google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KIAPO CHA KICHAWI

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
JUMAPILI 7 APRILI 2024
ASKOFU DKT JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: KIAPO CHA KICHAWI

Kiapo ni ukomo wa mashindano, zamani watu walipokuwa wanabishania jambo mkiapa basi jambo linaisha. Kwenye Biblia neno kiapo limeandikwa mara arobaini na tano, na Bwana ameapa limeandikwa mara kumi.

Aina za viapo;
  1. Kiapo kati ya mtu na mtu.
  2. Kiapo cha ndoa.
  3. Kiapo cha maagano.
  4. Kiapo cha Mungu.
  5. Kiapo cha wachawi.

Maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao; na kwao ukomo wa mashindano yote ya maneno ni kiapo, kwa kuyathibitisha. Katika neno hilo Mungu, akitaka kuwaonyesha zaidi sana warithio ile ahadi, jinsi mashauri yake yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati; Waebrania 6:16-17

Zamani kwenye agano la kale kulikuwa na makuhani wengi, ukoo mmoja wapo ulikuwa ni walawi, walawi ni mtu alieitwa Lawi, Mungu akitaka kuanza jambo huwa anaanza na mtu. Mungu anamwambia Musa katika makabila kumi na mbili kabila mojawapo watakoaozaliwa watakuwa makuhani mbele za Mungu. Kwa nini wao? Mungu ameshachagua, ndiyo maana Mungu anaweza akachagua mtu hata kama ana madhaifu mengi ila ndio ameshamchagua. Kabila la Lawi hawakupewa shamba wala chochote Mungu akasema mimi ndiyo urithi wenu, kazi ya walawi wenyewe wanatoka makuhani na ndio maana Musa alikuwa wa ukoo wa kabila ya Lawi.

Mungu alipotaka kumleta Yesu kuwa kuhani, akaapa kuwa huyu Yesu atakuwa kuhani wa milele yaani hazuiwi na kifo.

maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe u kuhani milele;) ' basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. 'Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu wazuiliwa na mauti wasikae; Waebrania 7:20, 22,23

"BWANA ameapa, Wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki. Bwana yu mkono wako wa kuume; Ataseta wafalme, Siku ya ghadhabu yake. Atahukumu kati ya mataifa, Ataijaza nchi mizoga; Ataseta kichwa katika nchi nyingi. BWANA ameapa, Wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki. Bwana yu mkono wako wa kuume; Ataseta wafalme, Siku ya ghadhabu yake. Atakunywa maji ya mto njiani; Kwa hiyo atakiinua kichwa chake. Zaburi 110:4-7"

Ukuhani wa Yesu ni wa milele na kwa sababu anakaa ndani yetu sisi pia ni makuhani, ukijiona wewe ambaye ni mtakatifu unaapa ndani ya ndoto maana yake Mungu ameapa kwa niaba yako.

"Malaika wa BWANA akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu Mwanzo 22:15-18"

Mungu akikupenda anakupa neno la kukuvusha, anakupa neno la kukuinua neno hilo ndilo kiapo. Mungu akimpa mtu jambo kwa kiapo huwezi kumnyanganya. Mungu akikuambia jambo hata kama hulielewi tii.

Isaka alikuwa anataka kuondoka kwenye nchi ya kiapo Mungu akamwambia kaa hapo hapo, na ndio nchi inayogombaniwa mpaka sasa hivi. Kiapo ndio mwisho wa mashindano. 

"BWANA akamtokea, akasema, Usishuke kwenda Misri, kaa katika nchi nitakayokuambia. Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako. Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia. Mwanzo 26:2-4"

Ukitamkiwa jambo kwamba hutakufa hata kama ukitokea ugonjwa wa kukuua Roho Mtakatifu atasimamia maneno yaliyotamkwa kwamba hutakufa.

Kiapo maana yake halibadiliki neno na wachawi wanaweza kuapa, wameapa hutaolewa, wameapa hutasafiri, kuna mizimu imeshaapa huwezi kukaa kwenye makochi, wameapa maishani mwako hutaendesha hata gari, lakini leo nakwambia utaendesha gari kwa jina la Yesu, tena ukifika nyumbani uanze na kufanya mazoezi ya kuendesha gari wewe mwenyewe chumbani kwako.

Kulipopambazuka, Wayahudi wakafanya mapatano, wakajifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala hawatakunywa hata wamwue Paulo. Nao wakaenda kwa wakuu wa makuhani na wazee, wakasema, Tumejifunga kwa kiapo tusionje kitu hata tumwue Paulo. Mjomba wake Paulo akasikia habari za kuotea kwao, akaenda akaingia ndani ya ngome akampasha Paulo habari. Paulo akamwita akida mmoja, akasema, Mchukue kijana huyu kwa jemadari; maana ana neno la kumwarifu. Basi akamchukua, akampeleka kwa jemadari, akamwambia, Paulo, yule mfungwa, aliniita akataka nikuletee kijana huyu kwa kuwa ana neno la kukuambia. 19Yule jemadari akamshika mkono akajitenga pamoja naye kando, akamwuliza kwa faragha, Una neno gani utakalo kuniarifu? Akasema Wayahudi wamepatana kukuomba umlete Paulo chini kesho, ukamweke mbele ya baraza, kana kwamba wanataka kupata habari zake kwa usahihi zaidi. Basi wewe usikubali; kwa maana watu zaidi ya arobaini wanamwotea, wamejifunga kwa kiapo wasile wala wasinywe hata watakapomwua; nao sasa wako tayari, wakiitazamia ahadi kwako. Matendo 23:12,14,16-21

Kila familia huwa hakosekani kuhani wa shetani, huyo usimuache unatakiwa kumpasua vipande vipande.

Mashetani wana namna tatu za kukaa kwa mtu; 

  • Anaingia ndani mwako.
  • Anakaa pembeni yako.
  • Anakaa kwenye kinywa.

Wasimamizi wa kiapo wanaweza kukaa kwenye kinywa chako, unasema hutaki shule, hutaki kuolewa, wanaitwa wasimamizi wa kiapo, unapata mchumba wasimamizi wa kiapo wanamtokea mchumba wako, mchumba anaota yupo kwenye chungu na wewe ndo unampika, mchumba anaghahiri kukuoa, hii ndio sababu unaweza kukuta binti mzuri mrembo lakini haolewi ni kwa sababu anasimamiwa, unaweza kushangaa kuna binti wa kawaida halafu akapata kijana mzuri, unaweza ukajiuliza huyu kaka kampendea nini, wewe huonekani kwa sababu unasimamiwa.

Kiapo kinaweza kusimamiwa na jini kuna kajini kadogo kamepewa damu kidogo aje asimamie jambo lako ukitamka kwa jina la yesu anatoka, kuna mwingine linatumwa jini kubwa amechinjiwa mbuzi, kuna mwingine anatoa kafara ya mtu dude linalokuja linakuwa kubwa kweli kweli. 

Kiapo cha kichawi kina wasimamizi wa kiapo ndio maana ukiomba huwezi kupata nafasi, wazee wamesema huwezi kuoa, unatakiwa kuomba kuwachakaza katika jina la Yesu.

Ili kushinda maneno ya viapo ya ufalme wa giza ni lazima utumie na utamke kwa mamlaka ya jina la Yesu.

Post a Comment

0 Comments