google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ADUI WA NJIANI

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
JUMAPILI 28 APRIL 2024
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGE
SOMO: ADUI WA NJIANI
Kila mtu ana kusudi ambalo Mungu amekusudia katika maisha yake. Ili kufikia katika kusudi hili ipo njia lazima upite. Njia hiyo inaweza kuwa ni MTU. Yesu anasema mimi ndimi njia, kweli na uzima hivyo njia inaweza ikawa ni mtu. Lipo kusudi Mungu amekuwekea kwenye maisha yako na yupo mtu ambaye Mungu amemuandaa ili awe njia yako ya kufika katika kusudi lako.

Mtu aliye njia ni mkuu kuliko watu wote, ndio maana Yesu alipomuona Yohana akasema huyu ni mkuu kuliko wote. Kuna wakati unapoteza mtu au unagombana na mtu lakini kumbe sio mtu ni NJIA. Kuwa makini sana unavyoongea na watu, unavyowatendea watu maana anaweza kuwa NJIA yako kufikia kusudi lako.

Mungu anaweza kuruhusu mabaya yakupate ili akuvute kwenye njia yako. Katika kutafuta tafuta suluhisho la tatizo lako, Mungu anaweza kukuvuta akupeleke kwa mtu ambaye ndiye njia yako. Unaweza ukakuta unafika kanisani unapata mtu ambaye atakuvusha kumbe ni Mungu amekuvuta na kukuleta kwa yule aliyemuandaa awe njia yako.

Kuna mtu kiwango alichofikia hakuombei upate kitu fulani, anatamka tu na wewe unapata. Mungu ana vitu lakini ili akupe kuna mtu anatakiwa kumwambia Mungu akupe. Mfano: Anaweza kuongea maneno kama “Hautakufa kabla ya wakati wako” yaje maogonjwa, zije ajali, yaje mitego ya adui HUWEZI KUFA MPAKA WAKATI WAKO UFIKE. Hii ni kwasababu yupo mtu ambaye ana mamlaka na nguvu aliyetamka hivo. 

"Ilikuwa hapo Farao alipokwisha kuwaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije wakaghairi watu hawa hapo watakapokutana na vita, na kurudi Misri; lakini Mungu akawazungusha hao watu kwa njia ya bara kando ya Bahari ya Shamu; wana wa Israeli wakakwea kutoka nchi ya Misri hali wamevaa silaha." Kutoka 13:17-18

"Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu. Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu. Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima. Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda. Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa. Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga. BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu. Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi; akasema, BWANA ameapa; BWANA atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi." Kutoka 17:8-16.

Post a Comment

0 Comments