IBADA YA KUSIFU NA KUMSHUKURU MUNGU.
03 - 08 – 2014
03 - 08 – 2014
John Lisu |
Ni ibada ya kusifu ambapo waimbaji mbali mbali wapo ndani ya
bonde la kukata maneno Ibada imeanza na kundi la John Lisu wakituumbuza kwa
nyimbo zao nzuri.
Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima:
Tunamshukuru Mungu Kwa
mambo matatu.
1.
Tunamshukuru Mungu kwa Helicopter ambayo imefika
jana tarehe 2-8-14 lengo la kununua hericopiter hii ni kwa ajiri ya kuihubiri
injiri katika mikoa yote kama tulivyoanza na Arusha, Kilimanjaro, Tanga,
Morogoro, kilombero, na sasa tunaanza na Iringa, Njombe, Songea, Mbeya,
Sumbawanga, Katavi, Kigoma, Kagera, Geita, Mara, Simiyu, Shinyanga, Kahama,
Tabora, Singida, Dodoma hapo tutakuwa tumemaliza awamu (phase) ya kwanza. Awamu
ya pili tutakwenda mikoa ya Lindi na Mtwara pamoja na Zanzibar. Baada ya hapo
tutakwenda wilaya zote, Tarafa zote,
kata zote na vijiji vyote.
2.
Mbunge wetu wa kawe alituomba tusaidie shule za
msingi kama kuwapatia madawati na umeme katika shule hizo.
3.
Ni mwaka wa tano tupo hapa kawe hivyo pia
tunamshukuru Mungu kwa hilo.
Wageni wetu rafiki zetu tulionao leo ni
hawa wafuatao:
Faustine Munishi na malebo, Rose Mhando, Tunajivunia vya kwetu ni vizuri kuwatambua watu wangali wakiwa hai. Pia tuna John Lisu, Flora Mbasha, mwanapinduzi, chengula, mabisa ema jacksoni Benti, david Robart,
upenndo nkone, Christina Shusho, Bon Mwaitege, watanzania tuna vitu vizuri tulivyopewa na Mungu, Mahanaimu Soundi hii ni bend mpya (mwanzo 32:1-2)
1 Yakobo akashika
njia yake na malaika wa Mungu wakakutana naye.
2 Naye Yakobo alipowaona, alisema, Hili ni jeshi la Mungu. Akapaita mahali pale, Mahanaimu.
2 Naye Yakobo alipowaona, alisema, Hili ni jeshi la Mungu. Akapaita mahali pale, Mahanaimu.
Serikali tatu ndo msimamo wetu Ufufuo na
uzima maana tunaserikali tata kwa sasa maana sasa tuna serikali ya Zanzibar naya
muungano na ya Tanganyika haipo Hivyo tunahitaji serikali ya Tanganyika nayo
iwepo.
Kama kawaida yetu wimbo wa Tanzania
unaimbwa na bendi yetu ya magereza.
Baada ya hapo Mwenyekiti wa Mtaa wetu ndugu
Hasani Ngonyani naye atusalimie Mheshimiwa mwenyekiti ametaja mwenyewe ipo siku
ataokoka na anawaheshimu sana viongozi wa dini na hivi karibuni ataokoka na
haya yawe kwake kwa jina la yesu.
Rose Mhando naye tunamkaribisha kwa nyimbo
zake. Rose mhando anatoa somo na anasema kumiliki ni haki yetu hivyo
tung’anga’anie kwa Mungu ili atubariki. Rose anasema kwake ni Unabii kwa maana
anasema leo anazindua albamu yake ya kamata pindo la yesu akianzia ndani ya
bonde la kukata maneno kawe kama alivyozindua nibebe miaka ile. Pia anamwambia
mwenyekiti hasani kuwa hajakosea kusema kuwa ataokoka hivyo asiwe na wasiwasi
maana amechagua fungu lililo jema kwani hata yeye alikuwa mwisilamu.
