IBADA
YA JUMAPILI YA TAREHE 21-09-2014
NA
MCHUNGAJI KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO:
NGUVU YA MSALABA
Nguvu ya Kanisa imeanzia katika msalaba wa Yesu Kristo ndio
maana utaona kila mahali hapa duniani kuna alama ya msalaba . Kuna maandiko mengi ambapo Yesu Kristo
aliongea kuhusiana na msalaba.
Mathayo
26:4
4 wakafanya shauri pamoja, ili wamkamate Yesu
kwa hila na kumwua.
Mathayo
27:32, 42
32 Hata walipokuwa wakitoka, wakamwona mtu
Mkirene, jina lake Simoni; huyu wakamshurutisha auchukue msalaba wake.
42 Yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa
msalabani, nasi tutamwamini.
Waefeso
2:16
16 Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika
mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba.
Wagalatia
2:14
14 Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya
kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu
umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.
Kimsingi unapoongea ukristo unaongelea mambo makuu matatu
ambayo ni:
Ø Nguvu
ya damu ya Yesu
Ø Kaburi
wazi (Nguvu ya ufufuo)
Ø Maneno aliyoongea Yesu msalabani.
Yesu alipokuwa msalabani akikaribia kukata roho alisema
maneno saba. Kawaida mtu bila kujali alikuwa anaishije anapokaribia kufa huongea
maneno ya maana na yenye uzito sana. Leo tunaangalia maneno saba aliyosema Yesu
wakati anakaribia kufa na umuhimu wake. Lakini je, ni kwa nini alisema maneno
saba wala sio kumi au mia moja?
Haya ni baadhi ya maandiko ambayo yanaonyesha kujirudia kwa
namba saba mara kwa mara katika biblia;
Mwanzo7:2
2 Katika wanyama wote walio safi ujitwalie
saba saba, mume na mke; na katika wanyama wasio safi wawili wawili, mume na
mke.
Nuhu alipotaka kuchinja alichukua wanyama saba
Mwanzo
7:4
4 Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea
dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya
juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali.
Mwanzo21:28
28 Ibrahimu akaweka wana kondoo wa kike saba
peke yao.
29 Abimeleki akamwambia Ibrahimu, Hawa wana kondoo wa kike saba, uliowaweka peke yao, maana yake nini?
30 Akasema, Hawa wana kondoo wa kike saba utawapokea mkononi mwangu, wawe ushuhuda ya kuwa ni mimi niliyekichimba kisima hiki.
29 Abimeleki akamwambia Ibrahimu, Hawa wana kondoo wa kike saba, uliowaweka peke yao, maana yake nini?
30 Akasema, Hawa wana kondoo wa kike saba utawapokea mkononi mwangu, wawe ushuhuda ya kuwa ni mimi niliyekichimba kisima hiki.
Ibrahimu aliwaweka wanakondoo saba kama ushuhuda wa yeye
ndiye aliyekichimba kisima kisichobishaniwa. Namba saba ni namba isiyo
bishaniwa.
Zaburi
119:164
164 Mara saba kila siku nakusifu, Kwa sababu ya
hukumu za haki yako.
Daudi alikuwa anamwabudu Bwana mara saba kwa siku.
Namba saba ni namba ya utimilifu na ukamilifu. Msalaba wa
Yesu Kristo kupitia maneno saba aliyoyasema Yesu akiwa pale ni ishara ya
ukamilifu na utimilifu wa maisha yetu sisi tuaminio habari za msalaba.
MANENO
SABA ALIYOONGEA YESU MSALABANI
1.
MUNGU WANGU MBONA UMENIACHA
Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima |
Watu wengine wanatumia sentensi hii kupotosha kwa kusema
kuwa kama Mungu alimuacha pale msalabani basi sio mwana wa Mungu. Ni kweli aliachwa
kwasababu ya dhambi zetu. Alionekana
mwenye dhambi si kwa kutenda bali kwa kubeba dhambi zetu na baba yake kwa
sababu ya utakatifu wake alimpa mgongo. Alipopigwa magonjwa yako yaliadhibiwa
katika mwili wa Yesu ndio maana Isaya 53:5 inasema kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Yesu
alikataliwa ili sisi tupate kukubaliwa na Mungu baba.
2. BABA
WASAMEHE KWA KUWA HAWAJUI WATENDALO
Wakati Yesu anasema maneno haya alikuwa katikati ya mateso
na maumivu makali lakini bado aliweza kusamehe. Kawaida mtu anapoumizwa
hushindwa kusamehe mara moja; mwingine husema nitasema maumivu yakipoa au mwingine
atakuambia nitakusamehe ila sitakusahau. Kuna watu wamekufa leo na wengine wana
magonjwa yasiyotibika kwa sababu ya kutokusamehe. Unaposhindwa kusamehe Mungu
naye hawezi kukusamehe hivyo sio rahisi kupata uponyaji wako kwa sababu Mungu
huponya baada ya kukusamehe. “Akusamehe dhambi zako zote akuponye magonjwa yako
yote.”
