UFUFUO NA UZIMA
CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 14.12.2025
ASKOFU BARAKA
THOMAS TEGGE
SOMO: VIKAO VYA
UHARIBIFU
Mambo yote ambayo yanampata mtu inaweza yakawa mema au mabaya yanayoonekana ulimwengu huu, yanatengenezwa kwenye ulimwengu usio onekana (roho) na inatengenezwa na watu ambao hawana mwili. ambao wanakaa kwenye vikao kwenye ulimwengu usio onekana (roho).
“Ndipo Shetani
akamjibu BWANA, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha BWANA bure? Wewe
hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo
navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika
nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye
atakukufuru mbele za uso wako”. Ayubu 1:9-12
Kuna mambo mtu anayapanga
yanaweza kuwa Biashara, kazi, masomo na mambo mengine ambapo mtu amepanga
kufanya. Ila kuna watu wameweka vikao kwenye ulimwengu usioonekana lengo lao ni
kuzuia usilitimize jambo hilo aliopewa na Mungu. Na baada ya muda fulani hilo
tukio litampata mtu katika ulimwengu wa mwili au unaoonekana.
Watu hao wanaopanga
vikao hivyo vya uharibifu kwa kuweka mipango ya muda mrefu ambapo mtu kama
asipo shughulika kwa sasa kuna matukio yanaweza kumpata kwa muda muda ambao
umeamuliwa katika ulimwengu usio onekana.
Watu wengi wanapuuzia
mambo ya rohoni ambapo mtu anaona kuwa hana muda wa kufanya hivyo ndio maana
watu wengi wakuwa wanaishi maisha wasiotaka. Ni kwasababu mtu hajashughulika na
mambo ya rohoni. Ukishughulika na mambo ya rohoni utaweza kuharibu mipango yao.Kuna
mambo mtu amefichwa machoni pake ili asiweze
kujua mipango ya Shetani kuhusu maisha yake.
“Mikaya
akasema, Sikia basi neno la BWANA; Nalimwona BWANA ameketi katika kiti chake
cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kuume na
wa kushoto. BWANA akasema, Ni nani atakayemdanganya Ahabu, ili akwee
Ramoth-Gileadi akaanguke? Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi. Akatoka pepo,
akasimama mbele za BWANA, akasema, Mimi nitamdanganya.”1wafalme 22:19-20
Kuna
watu wanahisi matukio wanayopata ni bahati mbaya ila sio kweli ila kuna mipango
imepangwa kwenye ulimwengu wa roho ambapo wanaweka matukio kwa wakati maalum.
Kuna wakati mtu anaona anacho kifanya ni sahihi ila ni mpango uliwekwa kwenye vikao kwa kutaka kuharibu kusudi la Mungu juu ya mtu huyo vilivyo pangwa kwenye ulimwengu wa roho. Kuna mambo yanaonekana ni sahihi kwa sasa ila baada ya muda fulani yanaleta matokeo mabaya kwa mtu huyo.
Mawazo ni mambo ya
rohoni pale mtu atakapo waza vibaya yataleta matokeo mabaya, kwenye vikao vya
uharifu pia wanaweka. Mawazo ndani ya mtu kama mtu huyo asiposhughulika anaweza
kufanya mambo kupita mawazo ya Shetani na kuharibu kusudi la Mungu kwa maisha
yako.
“Akasema,
Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu
hutoka mawazo mabaya, uasherati,” Marko 7:20-21
Kuna mambo mtu analea Watoto kutokana na Mawazo ya kishetani kuhisi kwa kumlea mtoto hivyo ni sahihi ila lengo la kutaka kuharibu uzao wako. Ni muhimu kushughulika kwenye ulimwengu wa Roho ili kuweza kuvunja vikao vya uharibifu.
Mawazo ndio kitu cha muhimu ambapo kabla mtu ajanza kufanya jambo huwa Mawazo ndio yaanza baada ya hapo yanaleta mtazamo baada ya mtazamo ndipo jambo litatokea.watu wanafanya maamuzi kwa kuongozwa na mtu ambaye hana mwili na yupo katika ulimwengu usioonekana.


0 Comments