google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SHERIA ZA UCHUMBA

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
ALHAMIS 19 APRIL 2024
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGE
SOMO SHERIA ZA UCHUMBA

Sababu ya kuhusisha mamlaka

  1.  1. Ili pawe na shahidi
  2.  2. Ili pawe na mtu atakaye walea (malezi)

Ni vizuri kuwa na mtu ambaye mnaweza kumwendea kama kuna jambo linawatatiza, kumshtaki, kujifunza. Ni muhimu kuwa na mtu huyo na mtu huyo awe na mamlaka. Hata Suleiman aliyekuwa mwenye hekima sana alikuwa ana watu wanaomshauri. Hivyo ni vyema kuwa na mtu ambaye atawashauri katika mambo msiyoyajua. Kutafuta ushauri kwa watu wa rika lako (Yaani vijana) utakupoteza kwasababu yeye uwezo wake wakufikiri ni sawa sawa na wewe. Mamlaka inaweza kushauri vizuri.

Kuna wakati katika mahusiano mnafarakana  au kupishana kidogo kiasi kwamba unawaza hapo ndio mwisho wa mahusiano lakini akiwepo mtu ambaye ana mamlaka anaweza kuwasimamia na kuwaelekeze namna kuendelea kuishi kwenye mahusiano yenu.

3. Usikutane na mchumba wako sehemu ya faragha mkiwa pekee yenu

Mfano wa sehemu za  faragha: nyumbani kwa mtu, sehemu ya giza, ni sehemu ambayo haina watu. Ni vizuri wachumba kukutana na kuongea lakini iwe sehemu ambayo ina watu. Sio sawa kumfuata mchumba wako nyumbani kwake au kwao. Ukikutana na mtu katika mazingira kama hayo yanaweza kukufanya utende dhambi hata kama hukukusudia. Biblia inasema uikimbie zinaa, sio kuikemea. Msikubali pia kuamsha hisia za mapenzi ukijuwa kabisa hauwezi kuyatimiza.

Uthamani wa mwanamke hupungua pale anapofanyiwa vitu mara kwa mara.

1.      4. Epuka kwa gharama zote kufanya sex kabla ya ndoa

1.     5. Usiwe muongo na kujifanya vile usivyo

Ishi maisha halisi maana kipindi cha uchumba ni kipindi cha kufahamiana. Usifanye mambo ili tu umpendeze mchumba wako. Kuwa wewe mwenyewe! Ni vibaya sana kudanganya wakati wa mahusiano. Wakati wa uchumba ni wakati wa kujuana na katika kujuana lazima kusema ukweli. Mf: Kama una mtoto ni vizuri kusema mapema. Kama kweli mtu amedhamiria kukuoa hawezi kukuhukumu kwa makosa yako ya nyuma. 

Ili uweze kujua namna ya kuenenda katika mahusiano inatakiwa uzijue sheria za uchumba


Post a Comment

0 Comments