Marko2:
1-5
1 Akaingia Kapernaumu tena, baada ya siku
kadha wa kadha, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani.
2 Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake.
3 Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne.
4 Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza.
5 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
2 Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake.
3 Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne.
4 Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza.
5 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
Biblia inasema
mkiwasamehe wawakoseao na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe, kumbe basi hata
msipowasamehe Baba wa mbinguni hatawasamehe pia. Unapokuwa husamehi kunakuwa na
mapepo yanayopata mwanya kuingia ndani yako na kupandikiza roho ya uchungu
ambayo huzaa presha, magonjwa ya moyo na kisukari.
Waebrania12:1
1 Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na
wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi
ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano
yaliyowekwa mbele yetu,
Ile dhambi ikuzingayo ya kutokusamehe iweke kando. Unapoamua
kusamehe wale mashetani wanaokaa ndani yako wanahama ndani yako na unapona
magonjwa yako yote.
3. AMINI AMINI NAKWAMBIA LEO HII TUTAKUWA WOTE PEPONI
Yesu hakuwa na shaka na alipokuwa anakwenda. Alijua
anakwenda wapi. Yesu alimwambia yule mwizi aliyemwamini pale msalabani kuwa hakika
leo hii tutakuwa wote mbinguni. Msalaba wa Yesu unatupa hakika ya mafanikio
yetu, unatupa uhakika juu ya uwepo wa mbingu na haki yetu ya kuishi huko. Duniani
zimejaa taarifa nyingi za kubahatisha ila wewe uliyeokoka msalaba wa Yesu ni
uhakika wa kwenda mbinguni. Biblia inasema “amini amini nawaambia yeye
aniaminie mimi amepita kuingia mbinguni” Tazama nabisha mlangoni mtu
atakayeisikia sauti yangu na kunikaribisha nitaingia ndani yake na atakuwa na
uzima wa milele. Mbinguni ni kwetu na msalaba wa Yesu kristo ni uhakika wa
kwenda Mbinguni na Yesu ndiye njia, kweli na uzima.
Yohana
14:1
1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini
Mungu, niaminini na mimi.
2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
4 Nami niendako mwaijua njia.
2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
4 Nami niendako mwaijua njia.
Msalaba ni uhakika wa kuolewa kwako, hakika ya promosheni,
hakika ya kazi yako, hakika ya safari
yako, hakika ya maisha yako. Kristo alikuwa na uhakika wa wapi aendako na nini
anaenda kufanya, kuandaa makao kwa ajili yetu.
4. MAMA TAZAMA MWANAO
NA MTOTO TAZAMA MAMA YAKO
YOHANA
19:26-27
26 Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule
mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama,
mwanao.
27 Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake.
27 Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake.
Msalaba unaweza kuleta upatanisho, msalaba ni nguzo ya
upatanishi. Inawezekana kuna migogoro kati yako na ndugu zako au wafanyakazi
wako lakini leo kuna msalaba wa upatanishi. Leo mataifa yanapigana kwasababu
hakuna mapatano, Baba na Mama wanagombana, hawapatani. Yesu alipokuwa msalabani
mkono wake mmoja alimshika Mungu Baba na mkono mwingine akawashika wanadamu
huku akiwa anakata roho akapiga kelele
akisema pataneni! Leo Yesu anaitwa daraja la upatanisho kati ya wanadamu na
Mungu.
5. EE BABA MIKONONI MWAKO NAIWEKA ROHOO YANGU
Kumbe Roho inaweza kuwekwa kwenye mikono, yaweza kuwa ya
Mungu Baba au mungu wa dunia hii ambaye ni shetani. Msalaba wa Yesu kristo
unaweza kukabidhi Roho zetu mikononi mwa Mungu. Yesu akatuonyesha kwamba Roho yake
ameiweka mikononi mwa Mungu Baba. Leo hii Roho za watu ziko kwa wachawi, nyingine ziko
kwa waganga wa kienyeji. Msalaba unatupa uhakika wa mahali pa kuwekwa roho zetu.
Biblia inasema msimwogope yeye awezaye
kuua mwili bali mwogopeni yeye awezaye kuiua Roho na mwili.
6. NAONA KIU
Yohana 19:28
28 Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa
yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.
Ni jambo la kushangaza mtu aliye katika hatua ya kufa kuhitaji maji. Haya maneno hakuwa akiwaambia
wale waliomsulibisha bali baba yake wa
mbinguni; kwamba pamoja na taabu niliyonayo bado ninaona kiu ya kutimiza
mapenzi yako. Yesu alikuwa msalabani tangu asubuhi na hapa alisema, “naona kiu”
Msalaba wa Yesu unatupa kiu ya uponyaji, kufufua, miujiza, utoaji, kufunga,
kuomba. Inawezekana kuna wakati ulikuwa
una kiu ya kuomba lakini leo umekuwa mkavu lakini upo msalaba wa yesu unatupa
kiu ya kuyatimiza mapenzi ya Mungu katika maisha yetu.
