UFUFUO
NA UZIMA CATHEDRAL
ASKOFU
BARAKA THOMAS TEGGE
SOMO: KIJANA NA NJIA ZAKE
MKESHA WA ALHAMISI 12.04.2024
Umri wa ujana ni umri ambao ni vigumu kutii mamlaka. Lakini
ili uweze kufanikiwa lazima uweze kutii mamlaka. Mawazo uliyonayo ni ya muhimu
sana maana yana baini njia utakayoiendea. Kwa mfano; kama kijana unaweza kuamua kutokufanya
tendo la ndoa kabla ya ndoa na ukafanikiwa maana hio ndio njia uliyoichagua. Hivyo namna yako ya kuwaza inabaini sana njia utakayoiendea.
Namna ya kusafisha njia yako kama Kijana;
- Kutii mamlaka.
Mawazo yako yanabaini njia utakapita. Lakini ukiwa chini ya mamlaka hauendeshi maisha yako kwa mawazo yako bali mamlaka unayoifuata na kuitii inaweza kukusaidia kufanikiwa na kupita njia iliyosahihi. Mtu mwenye mamlaka anaweza kukusaidia kwa maneno ambayo atakuambia na itaathiri mawazo yako. Kuna wakati mtu mwenye mamlaka anaweza kuongea vitu usivyovielewa au usivyovipenda ila ukitii maneno hayo utakuwa katika njia sahihi.
- Maombi.
Mungu ana namna mbili ya kuwaongoza watu;
- Mungu anakuongoza kupitia mtu aliyekupa.
- Mungu anakuongioza kupitia Mungu aliye ndani yako.
"Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho
langu likikutazama."
"Watakuja kwa kulia, na kwa maombi nitawaongoza; nitawaendesha penye
mito ya maji, katika njia iliyonyoka; katika njia hiyo hawatajikwaa; maana mimi
ni baba wa Israeli, na Efraimu ni mzaliwa wa kwanza wangu."
Maombi yana uwezo wa kubadili mawazo yako ili yakakubaliane na mawazo ya Mungu.
0 Comments