google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

VITA VYA HATIMA -- SEHEMU YA PILI

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 19 MEI 2024
ASKOFU DR JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: VITA VYA HATIMA - SEHEMU YA PILI

Hatima ni Mungu anafanya kazi kupitia UTU wa mtu. Kila mtu ana hatima yake na inajulikana kuwa mtu huyu atakuwa nani. Imani ni kujiita sawasawa na hatima yako.

“Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu." Kutoka 17:9

“Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima."Kutoka 17:10

Ndugu yako wa mwilini ana uhusiano mkubwa na hatima yako. Shetani anaweza kumtumia ndugu yako wa mwilini kuhakikisha haufanikiwi lakini vivyo hivyo Mungu anaweza kumtumia ndugu yako wa mwilini kukufikisha kwenye hatima yako.

“Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda.” Kutoka 17:11

Hata kama umechoka lakini kazi ya Mungu LAZIMA iendelee. Mungu alitaka Musa aweke mkono wake juu bila kushusha ili washinde vita. Mungu hakuwa anawaza kuwa atachoka maana kazi lazima iendelee ili Joshua aweze  kushinda vita. 

"Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga. 14BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu." Kutoka 17:14

Winning a spiritual battle is a combination of men and women praying for you, people singing and praising God. Ushindi wa vita ni muunganiko wa vitu vingi sana.

Amaleki ni watu wa aina gani?

Wana wa Israeli walipokuwa wanatoka Misri wakiwa njiani wakakutana na waamaleki, "wakawaambia tunapita tu hatupiti kwenye mashamba yenu, hatutakunywa maji au matunda yenu" lakini wao wakakataa na wakatuma jeshi kuwazuia bila sababu yoyte.

Siri ya kunena kwa lugha ni kwamba unaweza ukawa unaombea hata adui zako ukiwa unanena.

Amaleki ni nani kwa siku ya leo?

Amaleki ni mtu anayezuia wewe kufika katika hatima yako. Kila mtu anaye amaleki katika Maisha yake anaweza kuwa kuolewa na wewe, kukuoa, yupo kazini, shuleni au kwenye familia lakini kama waamaleki walivyofutwa na hao wa Maisha yako pia wafute. 

"BWANA akamwambia Musa, Njoo huku juu kwangu mlimani, uwe huku; nami nitakupa mbao za mawe na ile sheria na hiyo amri niliyoiandika ili uwafundishe. Musa akaondoka na Yoshua, mtumishi wake, Musa akapanda mlimani kwa Mungu." Kutoka 24:12

Mungu hakumwambia Musa aje na mtu lakini hatima ya Joshua imeungamanishwa na Musa, Musa alivutiwa na Joshua lakini ni kwasababu ya hatima yake. Fanya vitu ambavyo vitakufanya wewe uwavutie watumishi wa Mungu ili wakukumbuke katika mambo mengine.

Joshua anatoka kwenye kabila la Ephraim. Ephraim ni moja wapo wa kabila 12 za Israel lakini sio mtoto wa Yakobo, ni Mjukuu wa Yakobo.

 “Israeli akamwambia Yusufu, Sikudhani ya kwamba nitakuona uso wako, na Mungu amenionyesha na uzao wako pia. 12Yusufu akawatoa katika magoti yake, naye akainama kifudifudi 13Yusufu akawaweka wote wawili, Efraimu katika mkono wake wa kuume, kuelekea mkono wa kushoto wa Israeli; na Manase katika mkono wake wa kushoto, kuelekea mkono wa kuume wa Israeli, akawasogeza karibu naye. 14Israeli akanyosha mkono wake wa kuume akauweka juu ya kichwa cha Efraimu, aliyekuwa mdogo, na mkono wake wa kushoto akauweka juu ya kichwa cha Manase, huku akijua atiavyo mikono; maana Manase ndiye aliyezaliwa kwanza.” Mwanzo 48:11-15

“Yusufu alipoona kwamba babaye anaweka mkono wake wa kuume juu ya kichwa cha Efraimu, ikawa vibaya machoni pake. Akauinua mkono wa babaye auondoe katika kichwa cha Efraimu, ili auweke juu ya kichwa cha Manase. 18Yusufu akamwambia babaye, Sivyo, babangu, maana huyu ni mzaliwa wa kwanza; weka mkono wako wa kuume kichwani pake. 19Babaye akakataa, akasema, Najua, mwanangu najua, yeye naye atakuwa taifa, yeye naye atakuwa mkuu; lakini ndugu yake mdogo atakuwa mkubwa kuliko yeye, na uzao wake watakuwa wingi wa mataifa.” Kutoka 48:17-19

 “Na wana wa Efraimu; Shuthela, na mwanawe huyo ni Beredi, na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Ekada, na mwanawe huyo ni Tahathi; 21na mwanawe huyo ni Zabadi, na mwanawe huyo ni Shuthela; na Ezeri na Ekadi, ambao watu wa Gathi, wenyeji wa nchi, waliwaua, kwa sababu walishuka ili kuzipokonya ng’ombe zao. 22Na Efraimu, baba yao, akaomboleza siku nyingi, wakaja nduguze ili kumfariji. 23Naye akamwingilia mkewe, naye akachukua mimba na kuzaa mwana, akamwita jina lake Beria, kwa sababu mna mabaya nyumbani mwake. 24Na binti yake alikuwa Sheera, ambaye alijenga Beth-horoni, wa chini na wa juu, na Uzen-sheera. 25Mwanawe ni Refa, na Reshefu, na mwanawe huyo ni Tela, na mwanawe huyo ni Tahani; 26na mwanawe huyo ni Ladani, na mwanawe huyo ni Amihudi, na mwanawe huyo ni Elishama; 27na mwanawe huyo ni Nuni, na mwanawe huyo ni Yoshua.” 1 Nyakati 7:20

Kuna mambo ambayo utaona yataonekana ni makosa kumbe ina maana. Kama vile Yakobo alivyoweka mkono wa kuume katika kichwa cha Ephraim badala ya Manase maana yeye ni wa kwanza kuzaliwa. 

BONYEZA LINK HII KUTAZAMA IBADA NZIMA YA JUMAPILI


Post a Comment

0 Comments