1. 0 Utangulizi
Maandiko ya Msingi: Zaburi 18: 1-50, Waamuzi 6:1-40,
Kipindi ambacho Taifa la
Israel walipokuwa watumwa wa wamidian, watu walikuwa wanaonewa sana na kunyang’anywa
mali zao hata mazao yao yalikuwa yakiharibiwa. Hivyo Gidion alikuwa amejificha
kwenye mwamba akipepeta ngano ndipo malaika akamwita ewe shujaa Gidion,,lakini
Gidion alikataa kuitwa shujaa kwa maaana alikuwa hajiamini. Lakini malaika
akamhakikishia kuwa yeye ni shujaa ila ile madhabahu ya Baali aliyokuwa nayo
baba yake ndiyo iliyokuwa inamshikilia hata asijitambue kuwa ni shujaa. Hii
inatufundisha kuwa kuna madhabahu mahali ambayo inakuzuia wewe usifanikiwe kama
Mungu alivyokusudia kwako.
Kwenye madhabahu ile ya nyumbani
kwao Gidion kulikuwapo na ashera pia, ashera ni mti uliopandwa kwa ajili ya
kusimamia kitu fulani , kwa mfano mti unaweza kupandwa kwa jina la mtu na ule
mti ukistawi ndipo mtu Yule anapata matatizo mfano ugonjwa ndiyo maana kuna mtu
anakuwa mgonjwa wakati wa masika hii ni kwa sababu ya ule mti unakuwa umenawili
kwa mvua. Kuna mtu yuko mahali hapa na watu wasiompenda wamempandia mti eidha
wa balaa, magonjwa, umasikini, kukataliwa, kuachwa na kadhalika, lakini leo
tunatuma radi na kulipua maashera yote kwa jina la Yesu.
Kwa hiyo Gidion akaambiwa
na bwana wewe ni shujaa unatakiwa kwenda kupigana vita ila kwanza bomoa
madhabahu iliyo kwenye mji huu inayofanya watu kuwa waoga. Na sisi leo watu wa
Ufufuo na Uzima tunaenda kila mahali ilipo madhabahu inayolishikilia Taifa letu
na tunaibomoa kwa jina la Yesu. Leo lazima watu wote waliolazwa kwenye
madhabahu ya nchi hii watatoka na kuelekea katika hatima zao na mafanikio yao kwa jina la
Yesu. Gidion baada ya kuibomoa madhabahu
ya Baali watu wa mji walimtafuta ili
wamwuue lakini baba yake Gidion (Yoashi) akasema mwacheni baali ajitetee
mwenyewe kwa kubomolewa madhabahu yake, kwa hiyo nakutangazia hata wewe leo hakuna
dhara hata moja litakalokupata kwa kuzibomoa madhabahu za wachawi .
2.0 MADHABAHU NDANI YA BIBLIA
Mwanzo 8:20, Nuhu alipotoka kwenye safina akamjengea Mungu madhabahu,
Hii inaonyesha kuwa kila madhabahu lazima iwe na tukio inaloliwakilisha, kwa mfano
kuna madhabahu za utawala, kwa hiyo huwezi kumwondoa mtawala aliye na madhabahu
imara mpaka uibomoe ile madhabahu ndipo uguse utawala wake. Mwanzo
12:7, Ibrahim alipoongea na bwana kwamba nchi ile amepewa ndipo alipojenga madhabahu
mahali pale ili isimamie umiliki wake aliopewa kwenye ile nchi, ndiyo maana hata sasa hakuna mtu
anayeweza kuwanyang’anya wa Israel nchi yao ingawa mataifa mengi wamejaribu
kuwaondoa lakini wameshindwa. Mwanzo 12:8,
13:14, Utaona watu kwenye biblia walikuwa wakijenga madhabahu mahali
ili isimamie jambo fulani.
Madhabahu ni mahali ambapo
wachawi na waganga wa kienyeji wanakusanyikia , wanapokuwa mahali pale
wanatoa kafara za damu na wanakuja na mashitaka ya kuwashitaki watu na wananza
kujadili. Kwa hiyo mchawi mmoja anapeleka shitaka la kumshitaki mtu kwa mfano
atasema simpendi fulani kwa sababu analinga eti anahela ,au ana watoto wasomi
au anapendwa sana na watu hivyo nataka
tumkomeshe. Kwa hiyo wachawi wanasema sawa tutamkomesha na ndipo wanapoanza
kumtumia mtu mashetani ya kumharibia maisha yake. Lakini leo nakutangazia kuwa madhabahu zote
zilizotesa maisha yako lazima zibomolewe kwa jina la Yesu. Ninayo ndoto
na ndoto yangu ni kuwa Falme za dunia zimekuwa Falme za mwanakondoo na hii
imeishakuwa kwa maana madhabahu za kichawi zilizozuia injili ya Yesu
zitabomolewa zote kwa jina la Yesu.
