UFUFUO
NA UZIMA CATHEDRAL
JUMAPILI
31 MACHI 2024
ASKOFU
DKT JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: KALENDA ZA
KICHAWI
Kuna ulimwengu wa aina mbili ulimwengu wa kiroho na ulimwengu wa kimwili chochote kinacho tokea ulimwengu wa mwili kimeanzia rohoni. Mambo hayajitengenezi yenyewe yanatengenezwa katika ulimwengu usioonekana.
Ili mambo yatokee kuna
kalenda ya kiroho na jambo lolote ili likupate lazima liendane na kalenda ya
rohoni. Kanuni za kidunia zina kalenda, vivyo hivyo matukio yote yapo kwenye kalenda
ya kiroho yanatimia katika ulimwengu wa mwili.
Kila maisha yana adui
wake na wanakufuatilia kila mahali na hao ndio wanao tengeneza kalenda za
kichawi zenye matukio mbalimbali.
Kuna kalenda za
kishetani ambazo zimejaa matukio ya kishetani ili kupindua kal enda ya ki Mungu
yenye matukio ya ki Mungu yalio pangwa na Mungu kukupata wewe. Yanayo kupata
mwilini ni matokeo ya yale yalio pangwa katika ulimwengu wa roho.
“Baada ya hayo mfalme
Ahasuero alimwongezea cheo Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, akampandisha,
akamwekea kiti chake juu ya maakida wote waliokuwapo pamoja naye. Nao watumishi
wote wa mfalme, walioketi mlangoni pa mfalme, wakainama na kumsujudia Hamani,
maana ndivyo alivyoamuru mfalme kwa habari zake. Bali Mordekai hakuinama, wala
kumsujudia. Basi watumishi wa mfalme walioketi mlangoni pa mfalme wakamwambia
Mordekai, Mbona wewe waihalifu amri ya mfalme? Ikawa, waliposema naye kila siku
asiwasikilize, wakamwarifu Hamani, ili kuona kama mambo yake Mordekai
yatasimama; maana alikuwa amewaambia ya kuwa yeye ni Myahudi. Hata Hamani
alipoona ya kwamba Mordekai hainami wala kumsujudia, alighadhibika sana. Akaona
si shani kumtia mikono Mordekai peke yake; maana wamemjulisha kabila yake
Mordekai; kwa hiyo Hamani alitaka kuwaangamiza Wayahudi wote waliokuwa wakikaa
katika ufalme wote mzima wa Ahasuero, yaani, watu wake Mordekai. Basi
mwezi wa kwanza, ndio mwezi wa Nisani, mwaka wa kumi na mbili wa mfalme
Ahasuero, wakapiga Puri, yaanikura, mbele yake Hamani; siku kwa siku, na mwezi
kwa mwezi, hata mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari.” Esta 3.1-7.
Mambo yanampata mtu pale ambapo saa, siku na mwezi wa hilo jambo lililopangwa kutimia kwenye kalenda husika hutimia. Kalenda ndio inayoamua mambo gani yakupate kwa saa gani.
Kazi kubwa ya kishetani
ili itimie inahitaji tarehe ya kutimia kwa ilo jambo ambayo ndio siku ya uovu.
Siku ya uovu huwezi kuikwepa kwa kukodi gari, au kwa njia za kimwili, litatimia
tu. Siku ya uovu inabadilika kwa kuomba, kilicho tengenezwa kiroho huwezi kukitengua
kimwili bali kwa njia za kiroho tu.
“Basi Mordeikai
alipojua mambo yote yaliyofanyika, alizirarua nguo zake, akajivika gunia pamoja
na majivu, akatoka hata kufika katikati ya mji, akalia kwa sauti kuu ya
uchungu. Pia akafika hata mbele ya mlango wa
mfalme; maana hakuna awezaye kuingia ndani ya mlango wa mfalme hali amevaa
magunia. Na katika kila jimbo, ambako amri ya mfalme na mbiu yake imewasili,
palikuwako msiba mkuu kwa Wayahudi, na kufunga, na kulia, na kuomboleza; hata
na wengi wakalala juu ya gunia na majivu.” Esta 4.1-3.
0 Comments