Sasa ni wakati wa kumsikiliza Mbunge wetu
wa jimbo la kawe aseme machache mheshimiwa Halima Mdee mwanamke Jasiri Afrika
kwa maana siku chache hivi karibuni amechaguliwa kuwa mwanamke jasiri kati ya
kumi namoja waliokuwepo kwenye kinyang’anyiro hicho.
Mbunge anamshukuru mchungaji Kiongozi
Josephat Gwajima
Anasema hajazoea kusema neno kwenye
madhabahu hivyo anatetemeka hivyo ananukuu kitabu cha isaya 43:18-19
18 Msiyakumbuke
mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani.
19 Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka.
19 Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka.
Anasema helicopter ni chombo cha gharama nafuu sana na kinawezesha watu wengi
kulipata neno kwenye mikoa yote na vitongoji vyote. Pia anaghusia magazeti ya
udaku na anasema yataandika sana lakini
nyinyi songeni mbele. Na anasema tutaweza kuongeza chombo kingine ili kazi ya
Mungu iendelee mbele. Anasema asante kwa mwitikio wa kanisa la Ufufuo na uzima
kwa kuwapatia madawati wanafunzi wa shule za msingi kawe .
Hatimaye Halima achangia Milioni kumi kwa
kazi ya Mungu katika kuwapatia shule za msingi madawati. Kitu cha msingi kuliko vyote ni kusema
nimepiga hatua. Anasema Mapato ya kinondoni kipindi kile ilikuwa bilioni 9
baada ya miaka 3 yameongezeka mpaka bilioni 40 na wanataka yafikie bilioni 100
ingawa safari ni ndefu lakini kwa uwezo wa Mungu tutashinda.
Kuhusu jimbo tumefanikiwa kupata miradi
mbalimabali, tumejenga Barabara za rami na mambo mengine hata wao wanaamini
neno. Na kwa neno tutafika.
Ameleta tena salaam za majadiliano ya
kuhusu katiba mpya. Kwa mara kwanza ni katiba inayohusisha mawazo na maoni ya
watanzania wote . salamu kutoka Ukawa wanawasalimia wamesema ipo siku chembe chembe ya kuwa na katiba ,
yakutaka kuwa na taifa lenye neema, ya kutaka kuwa na viongozi wazalendo,
yakutaka kuwa na Tanzania mpya itafika. Wao ukawa watarudi mbungeni kama maoni
ya wananchi yataheshimiwa. Mwisho anawaasa watanzania wasiache mchakato
uendeshwe na wanasiasa peke yao hivyo kila Mtanzania ashiliki ili kutoa
mwelekeo wa taifa, wa rasilimali za taifa zigawanywe kwenye mgawanyo halali kwa
wantanzania wote. Tukiwa na katiba bora inayotoa mwongozo bora kwa mgawanyo wa
kweli na watanzania tujidhatiti ili kuokoa kizazi kijacho Mungu awabariki sana! Hayo
Makofi kwa yesu.
Flora Mbasha na wimbo wake wa
utukufu kwa yesu.
Upendo Nkone na wimbo wake usifurahi
Juu yangu ewe adui yangu.
John Lisu apata gari Jipya
"John Lisu ni kama Don Moen wa Tanzania, na ni mtu anayeubariki sana moyo wangu, ni vizuri kujifunza kuwatendea mema watu wa Mungu ambao Mungu anawatumia kuyagusa maisha yetu, na kwasababu John Lisu amekua akitumiwa na Mungu kutugusa kwa namna ya ajabu tunamzawadia gari jipya siku ya leo" Dady Josepha Gwajima
.
Faustine Munishi anaelezea habari za malebo anaeleza kuwa ni rafiki yake wa tangia utotoni walisoma pamoja na walikuwa pamoja na sasa malebo naye ameokoka.
mwanamapinduzi.
SOMO KWA UFUPI:
JINSI MTU ANAVYOWEZA KUIBA NYOTA.
NA MCHUNGAJI KIONGOZI.
MANENO YA MSINGI Mhubili 10:5-9, Ezekieli
13:19-21
Mhubili 10:5-9
5 Liko baa
nililoliona chini ya jua, nalo ni kama kosa litokalo kwake yeye atawalaye;
6 ya kuwa upumbavu huwekwa mahali pa juu sana, nao wakwasi hukaa mahali pa chini.