Mchawi anapenda
kumshambulia na kumwuua mtu wa karibu yake kwa mfano kaka, dada, mama, baba
nakadhalika. Kwa mfano mtu anataka dada fulani asiolewe kabisa, anapeleka jina
lake kwenye madhabahu na kumwaga kafara, kwa hiyo kuanzia pale yule dada hawezi
kuolewa kabisa kwa maana madhabahu inakuwa inaongea fulani asiolewe, asiolewe. Mwingine
anaweza kuwekwa kwenye madhabahu ya uoga, kwa hiyo hawezi kufanya lolote kwa
kuogopa eidha hasara kama ni biashara, ajali kama ni safari, kuachwa kama ni
ndoa nakadhalika.
Madhabahu inaweza kuwa
kakiwanja fulani ambapo wachawi wanakutanikia na kutoa kafara za damu kwa
miungu wao. Mtu anaposhitakiwa na jina lake kutajwa mahali pale ndipo mashetani
yanaanza kumwandama na kumharibia mambo yake, kwa hiyo mtu yule hawezi
kufanikiwa hata afanyeje mpaka atakapoibomoa ile madhabahu. Madhabahu
zinapobomolewa watu wanaachiliwa kwa hiyo wachawi na waganga wa kienyeji
wanapata hasara, ndiyo maana Gidion alitafutwa auawe kwa kuibomoa madhabahu ya
baali iliyokuwa nyumbani kwa baba yake Yoashi. Leo tutabomoa madhabahu
iliyokutesa na kuwalaza kwenye hiyo
madhabahu wale waliokuwa wamekulaza kwa jina la Yesu.
Madhabahu /kiwanja cha
wachawi huwezi kukiona kwa macho lakini kipo na wachawi wanakutana pale kila
usiku na kuwashitaki watu. Ndiyo maana utaona watu wengi wana matatizo
yasiyoisha, kwa mfano kuna mtu amelazwa kwenye madhabahu ya kuachwa kwenye ndoa
kwa hiyo utamwona mama ameshaolewa na wanaume watatu nakuachwa na wote bila
sababu ya msingi.
Mungu anapotaka kumwinua mtu
anaruhusu apitie mambo magumu sana kila upande na asione msaada. Ndipo sasa mtu
anapoona hana msaada anakumbuka kumlilia Mungu. Kwa mfano Israel walipokuwa na
njaa kali sana mpaka watu wamefikia hatua ya kula watoto wao, ndipo Mfalme akasema mwambie
nabii Elisha kesho saa saba atakatwa kichwa asipotabiri kwa habari ya njaa
kwenye taifa la Israel. Baada ya kutishwa ndipo nabii Elisha alitoa unabii
kwamba kesho chakula kitapatikana tena kwa bei nafuu sana kuliko hata kabla ya
njaa kutokeaa na kesho yake yakatokea
kama vile Elisha alivyosema. Hii inafundisha kuwa mtu unapopata matatizo
usianze kulia wala kuwalaumu watu bali wakati huo ni wakatiwa kuutafuta uso wa
Mungu ili upate jibu la kukutoa mahali pale.
Usifikiri magumu yanayokupata Mungu amekuacha siyo ni kwamba Mungu
anataka uanze kumlilia na kumtafuta yeye kwa moyo wako wote kwa maana aliona
umeanza kwenda mbali naye.
Kwa hiyo kuna madhabahu
ambayo inaweza kuwa imemshikilia mtu mfano mtu anaweza kuwa amelazwa kwenye
madhabahu ya umasikini hata akisoma na kusafiri nchi zote duniani hawezi
kufanikiwa. Kwa hiyo ili mtu huyo afanikiwa lazima aibomoea ile madhabahu. Leo
kila mtu ataomba kulingana na udhaifu alio nao kwenye maisha yake kwa mfano mtu
mwenye hofu ataomba akisema kwa jina la Yesu naibomoa madhabahu ya hofu iliyonishikilia na
kuiharibu kafara waliyoitoa kwenye hiyo madhabahu. Kwa jina la Yesu leo naamuka na kuondoka
kwenye madhabhu walioyonilaza kwa jina la Yesu. Na mtu yeyote aliyepeleka jina
langu kwenye madhabahu hiyo namponda kwa
jina la Yesu.
Wakati mwingine madhabahu
inaweza kuwa siyo kiwanja bali inakuwa kwenye kitu chochote kile, kwa mfano
dada mmoja alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni ya tajiri, siku moja yule dada
akaingia kwenye ofisi ya boss wake na kuona chupa ndogo lakini ndani ya ile
chupa yumo yule dada akiwa hai. Hii inatufundisha kuwa yule dada alikuwa
amelazwa kwenye madhabahu ya yule tajiri , kwa hiyo mafanikio aliyonayo yule
tajiri ni kupitia nyota ya yule dada.
