google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

USIOGOPE WALIO PAMOJA NA WEWE NI WENGI KULIKO WALIO NA PAMOJA NA ADUI

UFUFUO NA UZIMA UBUNGO CATHEDRAL.
IBADA YA JUMAPILI 14th MAY 2023.
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGE.
SOMO: USIOGOPE WALIO PAMOJA NA WEWE NI WENGI KULIKO WALIO NA
PAMOJA NA ADUI


Ndio andiko letu la msingi la kuanzia wiki iliyopita. Maneno Elisha anamwambia mtumishi wake Gehazi, wakati wamezungukwa na askari na kundi la washami walio na farasi, magari ya vita Gehazi akasema ole wetu bwana wangu tufanya je ndipo Elisha akamjibu,
“Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao. Elisha akaomba, akasema, Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote”.2 Wafalme 6:16-17. Elisha haongelei watu wanaoonekani wala uwepo wake yeye na Gehazi bali wale waliopamoja nao na anasema ni wengi.

Sisi watu wa Mungu ushindi wetu hutegemea Mungu wetu sio elimu zetu, ushindi wako wakila eneo la Maisha unamtegemea yeye. Mungu ameisha amua ushinde wewe ni mshindi na zaidi ya mshindi, hutakiwi kushindwa kabisa ukianza biashara, ndoa, masomo hutakiwi kushindwa kabisa, maana wako wengi walio pamoja na wewe, na upinzani ambao unakutana nao ni saizi yako, hutakiwi kulalamika au kulaumu au kulia unatakiwa uwakabili ikiwa unafahamu unao walio upande wako na ni wengi kuliko walio upande wawanaokupiga vita. Kuna mambo ambayo usipo yaelewa hata kama una msaada ule msaada haukusaidii. Shetani asingependa uelewe na atakushinda maana huelewi ikiwa kimsingi hatakiwi kukushinda. Imeandikwa wala hatukosi kuzifahamu fikra zake shetani asije akapata kutushinda maana anapata ushindi kwa watu wa Mungu wasipojua baadhi ya vitu.

Hao walio upande wako ni wengi na wana nguvu za kuwashinda walio upande wa adui zako. Unapopigwa vita usiwaone wanaokupiga vita bali uwaone wale waliopamoja nao, iwe ni vita kwenye biashara, masomo, watoto, ndoa usiwaone watu ila ona walio pamoja nao ambao una amri juu yao na una amri juu ya wakubwa wao.

Akawaita wanafunzi wake akawapa amri juu ya pepo wa chafu ili wawatoe na wewe una amri ya kuwatoa, walio pamoja na adui zako ni pepo wachafu na wewe una amri ya kuwatoa. Akawaita wanafunzi akawapa mamlaka ya kukanyaga nguvu zote, nyoka na hakuna cha kuwadhuru na wewe una mamlaka ya kuwa kanyaga, huwezi kumshinda mtu mwenye mamlaka. Mimi huwezi ni shinda hapa nina mamlaka. Nikija kwako mimi sio askofu nakuwa kama raia tu siwezi kukushinda una mamlaka na nikikushinda labda uwe huna maarifa.

Huwezi kushindwa na mtu una mamlaka juu yake. Una mamlaka ya kuwashinda walio pamoja na adui zako wanao wavuvia mawazo kinyume chako, mchawi una amri ya kumshinda maana una amri ya kumshinda boss wao mkubwa ambaye ni shetani una amri ya kukanyanga nguvu zake zote. Jambo lolote ukilianza hutakiwi kushindwa chochote. Na hapana kitu kitakacho wadhuru.

Una mamlaka ya kuwashinda walio pamoja na adui zako maana una mamlaka ya kukanyaga nguvu zao zote, kama Mungu asemacho ni kweli basi unayo mamlaka ya kumkanyaga boss wao wachawi ambaye ni shetani. Ukiamua kumkanyaga una mkanyaga na hapana kitu kitakacho wadhuru ila kuna wakati unapata madhara kwa sababu ni kutokuwa na maarifa.

Kuna mtu hajui wapo walio upande wake na tuna mamlaka ya wale walio upande wa adui, sisi tuna walio upande wetu na wao wanao walio upande wao. Na aliye upande wetu ni mkuu kuliko wote na anayaweza yote na hakuna gumu la kumshinda ndiye aliyeumba mbingu na nchi yuko pamoja nasi ni mkuu kuliko aliye pamoja nao.

