Bishop Dr. Josephat Gwajima
AMETUMWA KUKUCHELEWESHA
Jumapili,17.01.2021
Biblia
inasema Mungu ametupa miaka sabini na wenye nguvu sana amewapa miaka themanini.Mwili
wa mwanadamu unaukomo hivyo ulipotoka mbinguni umepewa maono na mission ya
kukamilisha hapa duniani, your work is to complete your God given mission.
Imeshaamuliwa kutoka mbinguni wewe utakuwa nani, sasa kuna watu wametumwa
kukuchelewesha watakusema vibaya, watakusongasonga lakini usikate tamaa wewe
songa mbele.
Upendo
hauchoki huvumilia yote . Upendo haupo kwenye vitu, ni afadhali uoe au uolewe
na mtu ambaye hana kitu lakini ana uhusiano mzuri na Mungu, Mungu atawabariki
na utakuwasehemu ya Baraka hizo. Don’t look at material things to be a factor
for you to be married to that person, it’s better to be part of the blessings.
Tatizo
litakalo kufanya usishinde ni kuangalia shida yako na kujitazama mwenyewe,
ukiangalia mawimbi utazama; unachopaswa kutazama ni kusudi la Mungu ndani yako.
Conviction is an inner assurance that even when
your all five senses nor your mind doesn’t sense its presence but you keep on
feeling that it will happen. It’s an art that no matter how many punch I
received that distorted my face still the match isn’t over yet, I can WIN. If
you feel the conviction do it, don’t wait. If you’re led by an inner conviction
things are going to be possible. Taking a risk is not risk but not taking a
risk is the greatest risk.
·
Philipians 4:12 ‘ I can do all things through Christ who strengthens me.’
·
Hesabu
14:11 ‘Kisha Mwenyezi-Mungu alimwambia
Musa, “Watu hawa watanidharau mpaka lini? Na, mpaka lini wataendelea
kutoniamini, hata pamoja na miujiza yote niliyotenda kati yao?’
-Ukiwasikiliza
watu wenye hali halisi utafia kwenye eneo hilohilo wakati wanao sikiliza
ushawishi watafika kwenye nchi ya ahadi.
Lazima
ujue ukitaka kupata jambo yakupasa kupigana ili umiliki au ukipate. Kwa maana
biblia inasema Kwa maana kushindana kwetu
sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa
giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.’ Kumbe
ni lazima ujue kupigana kwanza. Unaweza ukawa ni mtu lakini ukaingiziwa nia ya
kishetani alafu unaitenda kazi ya shetani, mtu kama huyu anapokuja kwenye
maisha yako anakuchelewesha kwenda kwenye hatima yako kwasababu amebeba nia ya
shetani ndani yake. Jinsi unavyojisikia ndivyo ulivyoitiwa, shetani akijua
unayo hatima kubwa lazima atume wakala wake wakucheleweshe. Kila hatima ya mtu imepimwa.
·
Waefeso
5:15 ‘Basi, muwe waangalifu jinsi
mnavyoishi. Msiishi kama wapumbavu, bali kama wenye hekima.’
·
Yohana
1:29-36 ‘Kesho yake Yohana alimwona Yesu
akimjia akasema, “Tazameni! Huyu ndiye
Mwana-Kondoo wa Mungu anayeondoa dhambi ya ulimwengu! Huyu
ndiye niliyewaambia kwamba, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi kwa
maana alikuwapo kabla sijazaliwa.’ Mimi mwenyewe
sikumfahamu, lakini nimekuja nikibatiza kwa maji kusudi apate kufahamika kwa
watu wa Israeli.”
Kisha Yohana akatoa ushuhuda huu:
“Nilimwona Roho akish uka kutoka mbinguni kama hua, akakaa juu yake. Mimi
nisingem tambua, lakini Mungu ambaye alinituma nibatize watu kwa maji ali kuwa
ameniambia kwamba, ‘Yule mtu utakayemwona Roho akimshukia kutoka mbinguni na
kukaa juu yake, huyo ndiye atakayebatiza kwa Roho Mtakatifu.’ Mimi
nimeona jambo hili na ninashuhudia kuwa huyu ndiye Mwana wa Mungu.”Kesho
yake, Yohana alikuwapo pale pamoja na wanafunzi wake
wawili. Alipomwona Yesu akipita, alisema, “Tazameni! Mwana-Kondoo wa
Mungu!”
Shetani
hawezi kuzuia hatima yako ila anaweza kukuchelewesha; na ndio maana yatupasa
sisi kuomba kwa bidii. Wapo watu ambao hatima zao zimecheleshwa na shetani,
Ukisoma Biblia unamuona Mariam Magdalena alijazwa mapepo lakini hatima yake
ilikuwa yeye kuja kuwa mwinjilisti wa kwanza duniani ndivyo na maisha yetu kila
siku yalivyo kwamba kuna mahali muda huu tulitakiwa kuwepo na sio hapa tulipo kwasababu
ya shetani na mawakala wake.
To
overcome any obstacle in a physical realm must first overcome in the spiritual
realm. What you sow in the spiritual realm will be reaped in the physical
realm.
BONYEZA HAPA👇👇 KUANGALIA
IBADA NZIMA YA LEO JUMAPILI
0 Comments