google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAARIFA KUTOKA KWA MUNGU

 UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 19.01.2025
ASKOFU DR JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: TAARIFA KUTOKA KWA MUNGU

Mungu kwenye agano jipya ana watu ambao ni zaidi ya wale kina Eliya, Musa tunaowaona kwenye agano la kale. Agano la kale ni kivuli cha yatakayokuja, na agano jipya ndio mambo yenyewe. Sisi tuna nguvu za ajabu kuliko ilivyokuwa kwenye agano la kale. Kuna jamii ya watu wa Mbinguni wameganyika katika makundi matatu;

1. 1. Hawajui kinachoendelea. Wale ambao hawajui kinachoendelea, wanatembea kwa kupapasa papasa na kuuliza uliza.

1. 2..  Wanaojua kinachoendelea. Wale ambao wanajua kinachoendelea na kufanyika.

1. 3. Wanaofanya vitu vitokee. Hawa wapo jikoni, wanapika mambo yanavyotakiwa kuwa. Wale wanaojua kinachoendelea na wanaelewa kinachopikwa.

Mwanadamu ni kiumbe peke yake anayeweza kuwa Dar es Salaam, akafanya kazi Dodoma au kusababisha matukio Mwanza. 

“Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.” Amosi 3:7

Kwa hakika na sio kubahatisha Mungu hafanyi kitu hapa duniani bila kuwajulisha watumishi wake na manabii. Ujumbe wa kwanza kuwa Yesu atazaliwa duniani amepewa Adamu na Hawa miaka 4000 kabla ya Yesu kuzaliwa. Nyoka ni shetani. kiiashara kanisa ni uzao wa mwanamke. Uadui wa kwanza ni kati ya nyoka na shetani na mwingine kati ya nyoka na uzao wa mwanamke.

“BWANA Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.” Mwanzo 3:14 - 15

Unabii wa pili ya kwamba Yesu atazaliwa, Mzee Yakobo wakati anakata roho akatamka maneno ya kuwabariki. Yakobo alitabiri kuzaliwa kwa Yesu miaka 1800 kabla.

“Yuda, ndugu zako watakusifu,Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako.Wana wa baba yako watakuinamia. Yuda ni mwana-simba,Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda;Aliinama akajilaza kama simba,Na kama simba mke; ni nani atakaye mwamsha? Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda,Wala mfanya sheria kati ya miguu yake,Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki,Ambaye mataifa watamtii.” Mwanzo 49:8-10

Mungu alimwambia pia Musa kuwa Kristo yuaja. Kadiri miaka inavyozidi kukaribia ndivyo Mungu huwajulisha watu zaidi. Musa alitoa utabiri wa kuzaliwa wa Yesu miaka 1500 kabla. Mungu anaongea na Musa kuwa atawaondokeshea nabii.

“Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.” Kumbukumbu 18:18.

“Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.” Yohana 3:14-15

Nyoka aliinuliwa miaka 1500 kabla ya Kristo kabla unabii wa Yesu kuzaliwa.  Nabii Mika pia alitabiri Yesu atazaliwa mji gani.

“Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.” Mika 5:2

Na wachawi yaani Mamajusi pia waliona kuhusu kuzaliwa kwa Yesu.

“Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.” Mathayo 2:1-2

Isaya pia alijua kwa hakika Yesu atakuwa nani na majina yake miaka 700 kabla ya Yesu kuzaliwa. Kwa kadiri ahadi Mungu unavyozidi kukaribia Mungu anazidi kusema na kuwajulisha watu zaidi. 

“Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,Tumepewa mtoto mwanamume;Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;Naye ataitwa jina lake,Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,Baba wa milele, Mfalme wa amani.Maongeo ya enzi yake na amaniHayatakuwa na mwisho kamwe,Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake;Kuuthibitisha na kuutegemezaKwa hukumu na kwa haki,Tangu sasa na hata milele.Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo.” Isaya 9:6-7

Mungu ni Mungu wa majira, ulimwengu haujiongozi wenyewe. Kama vile ambavyo kila kitu hakijajiweka chenyewe ila kuna mtu kaweka hata dunia kila kitu kuna aliyekiumba ambaye ni Mungu pekee.

“Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; maana mimi ni Mungu; hapana mwingine.” Isaya 45:22

Mbinguni kuna mfumo wa Mungu wa taarifa ambao hauendi kwa simu au internet ila kulingana na nyakati ambazo Mungu hutaka kufanya jambo lake. Chemchem ya taarifa ni Mungu, na anapoachilia kwenye mfumo Mbingu na kuna watu hapa duniani wanapata taarifa moja kwa moja.

“Tena Mungu akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli maneno haya, BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote. Enenda, ukawakusanye wazee wa Israeli pamoja, ukawaambie, BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea, akaniambia, Hakika nimewajilieni, tena nimeyaona mnayotendewa huko Misri;” Kutoka 3:15-16


Post a Comment

0 Comments