google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUFUNIKWA KICHAWI (VIFUNIKO VYA KICHAWI)

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 25.02.2024
ASKOFU DKT JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: KUFUNIKWA KICHAWI (VIFUNIKO VYA KICHAWI)

Shetani ni muovu na mabaya yote yanatoka kwake, ukiona unapitia mateso basi jua ni shetani anayeleta hayo mateso. 

Shetani kazi yake ni kufunika, inatokea mtu anakuwa ni mrembo, kasoma, ana kila kitu lakini watu wanamuona tofauti kwa muonekano usiofaa na mara nyingi bila kujijua. Kuna mtu anakutafuta akupe mtaji, akupe fursa lakini anakuona tofauti na vile ulivyo.

“Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari. Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.” Ezekieli 28:13-15.

Kama vile zawadi ikifunikwa vizuri itaonekana vizuri na kumpendeza mtu au ikifunikwa vibaya itaonekana vibaya na kumchukiza mtu, vivyo hivyo shetani anaweza kumfunika mtu aonekane vizuri au vibaya. Ndani ya zawadi kunaweza kukawa na vitu vizuri lakini watu watahukumu hio zawadi kwa mtazamo wa nje kama imefunikwa vizuri au vibaya. Shetani anamafuta ya kufunika hata vile vilivyo vizuri, kwa maana alikuwa malaika afunikaye tangu mbinguni. 

Shetani akikufunika watu wanaotakiwa kukupata hawakupati.

Mtu akiwa amefunikwa kuna mambo unaweza kumtendea yasiyofaa kwake. Tamari alijifunika kama kahaba akalala na mkwewe Yuda, bila Yuda kujua kuwa ni mkwewe. 

Mungu amewaumba watu tofauti tofauti, mtu anavyoonekana kwa uzuri na urembo wa nje inategemeana na yule anayemuangalia na kuvutiwa nae. Uzuri wa kitu upo kwenye macho ya muonaji. Sasa anayetakiwa akuone wewe, anakuona tofauti na vile anavyotakiwa kukuona.

Nini maana ya kufunikwa?

  • Wale watu wanatakiwa kukuona wamewekewa mapepo wanakuona kinyume na ulivyo.
  • Vifuniko ni namna watu wanavyokuhumu hata bila kujua uhalisia wako.
  • Kufunikwa ni kupewa muonekano ambao sio wako ili kila utakachotendewa itatokana na muonekano wako wakati huo.

Mungu huinua watu kupitia watu, mtu anapokuona mara ya kwanza kuna msukumo utafanya avutiwe na wewe au asivutiwe na wewe, iwe urembo, akili na hekima, maneno nk (first impression matters the most). Mungu anatumia watu kuinua watu. Watu wanawekewa macho ambayo yatafanye wakuone kwa namna ya kukusaidia na kukuinua.

Namna mtu anavyoweza kufunikwa.

  • Anayekutazama wewe amewekewa mapepo ili akuone tofauti.
  • Kuna kuwa na pepo katikati ya wewe na anayetakiwa kukuona ili mtazamo wake juu yako uwe ni kinyume na wewe ulivyo.
  • Wanakuwa ndani ya mtu wanaharibu muonekano wake hawaoni asili yake bali tofauti kabisa na alivyo.
  • Wachawi wana namna yao ya kuiba uso wa mtu, moyo wa mtu, akili ya mtu, mikono ya mtu kwa namna ya rohoni. Mungu anapokuleta duniani anaweka nyota ndani yako mikono yako itengeneze fedha, akili ili ikufikishe kwenye uongozi hivyo wachawi wanaiba hio ili kuleta Maisha magumu kwako.

Inaanza hivi kwenye ukoo, familia, siasa, ofisini nk, kuna kuwa na mtu anayeng’aa kuliko wengine, mtu huyo anafanya watu wengine kumuona kama tishio na kupelekea kufunikwa ili asionekana. Inatokea wewe sasa huna Yesu unategemea nguvu zako au urembo wako bila kujua kuna nguvu ya shetani imekusiriba usionekane. Dunia hii imejaa fitina, kile kitendo cha wewe kuchumbiwa, kuolewa, kupata kazi nk, kuna watu hawatapenda, watafanya juu chini kukushusha.

Kuna mtu anakutafuta wewe lakini hakuoni iwe kwenye biashara, kazi, siasa nk. Namna anavyokuona ni tofauti kabisa na vile ulivyo. Macho ya mtu yanaweza kabisa kufungwa asiweze kumuona mtu mwingine.

“Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili. Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia. Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao. Macho yao yakafumbwa wasimtambue.” Luka 24:13-16.

Unahitajika kuvunja vifuniko vya kichawi vilivyomfunika mtu ili aweze kuonekana kama vile anavyotakiwa kuonekana.

"BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA NZIMA YA JUMAPILI"

Post a Comment

0 Comments