7 Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa.
6 ya kuwa upumbavu huwekwa mahali pa juu sana, nao wakwasi hukaa mahali pa chini.
7 Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa.
8 Mwenye kuchimba
shimo atatumbukia ndani yake; Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.
9 Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo; Naye apasuaye miti huona hatari katika hiyo.
9 Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo; Naye apasuaye miti huona hatari katika hiyo.
Ezekieli
13:19-21
19 Nanyi mmeninajisi
kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili
kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao
haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo.
20 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege.
21 Na leso zenu nazo nitazirarua, na kuwaokoa watu wangu katika mikono yenu, wala hawatakuwa katika mikono yenu tena kuwindwa; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.
20 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege.
21 Na leso zenu nazo nitazirarua, na kuwaokoa watu wangu katika mikono yenu, wala hawatakuwa katika mikono yenu tena kuwindwa; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.
Hapa anasema kuwa kuna watu ambao
walitakiwa kufa lakini hawajafa na kuna watu waliokufa hawakutakiwa kufa.
Kuna kitu kinaitwa nyota ukisoma kitabu cha
mathayo 1:1-2 kinaandika habali za nyota iliyoonekana mashariki.
1 Yesu alipozaliwa
katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa
mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,
2 Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.
2 Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.
kwa
habari ya nyota tunaweza kujifunza yafuatayo:
1.
Kila mtu
ana nyota
2.
Numbe
nyota inaweza kufuatwa
3.
Nyota ya
mtu inaweza kuonekana.
NYOTA
NI NINI?
Nyota ni ule uwezo au kipawa cha mtu kutenda kazi na uwezo huo unaonekana
kabla hata mtu hajazaliwa
Kuna wengine nyota yao imewekwa kwenye
siasa wengine kwenye utawala na wengine kwenye biashara na kadhalika.
Kuna wengine nyota yao ipo kwenye uso unaweza ukamwangalia tu unampenda au
unataka kuongea nae, wengine darasani wengine biashara.
Shetani hakuumba chochote hivyo kwa
kuwatumia wachawi na waganga kuchukua nyota za watu na kuwapa wengine
wanaoshirikiana nao kwenye mambo ya kishirikina na mtu aliyechukuliwa nyota
yake wanamwachia mapepo na kumwacha na taabu.
Angalizo kila
mwanasiasa ambaye hana Mungu ana mganga wake wa kienyeji hakuna ambaye hayuko
huku wala kule (neutral) hivyo hao
wanaoiba nyota lazima wapigwe kwa jina la Yesu. Sasa mamajusi wa mashariki
Wakaiona nyota, lile neno mamajusi maana yake ni wataalamu wa anga (Astrologers
or Magician) waliotoka mashariki ya mbali ambayo leo ni Uchina na Korea na
sehemu za Japani wakaona nyota ya mfalme amezaliwa mashariki ya kati. Wakaja
kutoa zawadi uvumba na manemane.
Maana yake nini
sasa wale mama jusi wakasafiri mpaka Jerusalemu wakiifuata ile nyota
Ndiyo maana
unaweza ukamuona mtu ni maarufu kumbe ni mtupu tu, ana nyota za watu
Hatuishi kwa
majini wala mapepo hivyo mtu anayesema na kufundisha habari za nyota kwenye
redio na television kama shehe Yahaya huyo mtu anafundisha uchawi hivyo hatufai
mtu huyo.
Kwa dakika hizi
chache nataka kuamuru nyota ya kila mtu irudishwe kwa jina la Yesu.
Wengine wana
nyota za mvuto wengine wana nyota za
kupendwa .
Neno la Mungu ni
nyundo ivunjayo mawe vipande vipande.
Unakuta mtu anatumia nyota za watu anajichukulia umaarufu na kuonekana
ana maana sana kwenye jamii. kwa yule ambaye nyota yake imechukuliwa kama alikuwa anapendwa
anaonekana hapendwi tena.