7. IMEKWISHA
Yesu hakuuwawa bali
aliitoa Roho yake ili aitwae tena. Shetani hakujua kama Yesu alikuja ili afe ndio
maana aliingia kwa watu wamhukumu kifo lakini. Yesu alikuwa mtii hata mauti ili
atimize mapenzi ya baba yake. Alipokuwa msalabani Yesu aliangalia kama
ametimiza yote yaliyompasa kufanya, akaangalia akaona uponyaji upo, ufufuo upo
na maandiko yote juu yake yametimia ndipo akapiga kelele kusema imekwisha.
Baada ya Yesu kukata roho yakafuatia matukio yafuatayo:
Tukio la kwanza, Dunia yote ikawa Giza. Mungu akazima jua
lake na Dunia ikawa giza “MSALABA NI MSALABA WA MATUKIO”
Tukio la pili, miamba
ikapasuka. Msalaba unapasua miamba. Je, kuna mtu ofisini au kwenye familia yako
amefanyika mwamba? Mkutanishe leo na msalaba wa Yesu wenye uwezo wa kupasua
miamba.
Tukio la tatu, makaburi yakafunguka. Hapo ndipo penye nguvu
ya Ufufuo na Uzima yaani Yesu mwenyewe.
Tukio la nne, dunia
ikatikisika.
Tukio la tano, wanawake wakajipigapiga vifuani wakimaanisha
wanamtafuta Yesu.
Tukio la sita, pazia la hekalu likapasuka maana yake kila
mmoja wetu anayo ruhusa ya kuomba moja kwa moja kwa baba bila kupitia mtu
yoyote.
Tukio la saba, kwenye msalaba pakawekwa anuani maana yake anuani ya mahali
unakoelekea kwa makusudi ya Mungu ipo
msalabani.
Tukio la nane, yule
aliyekuwa anaongoza usulubishaji akasema “hakika mtu huyu alikuwa ni mwana wa
Mungu.”
Tukio la tisa, ilipofika jioni walienda kuwavunja miguu waliosulubiwa
maana kwa sheria ya kiyahudi hairuhusiwi mtu kuwa hai juu ya msalaba sabato
inapoingia. Akiwa hajafa hukatwa miguu ili afe kwa kuishiwa damu. Walikuta Yesu
amekwishakufa lakini mmojawapo wa wale wanajeshi alimchomi mkuki ubavuni ndipo
ilipotoka damu na maji. Hiki ni kithibitisho hakika kuwa Yesu alifia msalabani.
Yesu alipokufa kabla ya kufufuka alikwenda kuzimu ambako
kulikuwa na dhima wakishangilia kumshinda Yesu.Yesu alimfuata shetani palepale kwenye
kiti chake kuzimu akamkanyaga kichwa chake mbele ya malaika zake. Tena zaidi ya
hayo akamnyanganya funguo za kuzimu na mauti.
MAOMBI:
Tunawafuata adui zetu palepale walipo, tunawatokea kwenye
ulimwengu wa Roho na kuwakanyaga na kuwanyanganya mali zetu na vitu vyetu vyote
kwa nguvu ya msalaba wa Yesu kristo.
Kwa jina la Yesu nimepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge
na nguvu zote za yule adui kwa jina la Yesu. Kwa nguvu ya msalaba ninawafuata
wachawi, waganga wa kienyeji na adui zangu wote katika ulimwengu wa roho waliokaa
kikao kinyume na mimi, ninawaponda vichwa kwa jina la Yesu. Imeandikwa
wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo, ninawashinda kwa damu ya Yesu. Ninazikanyaga
mamlaka zote za giza kwa damu ya mwanakondoo. Kwa nguvu ya msalaba, kwa damu ya
mwanakondoo ninawashambulia wote mnaotumia nyota yangu, ninauponda uzao wa joka
katika jina la Yesu. Ninawashambulia mashetani katikati ya uzao wa wanadamu kwa
jina la Yesu. Kwa damu ya mwanakondoo,
ninavifuatilia vipawa vyangu vilivyofichwa katika mashimo kwa jina la Yesu. Ninaitumia
nguvu ya msalaba kwa jina la Yesu, waliofichwa kwenye mashimo, kwenye mapori, baharini,
kwenye mwezi, kwenye, nyota, kwenye anga
ninawarudisha kwa damu ya Yesu. Kwa jina la Yesu Kristo ninaamuru warudishwe,
natumia nguvu ya msalaba kwa damu ya Yesu kristo, biashara zilizofungwa, kazi zilizofungwa
ninazifungua kwa jina la Yesu.
Nakwenda msalabani, msalaba wa furaha, msalaba wa ukombozi,
msalaba wa ushindi, msalaba wa nguvu, msalaba wa maarifa nakata rufaa hapo kwa jina la Yesu.
Asante Bwana Yesu kwa ajili ya kunifia msalabani, asante kwa
ajili ya nguvu iliyomo ndani ya msalaba. Asante kwa ukombozi, uponyaji na
msamaha wako. Amen.
Maelfu wakiwa ndani ya ufufuo na uzima kawe |
Nguvu ya msalaba. |
0 Comments