Yeye anayesikia neno lakini halitendi ni mpumbavu amesikia ana amri ila amri haitumii kwahiyo anaonewa kwa sababu hatendi na una mamlaka ya kumshambulia shetani, Elisha anaye walio upande wake na wamemzunguka kwasababu walio upande wao wamemwambia. Adui anafahamu mipango yako unako elekea wanafahamu umechumbia kisirisiri na wao wanafahamu na wanamfahamu sana mchumba wako. Kwa Pastor Msimbe umegoma kujaa form ila wao wanafahamu uchumba wako na maongezi yenu yote wanafahamu, wajue wasijue aliyepamoja na wewe ni mkuu kuliko aliyepamoja na adui zako usiogope.

Kuwa na Mungu haimanishi hautapigwa na changamoto hazitakuwepo, kuwa nae ndio hasa itakuletea changamoto, lazima ujue kukabiliana na changamoto zinazokuja kwako na ukiwa na Mungu usidhanie ukichumbiwa kufuata utaratibu wa Mungu ndio hapana upinzani, Yesu anawaambiwa wanafunzi tuvuke kwenda ng`ambo, kuna kitu amevuviwa kufanya ng`ambo mawazo ya kuvuka ng`ambo sio ya wanafunzi wa Yesu ila ni ya Yesu pekee yake ila hapa katikati kuna upinzani na maandiko yanasema wakamchuka vile vile kama alivyo.

Usiseme baada ya kuolewa vita imeibuka unadhania sio mapenzi ya Mungu, au kuanza biashara unakutana na vita, hapo ndipo mahala pekee sasa hayo ndio mapenzi ya Mungu. Maana vita ijapo nitokea hata hapo nitatumaini, Mungu anategemea upigwe vita. Mungu anapenda vita anapenda kuona wanae wanapigana na wale wa upande wapili. Ni kama watoto wanasema mbwa wangu anangata kuliko wako, basi mlete na mbwa wangu wapigane, akishinda mbwa wako unakuwa na heshima, Mungu nae anataka aheshimiwe uwavunje vipande vipande adui zako Mungu nae aseme yule ni mwanangu. Sisi Ufufuo na Uzima hatujawahi kupoteza vita maana baba yetu ni mtu wavita tangu ujana wake.

 

Vita inafundishwa kwa kupigwa vita, una dondoshwa uwanja wa vita , anasema Daudi Bwana ananifundisha mikono yangu vita, lazima Bwana akufundishe vita maana maisha yamejaa vita, vita kwenye kila jambo, vita kwenye biashara ulikuwa unauza udaga ukaona vita ukahamia kwenye biashara ya maharage hata huko kuna vita, ulikuwa kwenye huduma ukaona vita ukaacha huduma ukaingia kwenye  mwanaharakati wa ndoa  hata huko kuna vita, hata ukiacha ndoa kuna vita ya mabinti walioolewa na ambap hawajaolewa kuna vita , pigana vita. Huna pakwenda jipange pigana. Ni vita kote kote Bwana ndio maana anakufundisha vita. Kuwa na Mungu haimanishi hakuna vita ila ndio kuna vita haswa. Kama ni siasa kuna vita, masomo kuna vita. Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo. Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye. Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji. Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia? Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu”. Marko 4:35-39

Vita ipo kwenye chombo ambacho Yesu yupo, kimepigwa na upepo na kimejaa maji. Yesu siku zote alikuwa anayafanya mapenzi ya Mungu asilimia 100 na kila alichofanya Mungu alimuongoza, na wewe unavuka ng`ambo ya huduma, ndoa, biashara kwenye mchakato wakuvuka chombo kinajaa maji, wavuvi wanafahamu chombo kikijaa maji basi kinaanza kuzama, maji yakianza kuingia basi kuna shida.

Walianza safari wakiwa na mwokozi na pengine walikuwa wakisifu lakini ghafla upepo huo. Wakamlalamikia anasinzia kwenye safari kama ile. Nafahamu watu wawili walilala katikati ya upepo, ambao ni Yesu na wapili ni Yona. Yesu aliwakemea maana alitegemea wangekabiliana na usumbufu wa ile hali kuwauliza iko wapi imani yenu,” Akawaambia Mbona mmekuwa waoga? Hamna Imani bado?” Marko 4:40, alitegemea wangeukemea upepo maana ameisha wafundisha na amewapa amri juu ya upepo.

