google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAHUSIANO IMARA

 UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
SEMINA YA MAHUSIANO
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGE
SOMO: MAHUSIANO IMARA

Kuna watu wana Maisha imara hatakama kuna wimbi gumu. Uhimara wa mtu haupimwi na mafanikio ya mtu. ila kwa yale magumu anayo yapitia, uhimara unapimwa kwa sababu kuna mambo anayaaamini na unayafanya hatakama kuwe na matokeo mazuri na matokeo mabaya. Kila mtu sio kila siku anapatwa na wakati mbaya na sio kila siku anapatwa na wakati mzuri.

“Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.” Yakobo 1:12

Kuna watu wanafedha na sio imara na akipata changamoto yoyote anachana nayo jambo hilo. kuna aina tofauti tofauti  ya mahusiano. kuna mahusiano ya mtu na Mungu na mahusiano kati ya mtu na watu. Kwenye sheria za Mungu kuna mahusiano kati ya mtu na Mungu,mahusiano kati ya mtu na wazazi wake na nyingine ni mahusiano kati ya mtu na watu wengine.

“Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,” Efeso6:2

Mahusiano kati ya mtu na Mungu ina athiri mahusiano mengine yote, kwasababu mtu mwenye mahusiano na Mungu ni rahisi kuwa mahusiano na ndoa yako kwa sababu mahusiano ya mtu na Mungu inajenga hofu ya Mungu ya kuto vunja mahusiano kwenye ndoa yako.

“Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.”1Yohana 4:21

Zamani watu walikuwa na mahusiano na miungu nayo hatakama sio wa kweli na wana desturi ya kuongea na miungu yao. Kuna mambo hufanyi kwasababu ya kuwa na hofu ya Mungu hatakama unauwezo wa kuifanya. mtu anayelinda mahusiano hataki kupoteza mahusiano na mtu huyo. mahusiano imara ya Mungu hutengeza mahusiano imara na mtu mwingine

“Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu.” Yohana15:9

Ili kuwa na mahusiano imara ya Mungu ni kuwa na mahusiano na familia ya kiroho, kwa kufanya hivyo inamsaidia kuwa imara. kuunganisha mahusiano inaweza kufanya mtu kuwa imara. masha imara ni ya kikanuni ambazo tukizifuata tunakuwa imara. Kuna sheria kwenye Biblia kuna kanuni ambazo Mungu ameziweka ili tuzi fuate na kuwa imara kwe nye mahusiano.

“Ndugu zangu, wana wa ukoo wa Ibrahimu, na hao miongoni mwenu wanaomcha Mungu, kwetu sisi neno la wokovu huu limepelekwa.” Matendo 13:26

Mungu ametukusudia tuwe Pamoja tumejengwa ili kwa kushirikiana au kuambatana kwa Pamoja na kuijenga uhimara, kwa kuwa na mahusiano na familia ya kiroho. maana ndugu katika kristo niwathamani kuliko mtu yoyote kwa maana asili yetu sisi ni roho watu wanashindwa kuwa na mahusiano na familia ya kiroho ili wasivunje mahusiano ya ndugu yao. mahusiano wa kiroho ni ya thamani kuliko mahusiano ndugu zako

“Malaika wa BWANA akamwambia Balaamu Enenda pamoja na watu hawa, lakini neno lile nitakalokuambia, ndilo utakalosema. Basi Balaamu akaenda pamoja na wakuu wa Balaki.” Hesabu 32:25

Mahusiano imara ya familia ya kimwili ambaye mume, mke na Watoto,mtu akikosa malezi ya kimwili Maisha yake yanakuwa ngumu,malezi ya kimwili ya natokana na mtu alivyo lelewa. mtu analea familia yake kama alivyolelewa, kama alilelewa vibaya au vizuri ndio inapelekea nanma utakavyo lea familia.

BONYEZA HAPA KUANGALIA SEMINA YA MAHUSAIANO

Post a Comment

0 Comments