Na Mwandishi wetu. | Dar es Salaam 2
Juni 2013
Zaidi
ya watu 50 wamerudishwa toka msukuleni baada ya kufanyika maombi ya kuwarudisa
leo mchana hapa Kanisani Ufufuo na Uzima kanisa la maelfu ya Watu ambapo
Mchunguji kiongozi Josephat Gwajima alifundisha somo liitwalo ‘Unaishi ingawa umekufa’ na baadaye
maombi yakiongozwa na yeye kwa zaidi ya dakika 15 ambapo watu hao walitoa
ushuhuda kuwa walikuwa wamewekwa kwenye makabati, kibuyu, kwenye chupa,
makaburini na kwa waganga wa kienyeji.
Akishuhudia
mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Neema alisema kuwa alikuwa kwenye chupa
alimowekwa na mke mwenzake, baadaye akasikia sauti ya watu wakimwita kwa nguvu
njoo njoo na baadaye alijikuta yupo chini kanisani akiombewa na wachungaji.
Akieleza
maana ya kuishi lakini umekufa katika somo alilofundisha Mch. Kiongozi Josephat
Gwajima alisema kuwa mtu sio mwili bali mtu ni roho, na roho yenyewe ina nafsi hai na inakaa ndani ya nyumba na nyumba
yenyewe inaitwa mwili. Akielezea zaidi Mchungaji alisema kuwa mtu anaweza kuwa
anaishi anakula anafanya kila jambo mwilini lakini kwa namna ya rohoni ameibiwa
na ametekwana kuhifadhiwa sehemu ama ndani ya chupa,au ndani ya kabati .
Somo
hilo lilifundishwa kwa msingi wa neno la Mungu (Biblia) ambapo Mchungaji
alisoma vifungu vingi vya neno la Mungu ambavyo msingi wake ni kufichua siri za
shetani za kuwaiba watu ambao ni roho zao ingali miili yao inaonekana kuwa hai.
Sehemu ya vifungu hivyo ni pamoja na 1 samweli 22:23,
1
falme 17;22 1 falme 19; 14, Ayubu 33;30 roho inaweza kupelekwa shimoni. Maandiko
haya huelezea namna roho ya mtu inavyoweza kutekwa na ibilisi shetani joka la
zamani na baba wa uongo. Pamoja na hayo Mchungaji alitoa dalili za mtu alikufa
angawa anaishi kutoka 1 Tim 5:6 ‘Bali yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa
angawa yu hai’.
0 Comments