google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAKATI WAKO UMEFIKA

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 19.01.2025
ASKOFU DR JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: WAKATI WAKO UMEFIKA 

Kuna mamlaka ya kiroho nyuma ya kila mamlaka ya kimwili, mamlaka za kiroho zikishindwa na mwili inashindwa na mamlaka ya kiroho ikishinda na ya mwili ina shinda. Kila mamlaka unayoiona kwenye ulimwengu wa mwili, kuna kuwa na mamlaka nyingine kwenye ulimwengu wa inayoiongoza. Ni sawa na mti ukikosa maji unakauka.

“Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji. Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.”Mwanzo 1:6

Kwenye kila jambo ambalo Mungu amekuwekea pale unapo enda kuna watu unatakiwa kuwa piga ili umiliki kile Mungu alicho kupatia. Yoyote atakaye jaribu kushindana na Mungu, Mungu humponda mtu huyo. Upande wa Mungu una nguvu kuliko upande wowote kwa hata maadui washirikiane hawawezi kumshinda mtu wa Mungu. kila kitu kina tokana na Mungu, upande wa shetani wana kopi kila kitu kama vile kuonekana na kupotea, kwa maana Mungu ni asili ya vyote.

“basi akatuma wajumbe kwa Balaamu mwana wa Beori, hata Pethori, ulio kando ya Mto, mpaka nchi ya wana wa watu wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna watu waliotoka Misri; tazama, wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili mimi. Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa.” Hesabu 22:5-6

Kwenye ulimwengu wa kiroho ukishinda ni swala la muda kudhiihirika kwenye ulimwengu wa mwili. Kuna mambo yakifanyika kwenye ulimwengu wa kiroho na matokeo yake honekana kwenye ulimwengu wa mwili.

“Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza;Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;” Mhubiri 3:1,6

Wana wa Mungu hawaangalii dalili  ya kitu ila wana angalia neno, wewe una nguvu si sababu ya kuomba ila ni lazima kuomba, na si kwasababu una funga ila ni lazima kufunga, kwasababu wakati wako umefika wa kubarikiwa umeshafika.

“Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana BWANA, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha.” Kumbukumbu ya torati 31:6

Mungu humchagua yeye amchaguaye na humchukia yeye hamchukiaye ili kusudi la Mungu la kuchagua lisimame. unaweza ukang’ang’ania jambo ila  ni mbinu ambayo adui amekusogeza ili akupige. Kila mtu ana wakati wake ambao Mungu amemwekea mtu ila si kwa kuomba ila ni kwasababu wakati ukifika umefika.

“Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye. Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu.” Warumi 9:15-16

Kwenye Maisha kuna wakati wa mandalizi ambao mtu anatengenezwa ili aweze kuelekea kule Mungu alipokukusudia kwenda. jambo la Mungu likikaribia Mungu sema mara kwa mara aidha ni kwa unabii au ndoto au kwa namna yoyote ili ujue kuwa wakati ukifika umefika. Pembe kwenye biblia inamaanisha nguvu. Umetoka mbinguni na umekuja duniani ili kuifanya kazi ya Mungu na baada ya kumaliza unarudi mbinguni ili kupeleka taarifa kwa kile Mungu alicho kuagiza.

“Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake. Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.” Yohana 1:32-33

BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA YA JUMAPILI

Post a Comment

0 Comments