google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUSUDI LA MUNGU KATIKA KIZAZI CHAKO

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 21 APRIL 2024
ASKOFU DKT JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: KUSUDI LA MUNGU KATIKA KIZAZI CHAKO

Kila mtu unayemuona anaisha duniani lipo kusudi la Mungu katika maisha yake, na kusudi la Mungu haliwezi kuzuiwa na mtu, kila juhudi ya kuzuia kusudi la Mungu kwenye maisha yako hiyo ndiyo hatua ya kuliwahisha, na litatokea kwa wepesi zaidi kuliko lilivvyokusudiwa.

“Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la BWANA ndilo litakalosimama.” mithali 19:21 

Mahali popote ulipo liko shauri la Mungu nalo litasimama.

"Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu." Matendo 13:36

Mungu ni Mungu wa makusudi na kila alichokiumba kina makusudi, Mungu ameweka kusudi juu ya kila mtu, na mtu kwa kadri anavyoishi anazidi kulitumikia kusudi, kusudi lako likiisha unalala, kama kusudi halijaisha hauwezi kufa. Kila aluiyezaliwa ana kusudi la Mungu na anayeshindana na wewe anashindana na kusudi la Mungu na ashindanaye na Bwana atapondwa kabisa.

“Washindanao na BWANA watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; BWANA ataihukumu miisho ya dunia; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake.” 1 samweli 2:10

Kusudi huwa haliondoki hata kama umekosea, Mungu akikupa amekupa na ndio maana unaona wanamuziki wa ki-dunia wanaimba kwenye ufalme wa shetani ila Mungu hawezi kuwanyang`anya atakutana nao siku ya wisho.

Mungu akikupa amekupa, wanadamu wakikupa ukiwaletea matatizo wanakunyang`anya, unapokwenda na mtu angalia kusudi la Mungu kwanza kwa maana kusudi la Mungu haliwezi kuzuiwa na mtu.

Kuna watu leo unaona hawafai kumbe Mungu ameweka kusudi ndani yao, kuna muda utafika wale uliowanenea mabaya utaona wapo juu ya Mlima.

“na Salmoni akamzaa Boazi; na Boazi akamzaa Obedi; 22na Obedi akamzaa Yese; na Yese akamzaa Daudi.” Ruthi 4:21

“Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu. Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake; Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu; Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni; 5Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese; Yese akamzaa mfalme Daudi. Daudi akamzaa Sulemani kwa yule mke wa Uria.” Mathayo 1:1-6

Unaweza kuwa hapa namna yako ya kuzaliwa ilikuwa ya ajabu ajabu lakini kusudi la Mungu kwako halibadiliki.

“na Yese akamzaa Eliabu, mzaliwa wake wa kwanza, na wa pili Abinadabu, na wa tatu Shama; na wa nne Nethaneli, na wa tano Radai; na wa sita Ozemu, na wa saba Daudi;” 1 Nyakati 2:13-15

Mungu anapokuitia jambo, anakupaka mafuta kwenye jambo hilo, hata kama unaona muda umeisha  lakini litatimia, kuna watu wako hapa ila si wa hapa yani wewe kuna nyumba yako Canada mahali lakini wewe hujijui, kazi yako iko Uingereza mahali.

Yule unayemuona hayuko sawa ndio kusudi la Mungu linawekwa ndani yake, kwenye familia yako muangalie sana asiyependwa, anaweza kuwa na kitu, Mungu ana kawaida akikuchagua anaruhusu udharauliwe ili ukifanikiwa watu washangae, kuna hatua polopole zitaanza za kusababisha uingie kwenye kusudi mahali unapotakiwa kuingia, kuna ufunguo uko mbele yako, Mungu akiwa na kusudi na wewe anakupa vifaa vya kuvitumia kwenye kusudi lako. 

