google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ADUI WA NJIANI

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 13.10.2024
ASKOFU DKT JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: ADUI WA NJIANI

Kila mtu maisha anayoyaishi sio kama ananvyo waza. adui wa njiani anakuja pale kwenye njia yako na adui huyo lengo lake ni kuizuia kile kitu ambacho Mungu amekupa. Kuna mambo mtu ananataka kufanya lakini kuna kizuizi ambacho kina zuia usifanye hilo jambo. Maisha yako sio kwamba unafanya ili ufanikiwe ila kwasababu Mungu alisha panga kabla ya kuumbwa kwa misingi ya Ulimwengu. Inakupasa kufanya vita na adui huyo ili asiweze kukuzuia.

“Kumbuka aliyokufanya Amaleki katika njia mlipokuwa mkitoka Misri; jinsi alivyokukuta katika njia, akapiga katika watu wako walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge nyuma yako, ulipokuwa umechoka na kuzimia; wala asimche Mungu. Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha BWANA, Mungu wako, katika adui zako wote walio kando-kando, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahau.” kumbukumbu ya torati 25:17-19

Kuna wakati Mungu anaruhusu magumu uyapitie na anaweza kumtumia mtu yoyote iliaweze kukuimarisha na uweze kuyafanya mapenzi ya Mungu itimie hatakama unamali. Mtu wa Mungu akipewa kitu na Mungu ameshampa na hakuna mtu wa kukuporomosha.  kinachotokana na Mungu lazima kitadumu kwasababu ilishaamriwa kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.

“BWANA akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne. Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi.” Mwanzo 15:13-14

Pale unapo haidiwa na Mungu kwa habari ya maisha yako ndipo pale adui anapojitokeza ili aweze kukuzuia kuya fanya ambayo Mungu amekuhaidi. na adui huyo anapambana ili usiweze kuyafanya mapenzi ya Mungu na kuna wakati unapitia mambo magumu. kuna wakati mtu anayapitia na anatamani hata amwache Mungu ila bado anakuwa na matumaini ndio mtu huyo anayokusudi la Mungu.

“usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.” Isaya 41:10 

Kabla ya kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu ulikuwepo tena ulikuwa mbinguni Pamoja na Mungu. baba na mama yako baada ya kukutana katengeza ganda ambao ni mwili na kuingia wewe ambae ni roho na kuwa ndani ya mwili. 

“Neno la BWANA lilinijia, kusema, Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.” Yeremia1:4-5 

Mungu akipanga jambo ni lazima litimie na hakuna mtu wakuzuia jambo hilo. Inakubidi uombe kwa bidii ili uweze kuyatimiza yale makusudi ya Mungu na kumwangusha kila adui anayetaka kukuzuia kuelekea kwenye hatima uliopangiwa. Usimdhalau mtu kwasababu wenye haki huwa hawawezi kumwaibisha mtu kama ilivyo kwa Yusuph alitaka kumwacha Maria bila kumdalilisha Maria pale alipokuwa ana ujauzito

“Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.” Mathayo 1:18-19

Kuna mtu hatakama amepigwa na adui wa njiani ila bado Mungu anakuwa na makusudi nayo. Kuna mambo mtu anayoyapitia ili yaweze kumfanya kuwa imara. Ili atakapo pata aweze kuwa na hekima wakati wa kumiliki kwake.

“Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.” Mithali 3:16

“INATUPASA KUMPIGA ADUI WANJIANI ILI KUWEZA KWENDA KULE MUNGU ALIPOSUDIA KWENDA.” AMEN.

"BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA NZIMA YA JUMAPILI"

Post a Comment

0 Comments