Na Mchungaji Yekonia Bihagaze (RP) Jumatatu 8.10.2012
UTANGULIZI:
Mwisho wa somo ili utagundua nguvu iliyopo nyuma ya
kusamehe. Kuna watu wanapitia kwenye matatizo na magonjwa kwasababu ya
kutokusamehe.
Mathayo 6:9-12 “basi ninyi salini hivi…12 msipowasamehe
wengine makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu” Zaburi
103:3 Hapa tunaona kuwa kanuni ya Mungu ni kusamehe kwanza kabla ya
kuponya. Na ndio maana waweza kumwona mtu anasema ameokoka lakini bado yupo
kwenye ugonjwa kwasababu ya kutokusamehe.
KWANINI UMSAMEHE
ALIYEKUKOSEA:
Kumsamehe mtu aliyekuumiza sio jambo la mzaha, na ndio maana
kuna watu wanasema kuwa wamesamehe lakini ndani ya mioyo yao bado hajasamehe. Tunatakiwa kusamehe kwasababu kuna nguvu
iliyopo nyuma ya mtu aliyekukwaza au kukuumiza.
Watu wengi wanashindwa kusamehe kwasababu hawajui nguvu iliyopo nyuma ya yule mtu aliyewakwaza. Emu tuangalie
mfano wa gari; Gari linapomgonga mtu serikali haishtaki gari bali anayeshtakiwa
ni dereva. Vivyohivyo ukiumizwa unatakiwa uangalie ile nguvu iliyopo nyuma ya
aliyekuumiza. Kimsingi kuna nguvu inayotenda kazi nyuma ya aliyekuumiza na
usipoijua hiyo nguvu utajikuta unashindwa kusamehe.
VITU VITATU AMBAVYO
NI VIPIMO KAMA UMESAMEHE AU BADO HUJASAMEHE:
1.
Ukimsamehe mtu utamwongelea vizuri:
Kama kweli umemsamehe mtu utamwongelea
vizuri mbele za watu, kama unasema umemsamehe mtu alafu bado unamwongelea
vibaya ujue bado hujasamehe kutoka moyoni mwako. Ukimkuta mtu anaongea mabaya
kuhusu mtu aliyemkwaza basi ujue ndani ya moyo wake kuna madabahu ya makwazo na
machungu. Na kwasababu hiyo kuna watu wamefukuzwa kazi, wamepigwa kwasababu ya
kushindwa kuwanenea watu mazuri.
2.
Ukimsamehe mtu utamwombea:
Ishara nyingine kuwa ya kuonyesha kuwa
umesamehe ni kumwombea mwingine mazuri; na ndio maana Eliya alipotaka kujenga
madhabahu ya Mungu alibomoa kwanza
madhabahu ya baali, hata leo huwezi kujenga madhabahu ya Mungu ya amani kama
bado moyoni unamadhabahu ya kutokusamehe. Watu wengi wamejikuta wakiomba mabaya
kwa watu waliowakosea na kwa namna hiyo wanashindwa kupokea majibu ya matatizo
yao.
3.
Ukimsamehe mtu utawasiliana kwa uzuri:
Ukimsamehe mtu utawasiliana naye kwa uzuri, nah
ii ni kwenye madhabahu ya moyo wako. Hata kama amekujibu vibaya wewe mjibu kwa
uzuri. Ni kweli kuwa ukisamehe Yule mtu atakudharau lakini ni muhimu kujua kuwa
tunasamehe si kwa ajili ya waliotukosea bali kwa ajili yetu.
Watu wengi wanashindwa kusamehe kwasababu ya kukosa nguvu ya
uwezesho ya kuweza kusamehe. Kila mtu aliyeokoka anayo nguvu ya uwezesho ya
kusamehe, nayo ni Roho Mtakatifu. Kila mtu aliyeokoka ana Roho Mtakatifu naye
hutuwezesha kusamehe, kuokoka kunakupa nguvu ya uwezesho kusamehe. Bila kusamehe huwezi kupokea kutoka kwa BWANA.
MAOMBI YA KUSAMEHE:
Baba katika Jina la Yesu Kristo ninaomba nguvu ya msamaha
wako; leo nimetambua kuna nguvu inayotenda kazi nyuma ya mtu aliyenikwanza, leo
ninawasamehe wote walionikwaza katika Jina la Yesu. Ninatangaza msamaha,
ninavunja madhabahu ya makwazo na kutokusamahe ndani yangu katika jina la Yesu
Kristo.
Baba ninaomba uniponye na matatizo yaliyoingia ndani yangu
kwasababu ya kutokusamehe katika Jina la Yesu. Leo ninabadilika katika Jina la
Yesu. Mimi ni mzima na nimeponywa katika Jina la Yesu.
UFUFUO NA UZIMA (THE GLORY OF CHRIST (T) CHURCH)
TANGANYIKA PACKERS,
KAWE, DAR ES SALAAM.
1 Comments
ubarikiwe sana mchungaji ujumbe wako umenifikia wakati sahihi asante sana
ReplyDelete