UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
ALHAMIS 26 APRIL 2024
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGE
SOMO: KANUNI NA SHERIA ZA UCHUMBA
Dating system ni namna ya kidunia kufikia jambo la ki-Mungu (Ndoa). Kuna mambo katika Maisha utayapata kwa kufuata kanuni. Ukiomba sana bila kufuata kanuni huwezi kupata unachokitaka.
Sheria zisipofuatwa hata kama hukupanga kufanya dhambi utajikuta umetenda dhambi hio.
Sheria
za uchumba lazima elimu ya msingi ifuatwe, usipofuata elimu ya msingi unaharibu
uchumba, na huwezi kabisa kuwa na ndoa imara, nyumba isipokuwa na msingi imara
inatengeneza ufa na baadae inavunjika unapata hasara ya kujenga ukuta ndoa ni
kama nyumba, ili usijenge ukuta jenga msingi imara kwenye mahusiano ya uchumba
fuata sheria za uchumba.
Kuna
baadhi ya mambo lazima umfanyie Mchungaji wako ili aweze kukutamkia maneno ya
baraka, kinacho angaliwa sio ukubwa wala
uthamani wa kitu bali ni moyo wa upendo, inabidi ufanye kitu ili uwe sehemu ya maisha
ya Mchungaji wako kiongozi, fanya kitu chochote.
Ukisha
mpenda binti mmoja ukamtamkia maneno hakikisha una maanisha ukishindwa kuwa na
msimamo hata ukija kuoa huwezi kabisa kutulia kwenye ndoa, maana hukuwa
na msimamo tangu mwanzo, ulishindwa kuzitiisha hisia zako tangu mwanzo. Ukishaanza mahusiano na mtu usiangalie tena mabinti wengine maana mabinti wazuri wataendelea kuwepo
Katika
mahusiano ya uchumba kununiana ni jambo la kawaida sana, tegemea kutofautiana na
kupatana sana, haya ni mambo ya kawaida sana katika Maisha ya mahusiano ya
uchumba, katika ndoa na katika Maisha ya
kawaida huwa tunatofautiana na wenzetu lakini haiwi milele bali huwa
tunaelewana na kupatana na Maisha yanaendelea. Jiandae kuwa mchumba wako
atakukwaza na hutakiwi wala huruhusiwi kabisa kumchukia ili
kuepusha kuharibu mahusiano kwa sababu ambazo sio za lazima. Hii itakusaidia
sana, ukiwa na mchumba pakatokea na mgogoro jaribu kusuluhisha au nenda kwa mamlaka husika ili mpate suluhu. Usiruhusu watu
wakaja kukutuliza maana watu wanapokuja kukutuliza wanaweza wakaondoka na moyo
wako, linda sana moyo wako usiruhusu moyo wako kupokea maneno kutoka kwa kila
mtu maana sio kila mtu atakuwa na nia njema na mahusiano ya uchumba wako.
8. Usianze kumhudumia Binti kabla ya kumuoa
Usianze
kumhudumia mchumba mahitaji yake binafsi kabla hajawa mke wako ili usije
ukavunjika moyo. Kijana usimsomeshe binti, usimlipie kodi, binti usijirahisishe
kwa vijana kama kwenda kupika kufua kudeki kutandika kupiga pasi hairuhusiwi
kabisa haitakiwi ni marufuku.
Binti hairuhusiwi kwenda kwa kijana kumpikia wakati wa uchumba, kumfulia nguo zake au kufanya usafi nyumbani kwake.
10.
Msianze miradi ya kifedha pamoja
Kuna
mambo mkianza pamoja ama ni biashara au kujenga baadae mkija kuachana lazima
mmoja ataumia na hili haliepukiki ili kuepusha ni vizuri sana kuepuka kuwekeza
pamoja.
Ni vizuri sana kuambiana ukweli katika yale mambo ya msingi ili muweze kushughulikia misingi mibovu katika familia. Mfano; kama mama yako aliolewa akaachika hapo unakuwa tayari umeshapata msingi mbovu wa kuharibu msingi wa ndoa, kama baba yako alifariki katika umri mdogo ni vizuri kusema ili muweze kuharibu vifo vya ghafla katika ndoa yenu. Kwa kufanya hivi itasaidia sana kuwa na ndoa imara sana maana kila misingi mibovu inakuwa imeshaharibika kabisa na inawezekana kabisa kuanzia kwenu familia ikawa imara sana. Ujifunze kuona mambo kuanzia kwenye chanzo chake ili uweze kulitatua tatizo na liishe kabisa.
Kuna mambo mtu wa
Mungu akifanya anazuia muendelezo wa matukio mabaya katika
familia au katika jamii inayomzunguka, watu wengine wanaoa wanaacha
kumbe ni jambo la rohoni, likishughulikiwa linaisha kabisa na familia yenu inakuwa imara kabisa, usishindane na matatizo katika familia shindana na vyanzo vya
matizo, katika familia ili tatizo liishe kabisa ng’oa mizizi ya tatizo usikate
matawi ya mti, ng’oa mizizi matawi hayawezi kustawi tena, tatizo ni kama matawi
chanzo cha tatizo ni sawa na mizizi ya mti.
0 Comments