google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SHERIA ZA UCHUMBA

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
ALHAMISI 11 APRIL 2024
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGE
SOMO: SHERIA ZA UCHUMBA

Swala la kuoa au kuolewa ni lazima upate mtu wa kukufundisha na wewe uwe tayari kujifunza. Hili jambo ni muhimu sana ili wote wawili kwenye uchumba kuwa salama. Kila mtu ana shauku ya kuoa au kuolewa siku moja hivyo ili kufanikiwa katika ndoa yako lazima upate mtu wa kukufundisha katika njia sahihi. Kuna sheria za uchumba lazima uzijue, ili uweze kudumu katika  uchumba na kuwa na ndoa imara.

Watu wengi leo maisha wanayo ya ishi ni matokeo ya ndoa zilizo haribika. Ndoa nyingi zimeharibika kwasababu ya ukosefu wa maarifa ya sheria za uchumba ambazo zikifuatwa zinaleta matokeo ya ndoa imara. Ni muhimu sana kuwa na mtu ambaye anaweza kukufundisha sheria za uchumba ili kuepeka kuwa na matatizo yanayoweza kuepukika katika ndoa. Kujifunza sheria hizo na kutozifuata zitaleta madhara mbeleni na kuishia katika majuto. 

Mungu anataka kwanza ulelewe ili uweze kuja kuwalea watoto wako baadae. Tambua kwamba huwezi kuwalea watoto wako katika njia zilizo sawa kama hujawahi kulelewa. Kuna tabia mbaya ulizo nazo leo kwa sababu tu hukupata malezi bora kutoka kwa walezi wako. Ndio maana ni muhimu sana kuwa na mtu ambaye anaweza kukufundisha katika njia sahihi na ni lazima ukubali kulelewa.  Leo tunamuona baba yetu yuko imara sana na familia yake yote ya kimwili na ya kiroho kwasababu baba yetu alikubali kulelewa na leo tunajivunia matunda ya malezi yake.

Zifuatazo ni sheria za uchumba ambazo kama ukizifuata utafanikiwa katika uchumba wako na kuwa na ndoa imara;

1. Ukitaka kuchumbia hakikisha umeshawishika kabisa.

Ni vyema sana kama unataka kumchumbia mtu uwe na uhakika kabisa huyo ndiye utakaemuoa. Hii ni kumaanisha kwamba hata akiwa na mapungufu yoyote una uwezo wa kuendelea kuwa naye. Ukiwa unamchumbia mtu au kuchumbiwa na mtu lazima uwe na msukumo (Conviction) ambayo inauwezo wa kuzidi udhaifu. Utakapo kutana na udhaifu wowote kwa mwenzako, ule msukumo wa kumchumbia inazidi udhaifu huo. Inakuwezesha kukaa na kuongea nae vizuri ili muendelee katika safari ya uchumba mpaka kufikia ndoa imara. Msukumo una uwezo wa kukufanya kutowasikiliza watu watakapo ongea mabaya kuhusu mwenza wako.

2. Usianzishe mahusiano ya uchumba bila kumhusisha mtu mwenye mamlaka ya juu kuliko wewe.

Ni muhimu sana kuwa na mtu mwenye mamlaka ya juu kuliko wewe ambaye anajua kuhusu mahusiano yako ili wote muwe salama. Utakapoanzisha mahusiano ya mtu taarifa hizo zifike kwa mtu mwenye mamlaka haraka iwezekanavyo ili kuepesha makosa kufanyika. 

Sababu ya kuhusisha mamlaka

a.) Ili pawe na shahidi

Ni vizuri sana pawe na shahidi wakati wa uchumba. Hii inafanya wote muwe salama. Mara nyingi katika mahusiano mabinti ndio wanakuwa ni wahanga wa kuumizwa katika mahusiano. Hivyo pakiwa na shahidi inakuwa rahisi wote kuwajibika katika mahusiano yao. Kuchumbiana katika siri inaleta madhara makubwa sana hasa kwa mabinti maana kama mahusiano hayo yakivunjika inakuwa ngumu kupata msaada wowote maana hamna mtu aliyejua kuhusu mahusiano hayo. 

"BONYEZA HAPA KUANGALIA SEMINA NZIMA YA MAHUSIANO"

Post a Comment

0 Comments