UFUFUO NA UZIMA
CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 08.03.2026
ASKOFU DKT.GERSHOM
MWAKILA
SOMO:
UNAWEZA KULOGWA BILA WEWE KUJUA
![]() |
Mtu
anaweza kulogwa bila yeye kujua. Mtu anaweza kusema kwamba haamini uchawi,
ingawa hiyo haiondoi kuwa uchawi upo. Kwa sababu biblia inasema kuwa uchawi upo,
basi uchawi upo. Iwe unaamini ama huamini. Biblia inaonesha mtume Paulo alikuwa
anajua ya kuwa uchawi upo na kuwa mtu anaweza kulogwa.
“Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga,
ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?”
Wagalatia 3:1
Ibilisi
hakutendei mabaya kwasababu umemkosea, ila anakutendea kwa kukuonea maana ni
asili yake kuonea watu. Ndio maana Yesu akaja
ili kutuweka mbali na uonevu wa Ibilisi.
Namna wachawi wanavyoweza kuloga watu
1.Unaweza
kulogwa kwa kuzuiwa
Unaweza
kufanya mambo yako kwa bidii lakini hupati mafanikio. Ni kwasababu wachawi wanazuia
usipate baraka zako. Zipo mamlaka za rohoni ambazo kazi yao ni kuzuia mafanikio
yako.
“Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo,
mara ya kwanza, na mara ya pili, na Shetani akatuzuia.”1Wathesalonike 2:18
2.Unaweza
kulogwa kwa kulazwa usingzi
Katika
sayansi, mtu anapolazwa usingizi wanalenga kukata kitu wakitoe au kuweka kitu ndani
ya mtu. Mfano mtu mwenye uvimbe tumboni anapoenda kufanyiwa oparesheni,
wanakuchoma sindano ya usingizi na baada ya mtu kuamka anakuta uvimbe huo umeondolewa.
Sayansi hii hata kwenye biblia imetumika. Mfano Mungu alimpa Adamu usingizi na
akachukua ubavu wake na kumtengeneza mwanamke.
“BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye
akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,” Mwanzo
2:21
Wachawi
nawao wanapo loga mtu, wanasubiri mtu huyo alale usingizi ili waweze kupanda
mbegu za matatizo na uharibifu ndani ya mtu. Wachawi wakikulaza wanaondoa kila
kitu ambacho umepewa na Mungu. Wanafanya hivyo ukiwa umelala au wamekulaza
usingizi. Nyuma ya kila tatizo ulionalo kuna kitu kimewekwa na wachawi au
kimeondolewa ndani ya mtu.
3.
Unaweza kulogwa ili ufe
Shetani
anamipango ya uharibifu juu ya mtu na ana hila juu ya watu wa Mungu. Wachawi
wanapotosha njia za Bwana kwa kufanya jambo zuri lionekane kuwa baya, ama wanapamba
jambo baya lionekane zuri. Lengo nikusababisha mtu aweze kupita kwenye njia ya
mauti. Usiende kwenye njia ambayo sio sahihi hata kama njia hiyo inafatwa na watu
wengi. Ukiwa kwenye njia ya haki, hata kama ukiwa peke yako utashinda maana
Bwana anakuwa pamoja na wewe.
“Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga
hila za Shetani.” Wefeso 6:11,
Kuna mambo kwenye maisha yako yalipaswa kuwa yameshafanikiwa, lakini mambo hayo yamekufa. Na yule ambaye mambo yake yalipaswa yawe yamekufa, mambo yake yamefanikiwa kwa kuwa ameiba mafanikio yako kichawi. Mfano, unakuta mtu amevaa pete au bangiri ambazo si za urembo, bali ni zana za kishetani kwaajili ya kufanikisha mambo yake.


0 Comments