Kuchaguliwa na Mungu haimaanishi kwamba watu watakupenda lakini kusudi la Bwana litasimama wapo watu wanapitia magumu wanajiuliza watatokaje, kuna wakati unafika utatoka , yale unayoyaona ni ya muda tu utatoka, kuna mambo Mungu anakuinulia ili uyatandike, ili uweze kungia kwenye nafasi nyingine, Mungu anaweza kuruhusu jambo fulani gumu, usilikwepe tunisha msuli useme hapo ndipo nitakapoinukia, ukiona fitina imezidi, maneno yamezidi, pesa hakuna, ujue unakaribia kupenya hapo, ukimuona Goliathi cheka kwanza maana bila Goliathi Daudi anabakia pale, kama huna Goliathi kwenye maisha yako, mbele yako hakuna kitu.

Goliathi anaweza kuwa madeni, kuna watu wamezima simu si kwa sababu wapo kwenye ibada ila ni kwa sababu wanadaiwa, mwenye kusudi ndani yake hawezi kukosa madeni lakini si kwamba Mungu amekuacha anakupeleka mahali alikokupangia, hali yako ya leo haimaanishi ndio hali yako ya kesho, kila unaloliona lina makusudi

Mungu akitaka kufanya jambo anasababisha tukio ili akubebe wewe, Mungu anasababisha tukio ili uanze kwenda. 

Nyuma ya kila kuinuliwa yuko Goliathi, wapo watu ambao hatima yao imeunganishwa na hatima yako, hatima ya Daudi ilikuwa imeungana na ya Nathaniel. `

Kusudi la Mungu haliwezi kuzuiwa na mtu, ukiwa una tatizo leo haimaanishi kwamba Mungu amekuacha , Mungu anaruhusu shida ili akunoe, Mungu akitaka kukuinua anaweza kusababisha jambo fulani, wanakusingizia jambo kumbe ndio wana kupeleka kwenye hatima yako. Watu wanaweza kukusemea mabaya ipo siku Mungu atakuinua na hali yako hiyo hiyo.

Usishindane na mtu ambaye kusudi la Mungu liko kwenye maisha yake, ukiwa na wito wa Mungu wewe hujijui ila tu unakuwa unaona mbona mimi nampenda sana Mungu, kusudi la Mungu ni la watu wote. Kila jambo linalopangwa yupo mtu amaendaliwa na Mungu atakuokoa, hauwezi kufa mpaka kile ulichopewa na Mungu kitimie kwenye maisha yako. 

Mtu unayempenda zaidi, unayemuamini, unayemsaidia ndio atakuwa wa kwanza kukusaliti, lakini mwisho wao wote watapondwa watasagwasagwa, hatari unazokutana nazo haziondoi kusudi la Mungu ndani yako, Mungu akikupenda hakupi hela maana zinaweza zikaisha, hakupi nyumba maana inaweza kuungua, hakupi gari maana linaweza kupata ajali, Mungu akikupenda anakupa Neno ukilishikilia Neno unapata vyote, hautakufa mpaka utimize mambo yako yote kwa jina la Yesu. 

Mungu akiwa na mpango na wewe wanaokutafuta ni wengi, ila usiogope Mungu yupo pamoja na wewe hatakuacha mpaka kusudi lako litakapotimia hakuna hata jambo moja ambalo halitatimia kwenye maisha yako.

Kila mtu ukimuangalia unatakiwa ujiulize hivi huyu  atakuwa nani, wangekuwa wanajua Daudi atakuwa Mfalme wangekuwa na urafiki nae, uwe na uwezo wa kuona rohoni hazina iliyojificha ndani ya watu na uwapende si kwa sababu ya vitu bali kwa ajili ya hazina iliyoko ndani yao.

Juu yako liko kusudi la Mungu na halitazuiwa na magonjwa, na ajali mpaka liweze kutimia, wako adui zako wanaweza kukuzuia, kusema maneno mabaya juu yako ili usipige hatua, pigana nao uwamalize wakati wa uhai wako, utakayembakiza atakuwa adui wa wanao, Naamuru kuanzia leo kusudi la Mungu lisimame juu yako kwa jina la Yesu.

BONYEZA HAPA KUTAZAMA IBADA NZIMA YA JUMAPILI

Post a Comment

0 Comments