3.0 MAMLAKA TULIYOPEWA NA BWANA WETU YESU KRISTO
Mathayo 10:1, kwa hiyo watu wa Mungu tumepewa mamlaka ya kutamka na
ikawa na leo tunaenda kuzibomoa madhabahu zote kwa jina la Yesu. Mambo hapa
dunia hayatokei yenyewe ila kuna kitu
kinafanywa ili yatokee. Na nguvu ya kufanya mambo yatokee ni uwezo wa
mtu wa Rohoni alionao ndiyo unaleta
matokeo mazuri ya mwilini. Kwenye ulimwengu wa Roho unapotamka kwamba navunja
madhabahu iliyonishikilia mahali popote itakuwa kama utakanyotamka.
4.0 HITIMISHO
4.1 MAOMBI
Kwa damu ya mwanakondoo
naibomoa madhabahu ya wachawi kwa jina la Yesu, mahali popote walipotaja jina
langu napaharibu kwa jina la Yesu, Naibomoa hali ya kuwa kichaa, naibomoa madhabahu ya wendawazimu,naibomoa
madhabahu ya mikosi kwa jina la Yesu. Mtu yeyote aliyenilaza kwenye madhabahu
yake ya utawala leo naondoka na nakataa kubaki pale kwa jina la Yesu na nyota
yangu naimuru ianze kung’aa.
Nakataa watoto wangu ,
kazi yangu, ukoo wangu kuwekwa kwenye madhabahu ya wachawi kwa jina la Yesu.
Naibomoa madhabahu ya kifo, umasikini,uoga na mikosi kwa jina la Yesu.
Imeandikwa Gidion aliwapeleka watumishi wake kumi wakaibomoa madhabahu ya
baali, na sisi watumishi wa Mungu leo tunazibomoa madhabahu zote zilizoshikilia
taifa letu na watu kwa jina la Yesu. Imeandikwa bomoeni bomoeni hadi msingini, leo
nabomoa madhabahu zote, madhabahu ya dhiki, magonjwa, umasikini kwa jina la Yesu.
Nabomoa madhabahu ya shaba, udongo, chuma ,mti kwa jina la Yesu. Nakataa kushikiliwa
kwa jina la Yesu, mtu yeyote anayenicontrol kupitia madhabahu yoyote leo
nakaataa kwa jina la Yesu. Madhabahu ya mabaya iliyoimarishwa naivunja kwa jina
la Yesu, mabaya hayatanipata mimi. Naamuru mizimu, majini, majoka anza kuondoka
kwa maana madhabahu zenu zimebomolewa kwa jina la Yesu. Imeandikwa bwana amenifunga mshipi wa vita, leo nafanya vita na kuziteketeza madhabahu
zote na nawachinja makuhani wote wa hizo madhabahu.
Naivunja madhabahu
inayoninyima promosheni,inayonizuia nisisafari, inayonizuia nizipate pesa kwa
jina la Yesu,. Na kuhani yeyote
aliyenipeleka kwenye hizo madhabahu leo namchinja . Imeandikwa bomoeni bomoeni
hadi msingi leo naenda kubomoa madhabahu za njia panda, porini, bahari .
Nainyamazisha damu iliyomwagwa kwenye madhabahu za wachawi kwa damu ya Yesu.
Ninaamuru kuanzia sasa kila madhabahu inayonena nainyamazisha kwa jina la Yesu.
Kila madhabahu iliyojengwa kwenye nchi ya Tanzania ili kukamata akili na nia za
watanzania leo nakupasua vipanda vipande kwa jina la Yesu. Naamru na roho zote
zilizolazwa kwenye madhabahu zianzae kuamka kwa jina la Yesu. Nakata kamba zote
zinazounganisha watu na madhabahu za wachawi kwa jina la Yesu.
Nakata ashera zote
zilizopandwa kwa majina ya watu kwa jina la Yesu. Nazilaani ashera zote na kuanzia
sasa zianze kukauka kwa jinala Yesu. Nawateka nyara wasimamizi na makuhani wa
madhabahu nawachinja kwa jina la Yesu.
Ewe Mungu wa madhabahu nakukamata na kukuteketeza kabisa na enzi yako yote kwa
jina la Yesu. Leo naamuru mioyo, nafsi, akili na vyote vilivyoshikiliwa
kuachiliwa kwa jina la Yesu. Nauzima moto uliwashwa kwenye madhabahu ya wachawi
ili watu wapate magonjwa, kichaa, umasikini , balaa na mikosi kwa jina la Yesu.
Naibomoa madhabahu iliyojengwa kwenye kichwa, tumbo, kifua kwa jina la Yesu. Naibomoa madhabahu iliyohai
na inayotembea kwa jina la Yesu.
Ufunuo 6:9, kuna roho za watu zinaweza kuwa zimewekwa chini ya
madhabahu. Hata wewe leo unaweza kuwa
hapa lakini roho yako imelazwa kwenye madhabahu, sema leo naivunja madhabahu
iliyonilaza na toka kwa jina la Yesu. Wachawi wa familia wanaweza kumwuuza mtu na kumpeleka alazwe
kwenye madhabahu. Leo naiteketeza hati
ya makubaliano yao ambayo imewekwa kwa jina la Yesu, hati iliyonifanya niuzwe
na nibaki madhabahuni leo naichana na kuiteketeza kabisa kwa kwa jina la Yesu.