwezo wa kukulaani ila Mungu wa baba yako amenionya nitakufa.

Kama unapenda kifo kabla ya wakati, vidonda vya tumbo, msongo wa mawazo basi mfuatilie mume wako kila hatua ametoka mkesha anaongea na nani akiwa kanisani, basi utaishi muda mrefu lazima umuamini Mungu anaweza kufanya mambo yote aliyokuahidi. Mungu anaweza kutoka mbele yako akawalinda wanao, mume wako anaweza kulinda Zaidi yako maana niende wapi nijiepushe na uso wa Bwana, wewe huwezi kwenda sehemu zote ila Bwana anaweza.

Hawa watu wametoka kwenda kumkamata Elisha, ishu ni nani yuko nao na sisi nani yupo nasi, akamwambia Gehazi usiogope endelea na kazi zako. Ili vionekane kwa macho ya nyama ilibidi Elisha aombe ili huyu Gehazi aone, Mungu akamfungua macho Gehazi akaona waliowazunguka wamewazunguka ina maana wapo walipamoja na sisi, Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu msaada uonekana wakati wa matesi kwetu Mungu hapendi kumtesa mtu, mpenzi ufanikiwe na kuwa na afya kama vile roho yako ifanikiwavyo kwenye kazi ufanikiwe kwenye biashara masomo ufanikiwe. Haya maisha huwezi kufanikiwa mpaka Mungu akusaidie, huwezi fanikiwa popote kama Mungu hakusaidi na Mungu amekupatia msaada na wako walio pamoja na wewe ni malizie kwa kusema kwanini watu wa Mungu kuna wakati wanashindwa kama ni kweli wako wengi walio rohoni zaidi ya wale walio na adui zako ni kwanini?

Kwa sababu; Kukosa maarifa. Maarifa hayo ni kutokujua kuna walioupande wetu viumbe wa rohoni kile ambacho unachoni. Unakuwa kama Gehazi, Elisha hakuomba ili waje ila aliomba wadhihirishwe ili Gehazi awaone maana alipatwa hofu. Bwana yuko Pamoja na wewe apekupeleka msaada yuko na wewe.  

“Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako”. Hosea 4:6,

Mambo gani inabidi ufanye ili viumbe hao wajue cha kufanya, viumbe wa rohoni wa giza au wa nuru wanafanya kazi mpaka waagizwe. Viumbe wa rohoni wa nuru au wa giza hutenda kazi mtu mwenye mamlaka akiongea maneno. Mashetani hawawezi ingia mtu mpaka watumwe. “Na tazama, mmoja wao waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio. Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga. Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika? Yatatimizwaje basi maandiko, ya kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kujiri?”. Mathayo 26:51-54

Jeshini hawawezi kufanya kazi bila kufuata amri hata kama kuna vita imetoke Nchi ya Kenya hawawezi kujiamria kwenda mpaka waambiwe, hata wewe una wanajeshi wa rohoni lakini hawawezi kufanya kazi mpaka uwaagize.

Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu. Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu. Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima. Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda. Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa. Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga”. Kutoka 17:8-13

Kipi hutokea ukianza kuomba na kipi hutokea usipoomba?

Kuna mambo usipofanya unapoteza vita hata kama walio pamoja na wewe ni wengi. Malaika uliopewa wanafanya kazi ukianza kuomba, Kornelio alikuwa anaomba Malaika akaja, Danieli alikuwa anaomba Malaika akaja. Maelekezo ya Mungu ya dakika mbili yanaweza kubadilisha maisha yako yote. Hutakiwi kushindwa kwenye jambo lolote kwenye maisha kwa sababu walio pamoja na wewe ni wengi. 

Post a Comment

0 Comments