UFUFUO
NA UZIMA UBUNGO CATHEDRAL
IBADA
YA JUMAPILI 18 FEBRUARI 2024
ASKOFU
DKT JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: MASHETANI
KATIKA UZAO WA WANADAMU
“Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.” 1 Yohana 3:10.
Biblia inasema watoto wa Ibilisi ni bayana vivyo hivyo na watoto wa Mungu ni dhahiri. Yesu anasema ukimuona Baba umemuona mwana, kama mtu ni mtoto wa Mungu umemuona Mungu, kama mtu ni mtoto wa Ibilisi umemuona Ibilisi. Ukimuona Baba na mtoto ni wale wale. Yesu anawaita wana wa Ibilisi kama alivyo baba yao.
“Ninyi
ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye
alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli
ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni
mwongo, na baba wa huo.” Yohana 8:44.
Neno
Baba maana yake ni asili, mwanzilishi na chanzo, kama Baba alivyo wale
anaowazaa wanakuwa kama yeye. Unaweza kukutana na mtu anashindana na wewe
kwenye maisha kumbe ni mwana wa Ibilisi.
Yesu
anaonyesha tena namna wana na baba ni wamoja; Watu wengine waliwaona watu
lakini Yesu aliwaona siyo watu.
“Enyi
nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?” Mathayo 23:33.
Hata
leo kuna watu wanaoonekana watu lakini asili yao sio ile unayoijua wewe.
“Hata
alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake,
aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira
itakayokuja?” Mathayo 3:7.
Tunajifunza
kuwa wanaonekana watu lakini kumbe ni mashetani. Mtu kabisa anaonekana mtu
kabisa ila kuna uwezekano akawa wa uzao wa shetani, ndiyo maana Yesu anawaita
mashetani japo wanaonekana wanadamu.
“Na kama vile ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo.” Danieli 2:43.
Kila mtu unayemtazama kuna asili anayokuwa katokea. Ibrahimu walipokea wageni ambao walionekana ni wanadamu kabisa lakini hawakuwa wanadamu wa kawaida.
“BWANA
akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa
hema yake mchana wakati wa hari. Akainua macho yake akaona, na tazama,
watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka
mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi, akasema, Bwana wangu, kama nimeona
fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako. Na yaletwe
basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu. Nami
nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia
mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema. Basi Ibrahimu akaenda hima
hemani kwa Sara, akasema, Himiza vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye
mikate. Ibrahimu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng’ombe
aliye laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akahimiza kuiandaa. Akatwaa
siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandikia mbele yao, akasimama karibu
nao chini ya mti, nao wakala. Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo
hemani. Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na
tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema
iliyokuwapo nyuma yake. Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri
wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake. Kwa hiyo
Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana
wangu mzee? BWANA akamwambia Ibrahimu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli
nitazaa mwana, nami ni mzee? Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda
BWANA? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata
mwana wa kiume. Akakana Sara, akisema, Sikucheka, maana aliogopa. Naye
akasema, Sivyo, umecheka. Mwanzo 18:1-15.
Kila mtu alipoumbwa Mungu kamuita kuwa mtu fulani, awe bora kwenye kitu fulani iwe siasa, biashara, elimu nk. Wana wa mashetani wanaona kile kilichokuwa ndani yako wanakuja ili kupindisha hatima yako. Unahitaji macho kuona maana anakuja kama mtu wa kawaida. Wana wa Mungu wanavaa miili vivyo hivyo wana wa Ibilisi wanavaa miili.
“Ikawa
hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia,
na tazama, mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi
mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au
upande wa adui zetu? Akasema, La, lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la
BWANA. Yoshua akapomoka kiusouso hata nchi, naye akasujudu, akamwuliza, Bwana
wangu aniambia nini mimi mtumishi wake? Huyo amiri wa jeshi la BWANA akamwambia
Yoshua, Vua viatu vyako miguuni mwako; kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni
patakatifu. Yoshua akafanya vivyo.” Yoshua 5:13-15.
Wasio watu wana
makundi matatu;
- Mtoto wa dawa - Mama aliyeolewa aliyekaa muda bila mtoto anaenda kutafuta mtoto kwa mganga ambaye anakuja kuzaliwa mtoto kabisa. Watoto wa dawa wanakuwa na shida kweli maana wamezaliwa kutoka kwenye nguvu za giza. Mwili ni wa mtu lakini ndani ni kitu tofauti kabisa. Mtoto wa dawa ametengwa wakfu tangu tumboni mwa mama yake kwa ajili ya makusudi fulani ya uharibifu.
- Shetani (roho) anavaa mwili - Shetani ambaye ni roho kabisa anavaa mwili na kufanya kazi za uharibifu duniani.
- Mapenzi ya ndotoni (Sexual dreams) – Mtu unapolala unaota unafanya mapenzi ndoto mpaka wakati mwingine mpaka unazaa mtoto, anakuwa jini amevaa sura ya mnyama au mtu unayemjua. Mwanadamu anaweza kulazwa usingizi na jambo likaendelea. Kama Mariamu alivyotunga mimba kwa uweza wa roho mtakatifu, kuna namna ya kichawi ya kufanya watu kutunga mimba.
Ulimwengu wa mwili miaka hii tunayoishi na tunayoelekea umegeuka kuwa uwanja wa vita baina ya ufalme wa Mungu na ufalme wa Ibilisi wote wakitenda kazi ndani ya watu, inahitaji macho kujua ni nani unayejihusisha nae iwe kwenye ndoa, kazi, biashara au siasa.
0 Comments