Kabla hujazaliwa Mungu alishaamua utakuwa nani. Ndoto ni kiashiria ya utakuwa nani lakini njia ya kufikia hapo Mungu hakuonyeshi na anafanya hivyo ili usiogope na kuacha kufuatilia hatima yako.
“Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa.
Naye BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.” Mwanzo 25:21
Mungu huwa anakupeleka sehemu kwanza kabla hujawaongoza wengine sehemu hio. Huwezi kuongoza watu sehemu ambayo hujafika. Mfano kwenye biblia, Musa alikimbilia Jangwani. Musa huyo huyo akawaongoza watu jangwani lakini hakuingia nchi ya ahadi maana hakuwahi kufika. Lakini wapelelezi waliotoa ripoti nzuri ya nchi hio ndio waliyowaongoza wana wa Israeli kufika nchi ya ahadi.
Kwa nini Yesu ndio njia ya kwenda Mbinguni, Ni kwa sababu yeye
alishawahi kufika Mbinguni.
Kuna matukio yanakupata wewe ni fundisho unalolipitia ili uweze kumsaidia mtu
“Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza BWANA. BWANA akamwambia, Mataifa mawili yako tumboni mwako, Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako. Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili, Na mkubwa atamtumikia mdogo.” Mwanzo 25:22-23
"Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake," Wagalatia 1:15
"Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado." Zaburi 139:16
Kipo kitabu kilichoandikwa kuhusu wewe na huwezi kufa mpaka yote
yatimie, pia hakuna atakayebadilisha yaliyoandikwa. Ikishaandikwa imeandikwa.
Mungu ana kitabu chake cha hatima zetu. Watu wanaweza kuwa na uadui na wewe sio
kwa sababu umekosea bali ni kwa sababu ya hatima yako njema. Mfano:Yusufu aliota
ndoto kwamba kaka zake wangemuinamia wakaamua kumuua.
Mungu akikupenda anakuunganisha na watu. Hao wanakuchukia
kwa sababu ya hatima yako, anaweza kukuchongea njia nyingine ili usifike kwenye
hatima yako. Lakini kama Bwana aishivyo, kile ulichoandikiwa kitafanikiwa.
0 Comments