google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MUNGU HUTUMIA WATU KUINUA WATU

UFUFUO NA UZIMA UBUNGO CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 11 FEBRUARI 2024
ASKOFU DKT JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: MUNGU HUTUMIA WATU KUINUA WATU

Mungu akitaka kufanya jambo lolote huwa anaanza na mtu, ndio maana Tanzania imeanza na mtu yaani Baba wa Taifa, hivyo ndivyo kwa nchi nyingine kama Kenya. Hata taasisi kubwa duniani kama Bill Gates Foundation na Mwalimu Nyerere Foundation zinaanza na mtu.

Watu ni wa muhimu kuliko vitu, vitu vyote vimefichwa ndani ya watu. Kesho imeficha matukio mengi usiyotarijia hata yule anayeonekana dhaifu ndani yake anaweza kuwa amebeba kitu kikubwa iwe taasisi, kampuni, biashara, huduma nk. 

Mungu huinua watu kupitia watu. Mungu akiamua kufanya jambo hutumia watu, hata kupitia watu wale wanaoonekana wa kawaida na dhaifu. Kupitia watu Mungu huinua watu, Hata Yohana alikwenda mbele za Yesu ambaye ni Mungu ili aitengeneze njia yake.

“Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya, Tazama, Namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako. Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake. Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi. Wakamwendea nchi yote ya Uyahudi, nao wa Yerusalemu wote, wakabatizwa katika mto wa Yordani, wakiziungama dhambi zao. Na Yohana alikuwa amevaa singa za ngamia na mshipi wa ngozi kiunoni mwake, akala nzige na asali ya mwitu. Akahubiri akisema, Yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza gidamu ya viatu vyake. Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.” Marko 1:1-8.

Hakuna mtu ni zaidi na hakuna mtu ambaye si kitu bali kila mtu ni sahihi kwenye eneo alilotumwa. Wewe umetumwa na Mungu kufanya jambo la kiuchumi, jambo la kisiasa nk. unapokuwa kwenye eneo hilo Mungu anafanya kazi kupitia wewe, mikono yake inakuwa yako, akili yake inakuwa yako, jambo lolote unalotenda inakuwa ni Mungu anafanya.

Hakuna siku Mungu atashuka kukusaidia au kukubeba, Mungu tayari yupo ndani yako, wewe fuata ile shauku yako na mtu ambaye Mungu tayari amemuweka kwa ajili yako.

Kutoka hapo ulipo unahitaji mtu akutaje, Sio wenye mbio ndio washindae, sio wenye bidii ndio wafanikiwao nk. Wakati na bahati huwapata wote. 

“Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.” Mhubiri 9:11.

Lazima awepo mtu wa kukutaja mbele za wakuu ili uinuke kutoka pale ulipo. Yusufu alifanya jambo ambalo lilifanya atajwe mbele ya Farao. Ingewezekana Mungu amtoa Yusufu kutoka gerezani mpaka kuwa waziri mkuu, lakini ilibidi amtumie mtu kumuinua Yusufu.

“Basi mkuu wa wanyweshaji akamwambia Farao akisema, Nayakumbuka makosa yangu leo. Farao aliwakasirikia watumwa wake, akanitia nifungwe nyumbani mwa mkuu wa askari, mimi na mkuu wa waokaji. Tukaota ndoto usiku mmoja, mimi na yeye; kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake tukaota. Na huko pamoja nasi palikuwa na kijana; Mwebrania, mtumishi wa mkuu wa askari, tukamhadithia, naye akatufasiria ndoto zetu; akamfasiria kila mtu kama ilivyokuwa ndoto yake. Ikawa, kama vile alivyotufasiria ndivyo ilivyotokea; mimi nalirudishwa katika kazi yangu, na yeye alitundikwa.” Mwanzo 41:9-13.

Janga kubwa ni kukosa mtu wa kukutaja hata kama umesoma sana, usipigane kila vita na kila mtu, chagua vita nyingine kuacha zikupite. Ukitoka kutoka pahali pa chini kwenda juu, anainua mtu wa kukutaja mahari, ishi na watu vizuri ili awepo mtu wa kukuinua.

Utimilifu wa mambo aliyokupangia Mungu kwenye maisha yako, unatimia pale mtu anapokutaja kwa mtu mkuu. MUNGU ANAANZA NA WATU.

"BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA NZIMA YA JUMAPILI"

Post a Comment

0 Comments