Na mwandisi
wetu.
Sehemu ya Maelfu wa Washirika wa Ufufuo na Uzima wakiwa Tanganyika Packers ibadani (Majeshi ya BWANA) |
Mwaka
mpya wa 2013 Dar es Salaam itatekwa na moto wa Mungu kwa namna isiyo ya kawaida
ambapo maelfu na maelfu ya roho za watu zitavunwa kumwelekea Mungu kuliko
kipindi kingine chochote katika historia ya moto wa Mungu hapa jijini.
Akitoa
sehemu ya salamu za mwaka mpya Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,
Mch. Josephat Gwajima alisema hayo leo tarehe 29 Disemba 2012 alipokuwa akifundisha
kundi kubwa la viongozi wa wapatao elfu 10,000 wa kanisa hilo lenye washirika
zaidi ya 70,000.
Mchungaji
kiongozi alisema kuwa ameamua kusitisha mikutano yote ya Injili ya nje ya nchi
kwa mwaka 2013 isipokuwa mikutano miwili itakayofanyika China na Marekani.
Kanisa la Ufufuo na Uzima lenye makao yake makuu Tanganyika Packers jijini Dar
es Salaam litaanza rasmi mikutano ya injili itakayofanyika nchi nzima kwa mwaka
2013 ambapo maefu ya watu wanatarajiwa kuokoka, kuipa dunia kisogo, kuacha
dhambi na kuwa watoto wa Mungu.
Mkutano
wa kwanza wa Ufufuo na Uzima unatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Biafra
kwa muda wa juma moja mpaka majuma matatu mwaka 2013. Mikutano
itakayofuata itafanyika katika wilaya zote za Dar es Salaam katika viwanja vya
Mwembe Yanga (Temeke), Biafra (Kinondoni) na Kidongo chekundu (Ilala).
0 Comments