google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHAPA NA MIHURI YA KICHAWI

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 14.04.2024
ASKOFU DKT JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: CHAPA NA MIHURI YA KICHAWI

Chapa ni muhuri, ni alama ya tofauti imewekwa mahali ili kufanya barua kwamba ni halali, kwamba ni ni kitu cha mtu fulani.

"Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu." Wagalatia 6:17

Chapa inamfanya mtu ajulikane ni wa nani, ziko alama ambazo mtu anakuwa nazo ambazo zinaashiria kitu fulani ama kwenye mwili, ama kwenye nyama. Hio sio sawa maana Mungu amesema usiweke alama kwenye nyama ya mwili wako. 

"Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;" Ufunuo 13:15-16

Iko chapa ambayo mtu akiwekwa inatoka kwa shetani na hiyo chapa akiwekwa inamletea matatizo fulani fulani. Lakini pia ipo chapa inayotoka kwa Mungu, mara tu unapookoka unapata muhuri wa Yesu, sio dini wala sio dhebu, dhehebu ni mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu, wokovu ni mpango wa Mungu kumtafuta wanadamu.

"awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo. 'Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake." Ufunuo 14:9-11

Kumbe kuna chapa ukiipokea hamna raha mchana wala usiku, wachawi ni watumishi wa shetani

"Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu." Ufunuo 20:4 

Kuna watu huwa wanazaliwa na alama kwenye mwili wao, mwingine ana alama mgongoni au ubavuni, mwingine unakuta ana vidole sita kwenye mikono au kwenye miguu, hakuna jambo ambalo halina maana, kila unaloliona lina maana.

Neno chapa kwa watu wa Mungu ni Roho Mtakatifu, unawekwa alama baada ya kuokoka, maana yake ni kwamba wewe ni wa Bwana, shetani naye ana watu wake anawatia alama, wachawi kwa wachawi wakionana wanafahamiana kwa sababu wana alama, hivi unajua kwamba wachawi hawaamini kwamba ulicho nacho wewe ni nguvu za Mungu, wanaamini kwamba ni uchawi wa ngazi za juu, kila unayemuona yuko kwenye maisha haya kuna nguvu ya kiroho anayoitegemea, ili uweze kufanikiwa unatakiwa kuishi maisha ya kiroho, wale wanaomcha Mungu wana alama ya ulinzi wamepewa na Mungu, washindane na wewe, wakuwinde hawawezi kufanikiwa kwa sababu Mungu anakulinda.

Kuna watu wamewekewa alama ya kushindwa ndio maana unabadilisha mji lakini maisha yako pale pale kumbe ni kwa sababu kuna alama ya kushindwa, alama ya ubaya, alama ya kuaibika, alama ya talaka, ukimuona mama amezaa nje ya ndoa halafu akaolewa ujue mtoto atakayemzaa naye atazaa nje ya ndoa halafu ndio ataolewa, mwingine anachumbiwa halafu naachwa, mtoto wake naye anachumbiwa halafu anaachwa chungulia maisha yako, ukiona baba maisha anayoishi usipokuwa makini utaishi maisha kama anayoishi baba yako, Ibrahim ni baba wa Imani alikuwa na mke wake Sarah, hawakuwa na mtoto kwa sababu mke wake alikuwa ni tasa, akazaa  mtoto anaitwa Isaka, Isaka nae akamuoa Rebeka, Rebeka nae alikuwa hazai, Yakobo nae akamuoa Rachel, Rachel nae alikuwa hazai, ni kwa sababu ya nasaba ya kwenye familia, kuna watu wengine kumcha Mungu kwako kunatoka kwa bibi  yako, angalia maisha ya mama yako na ya baba yako na ujiangalie na wewe ulivyo. 

Ibrahim alikuwa na wasi wasi kwa habari ya Sarah kwa sababu ni mzuri, akamwambia wadanganye kuwa ni dada yake, baada ya miaka mingi Isaka alivyozaliwa naye akaenda Misri, akamwambia Rebeka tufika sema mimi na wewe ni mtu na dada yake, baadae anazaliwa Yakobo ndio akawa mafia mpaka jina lake lilikuwa lina utata ikalazimu kubadilishwa aitwe Israel, unaweza kuwa kuna alama kwenye ukoo wenu alama haiko kwenye mwili iko kwenye damu ya ukoo wenu, ndio maana ukienda hospitali kwa Daktari mfano una kisukari anaweza kukuuliza kwenye familia yenu kuna mtu anayeugua kisukari. Unapokuwa unatembea kuna kuwa na viumbe wanakuangalia kwa sababu una alama.

Hivi unajua kufanikiwa ni rahisi kuliko kushindwa, ndege ameumbwa na uwezo wa kupaa haendi tuition, jaribu kupaa wewe, kiumbe ameumbwa na uwezo wa kufanikiwa, mtoto hafundishwi kunyonya shule, akizaliwa anajua tu maziwa sio kupuliza ni kuvuta, kila kiumbe imeumbwa na uwezo wa kufanikiwa na ndio maana kila kiumbe ana nguvu kwenye eneo lake, mamba akikukamata anakuvuta na kukutupa kwenye maji kwa sababu ndio eneo lake, sisi eneo letu ni neno la Bwana, mechi yetu ni imeandikwa, unatumia maandiko ili uweze kushinda vita.

Sisi asili yetu ni mbinguni kitabu chetu ni neno la Mungu, ukirudi kwenye asili yako hakuna atakayekuweza, kuna familia chapa ya familia imewekwa kwenye damu, mtu mwenye chapa ya kushindwa hata kama ukimshika mkono kumtoa hatoki, ukiwekewa alama kila kiumbe anakushughulikia kulingana na alama uliyo nayo, inawezekana kwenye familia yenu wachawi wameweka chapa, inawezekana kitovu wamekizika mahali ili usifanikiwe, tukimfuata Yesu hatuangalii kitovu kimezikwa wapi, matukio ya kichawi yapo na yanaweza kupandwa ndani ya familia ndani ya ukoo. leo tunayavnja kwa jina la Yesu.

Post a Comment

0 Comments