Unaenda mahali umetokea upinzani na Yesu unaye kwenye chombo chako , hiki ndicho Yesu anatarajia ufanye maana una imani, na mwenye Imani amuhamshi Yesu ila ana ukemea upepo. Huu upepo ni shetani amejigeuza kuwa upepo maana ulipo kemewa ukasikia na ukafanya kitu ulichoambiwa ufanye. Ni mtu asiye na mwili yuko nyuma ya upepo, safari ingeishia hapo kwa ajili ya upepo maana alikuwa anaelekea ng`ambo kule kuna mtu ana mapepo, Yesu anaenda kumfungua na shetani anajua Yesu akienda amepoteza mtu ndio maana shetani analeta upepo, ila Mungu ametupa amri.

Ina maana wangekaa kimya wasimuamshe Yesu wangezama wakafa ila Yesu asingekufa , Yohana Yakobo na  Andrea wangeogelea Lawi na mashaka nae na  Yuda angekuwa wakwanza kufa . Ila Yesu anataka kuwa fundisha ikitokea changamoto wanafunzi wake wasemeshaa upepo maana nyuma yake kuna mtu asiye na mwili. Mambo ya kujiliza liza na kupenda kuonewa huruma hapana, jifunze kusemesha mambo.

Sema upepo unaopiga uchumba wangu tulia iwe shari kuu nivuke nikaolewe, acha maneno mengi neno la Kristo lijae moyoni. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu, kwa msaada wa Bwana nafatia jeshi kwa msaada wa Bwana naruka ukuta, kwa Imani walifukuza majeshi na wafukuza, wakimbize hao ndio maneno yakuongea katikati ya changamoto, ukiamka semesha ni biashara semesha ndoa wanakusikia mwenye amri asipoongea mambo hayatokei, mwenye mamlaka huwa anasema. Yale mambo yakujihurumia ni mtu wa mjini mwenye elimu shetani haheshimu elimu yako.

Mambo yakujifanya maombi huhitaji kwasababu una mali una kila kitu, sikiliza shetani atakapokuja kutembelea atafuta vyote una muhitaji Mungu maana shetani alimpoteza billionea ndani ya siku moja. Yasemeshe matukio maana nyuma kuna aliyepamoja nawe. Unapoona mtu ana Sali na kunena kwa lugha unamuona kama hana kitu ana shida ndio maana anasali. Wakiitwa walifanikiwa tutaenda walioenda shule tutaenda na bado tuna mtumikia Mungu. Msaada wa Bwana lazima uongee ndipo atafanya kazi. Unaweza kupambana mwenyewe kwenye vita yako ila umejidekeza. Unayaweza mambo yote katika yeye atutiaye nguvu kila uumbaji una sauti ya kusikia.

Unaweza kuwa unakaa kanisani na umuelewi muhubiri hizo ni nguvu za shetani ana kuwekea upinzani, mambo yote ambayo yanaonekana ni magumu, unataka kuanza biashara kwenda china, anza kuongea waambie waachie njia au mambo kwenye familia ya ndoa mna changamoto umekaa na mkeo unaongea nae muda lakini hakuelewi ukimrekebsha ni mkali mno leo isemeshe ndoa, wapige, vunja haribu uikoe ndoa yako. Kuna nguvu rohoni inakujengea chukia na watu ambao ni wa muhimu sana kwako, inakutenge na watu wako wa muhimu kama Sauli anakuwa na vita na Daudi ambaye anampigia kinanda roho chafu ina muondokea ila anampiga vita kama mimi unakuwa na vita wakati nakuhubiria hayo ni mashetani kama mgerasi, mtu anakuchukia bila sababu ila sio yeye ni mashetani, Mungu akitaka kukusaidia anakutumia mtu. 

Anasema ewe Yerusalemu uwauwae manabii na wale walitumwa kwako mara ngapi nimetaka kukuweka chini yambawa zangu kama kuku awekavyo vifaranga vyake ila hukutaka kwasababu ya hiyo nyumba yako imeachwa mkiwa, ni mtu wa makasiriko, kuchukia maana anayetumwa umemkasirikia huwezi kupokea kutoka kwa Mungu ikiwa aliyetumwa na Mungu ujampokea. Tuombe kwa tusemeshe kemea matukio, biashara, safari, ndoa ambayo haiendi kwa jina la Yesu  na baada ya hapo  unaamuru iweje vile utakavyo. AMEN.

Post a Comment

0 Comments