UFUFUO NA UZIMA
CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 27.12.2025
ASKOFU BARAKA
THOMAS TEGGE
SOMO: KULITUMIKIA KUSUDI LA BWANA
KWENYE KIZAZI CHAKO
![]() |
“Mungu, fikira zako zina thamani
nyingi kwangu; Jinsi ilivyo kubwa jumla yake!” Zaburi 139:17
Watu wengi hudhani kumiliki vitu
ni muhimu sana. Mtu anaweza kufanya jambo la kumkosea Mungu, ili tu aweze
kumiliki vitu fulani. Lakini hii ni kwa sababu watu hawatambui kuwa, mtu ni
roho hivyo kila kitu alichonacho kwenye ulimwengu huu atakiacha. Zile mali,
pesa, magari, muonekano na mwili ulionao vyote utaviacha, nawe utarudi ulipotoka.
Nawe utaenda kupeleka ripoti kwa mambo unayoyafanya mbele za Mungu kutokana na kusudi alilokutuma kufanya.
“Na alipokwisha kumwondoa huyo,
akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi,
mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote.” Matendo
13:22
Andko hili linaonesha Mungu humweka
na kumtoa mtu yoyote kwa ajili ya kusudi lake. Kila kitu ambacho Mungu
anakupatia ni ili kitumike kutimiza kusudi lake. Mtu mwenye akili anajua kuwa anaishi
hapa kwa muda tu. Hivyo anatambua kuwa muda wake ni mchache, anafanya mambo
yake yote ili kulitimiza kusudi lake ndani ya muda.
Wakati ukifika wa kuondoka duniani,
utaondoka hata kama bado hujamaliza kusudi la Mungu. Ndomaana Mungu
hutukumbusha kuukomboa wakati. Maisha ni mfano wa mtu ambae yupo kwenye chumba
cha mtihani, muda wakumaliza mtihani ukifika ukiwa umemaliza au haujamaliza lazima
utakusanya na kusubiri matokeo.
“Kwa kila jambo kuna majira yake,Na
wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa
kufa;Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;”Mhubiri 3:1-4
Mungu humchagua yoyote amtakaye
hata kama hafai machoni pa mtu. Kuna nyakati mambo kama vile chuki ama kusalitiwa,
ni mpango wa Mungu ambao ni sehemu ya kutengeneza kwaajili ya kufanya kusudi
lake.
“Nasi twajua ya kuwa katika mambo
yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani,
wale walioitwa kwa kusudi lake.” Warumi 8:18
Ukitaka kuamua mambo usitake
ushauri wa watu, ukishawishika kufanya jambo fulani, lifanye bila kusikiliza
ushauri kutoka kwa watu. Maana kuna ushauri wa watu unakuzuia usilifanye lile
kusudi la Mungu.
“Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka
mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka.” Yohana 6:38
Kuna mambo unatakiwa ufanye jambo
kwa bidii kwa maana ni muda tu, usipoteze kusudi kwa ajili ya mtu, inakubidi
ulifanye kusudi la Mungu kwa bidii ili uweze kuikamilisha mapenzi ya Mungu.
1. Kusudi la Mungu ndio sababu mama
la wewe kuwepo duniani. Ukiwa duniani yapo mambo mengi yakuafanya, ingawa kuna
vitu ukikosa haina shida ila ukishindwa kulifanya kusudi la Mungu ni umepoteza
kila kitu. Kusudi lilitangulia kabla ya wewe kuwepo duniani.
“Kabla sijakuumba katika tumbo
nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa
mataifa.” Yeremia 1:5
2. Kusudi la Mungu halizuiliki,
Mungu hutangaza mwisho wa mtu hata kabla ya mwanzo wake. Mungu akiwa na jambo,
hakuna awezaye kulizuia. Kuna mambo unahisi kwamba ni kikwazo cha kuzuia
usifanye kusudi la Mungu, ila ni Mungu anaruhusu ili liweze kukupeleka kwenye
kusudi la Mungu.
“Wakamwona toka mbali, na kabla
hajawakaribia, wakafanya shauri juu yake ili wamwue. Wakasemezana wao kwa
wao, Tazama, yule bwana wa ndoto anakuja. Haya, twende, tukamwue na
kumtupa katika birika mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha
tutaona zitakuwaje ndoto zake.” Mwanzo 37:18-20
Kupingana na mtu mwenye kusudi la Mungu, ni kupigana na Mungu. Na kila anayepigana na Mungu, hupondwa kabisa. Moja ya sababu ya kifo kabla ya wakati, ni kupingana na kusudi la Mungu juu ya mtu.8\
“Basi sasa nawaambia, Jiepusheni
na watu hawa, waacheni; kwa kuwa shauri hili au kazi hii ikiwa imetoka kwa
binadamu, itavunjwa, 39lakini ikiwa imetoka kwa Mungu hamwezi kuivunja;
msije mkaonekana kuwa mnapigana na Mungu.” Matendo ya mitume 5:38-39


0 Comments