Kwa
mfano Tanzania yenye Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu kuliko milima yote Afrika, yenye ziwa
kubwa kuliko maziwa yote ulimwenguni na ziwa lenye kina kirefu kuliko yote
afrika na madini ya kila aina halafu leo shule zikose madawati na umeme kwa
nini Tanzania nchi yenye Dhahabu. Hili ni tatizo la akili watu wanashindwa
kutumia mali tulizonazo lakini jiulize Japani hawana chuma lakini ndiyo
wanaongoza kuuza magari.
Tanzania
mpya inakuja kwa jina la yesu.
Tanzania ni nchi
ya watu wote na kiongozi asiyewasaidia watu hawa hafai kuwa kiongozi wetu
nitaendelea kusema ‘’ Tanzania mpya inakuja’’
Unakuta mtu
anahangaika kila siku kumbe wanaitumia nyota yake kwa kazi zao
Kuna aina nne za
mashetani:
1.
Majoka - hawa ni wale malaika waliotupwa kutoka
mbinguni pamoja na shetani
2.
Majini - ni mashetani wanaoendana na mila za
kiarabu
3. Mizimu - ni mashetani yanayofuata familia
ndio maana unakuta familia zina mambo
Yanayofanana.
4.Miungu – Hawa wanatawala
japani na nchi za mashariki ya mbali.
Ulimwengu wa Roho ni dhahili hivyo
shetani anaweza kutumia wachawi na wanganga kufanya kazi yake ya kuuwa na
kuharibu na kuchukua nyota za watu. Nyota ikichukuliwa maisha yako yanaanza
kuharibika hapo, unaanza kitu unaacha wachawi wana uwezo wa kukufanya uache
kazi, biashara familia mke au mme.
Unakuta mtu yule aliyekuwa kilaza
darasani ndo anaamua hatima za watu.
matendo13:16
elimu ni taa ya kumulika mafanikio
katika maisha kulingana na uwezo ambao Mungu amekupa hivyo ni uwezo wa
kuendeleza kipawa chako ulichopewa na mungu maana kuna kitu ulichopewa. Hivyo
kila mtu ana kitu chake ndani ambacho amepewa
UKIRI
‘’Sema nakataa, sema nakataa, sema
nakataa sema tena nakataa’’ kwa nini tunasema nakataa kwa sababu tumeumbwa kwa
mfano wa Mungu hivyo kila tunachosema kinatokea hivyo kila jini kila mzimu unaoshikilia
nyota za watu achia kwa jina la Yesu kila kiongozi wa kisiasa unayetumia nguvu
za kichawi na kung’oa kwa jina la yesu.
maelfu wakiponywa katika shida zao |
Shika kichwa chako sema kwajina la
yesu kuanzia leo aliyeiba nyota yangu nakuitumia awe kiongozi, awe shehe au imamu
rudisha nyota yangu kwa jina la yesu.
Kwajina la yesu natumia uwezo wa
jina la yesu kila mtu aliyeweka mkono wake kichwani na anasoma neno hili
naamuru katika jina yesu naamuru nyota yake irudi kwa jina la yesu.
Sema maneno haya ‘’Baba kwa jina
la yesu naomba leo mahali nilipofungwa unifungue fungua maisha yangu leo’’
‘’Damu ya yesu inifungue sasa kwa
jina la yesu’’.
Nakuamru ewe jini uliye ndani ya
mtu huyu toka kwa jina la yesu.
Yesu yu hai leo wewe jini
unayemshikilia achia mwili wake ewe jini
uliyechukua nyota yake ya kazi, ya kupendwa, ya safari mwachie atembee kwenye
Baraka zake katika jina la yesu naagiza
wewe usitembea tembea usiyesikia sikia usiyeona ona kwa jina la yesu.
Naomba ulinzi kwa watu hawa
walionyosha mikono yao bwana yesu gusa mikono yao. Na kila aliyepanga kukuua
afe yeye kwa jina la yesu naamulu uzima kwa jina la yesu.
1 Comments
jina la Bwana libarikiwe
ReplyDelete